GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 5,406
- 7,386
Haya ni miongoni mwa "mauozo" machache:
1. Kiwanja kimoja kumilikishwa kwa watu zaidi ya mmoja
2. Wamiliki halali wa rdhi kupokonywa maeneo yao kinyemela
3. Shamba au kiwanja kimoja kuuzwa kwa zaidi ya mtu mmoja.
4. Watu kuuziwa mashamba/viwanja hewa
Wauzaji wa viwanja hewa, kwa mfano, hujitapa kuwa hata wakishtakiwa, kesi itakuwa ya madai na kwamba kesi ya madai haimfungi mtu. Hujidai kuwa hata wakiamriwa na mahakama kurejesha fedha walizotapeli, wanaweza watajipangia kurejesha kwa awamu, na kila awamu itakuwa ni kiasi kidogo sana. Ndiyo kusema, atahakikisha anarejesha kiasi ambacho hakitamwathiri sana (tapeli) na hakitamnufaisha anayelipwa.
Hiyo inatoa picha gani? Sheria ni dhaifu? Hali ikoje kwa nchi zingine kama Rwanda, China na Botswana?