Jerry Slaa amejitolea pesa kufungua kesi ya madai kusaidia wananchi waliobomolewa nyumba kinyume na Sheria

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
17,804
27,363
Salaam, Shalom!!

Ndugu Respis Brasius mkazi wa Unga Limited ameahirisha kujitoa uhai wake baada ya kuvutiwa na hotuba ya ndugu Jerry Slaa aliyoitoa Bungeni kuhusu utatuzi wa migogoro ya Ardhi.

Iko hivi, Don Mmoja Unga Limited alishinda case mwaka 2012 iliyohusu baadhi ya wananchi kuvamia kiwanja chake Cha biashara, execution ya HUKUMU hiyo ikaja kutekelezwa mwaka 2023, Mahakama iliruhusu brokers kubomoa nyumba zote zilizokuwa zimejengwa kwenye kiwanja Cha tajiri huyo sawasawa na mipaka husika.

Kitu Cha ajabu kilichojitokeza ni kuwa, tajiri huyo akanyosha mkono Kwa brokers wakabomoa nyumba zilizokuwa ndani ya kiwanja husika, na wakabomoa nyumba zingine nyingi tu ambazo hazikuwa kwenye eneo husika ambalo tajiri huyo alishinda kesi.

Ndugu Brasius baada ya kubomolewa nyumba yake isivyo halali, alipoteza dira ya maisha, anadai alipanga na alikwisha andaa Sumu ambayo angeibwia jumapili hii, lakini kabla ya kujimaliza, alipanga atafute silaha Ili akammalize tajiri huyo Kisha arudi kujimaliza mwenyewe.

Tunajifunza kuwa, kumbe utendaji mbovu wa watumishi wa Serikali unaweza kusababisha vifo vya kabla ya wakati Kwa waliodhulumiwa, pia vinaweza kusababisha magonjwa ya moyo nk nk.

Ndugu huyo ametamka hadharani kuwa atakwenda kutubu Kanisani Kwa dhambi ya kudhamiria kujitoa uhai na kumaliza wengine.

Ndugu Slaa amejitolea pesa, kufungua kesi ya madai kusaidia wananchi waliobomolewa nyumba kinyume na Sheria, Ili kiwanja Cha tajiri kiuzwe na Mali zake Ili kujenga nyumba UPYA za Wana chi zilizobomolewa.

Sitakupongeza ndugu Slaa sababu uyafanyayo ni sehemu ya majukumu Yako, na waliosababisha UOVU huo ni viongozi chini Yako, ila itoshe kusema, natambua uwepo wako katika wizara ya Ardhi.

Mungu Mbariki na kumlinda waziri Jerry Slaa.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿. Amen

Source: Habari Mpya TV.

Karibuni🙏
 
Kumbe dhuluma kwenye ardhi, zinaweza kuzalisha Majambazi wa kutumia silaha mtaani kama ilivyotokea Kwa Hamza, yule kada wa CCM!!

Watumishi wa umma hakikisheni HAKI inatendeka,

Ogopeni RUSHWA.
 
Back
Top Bottom