Sheria ya salamu ya "Shikamoo"

Sasa kwa tafsiri hyo ya hilo neno......kuna utumwa gani unaouona ndani yake?
Ndio maana nikasema, hata kusema "good morning" wakati una lugha yako bado ni utumwa, inaonyesha kiasi gani waafrika tupo dependant kwa waliotutawala, iwe kidini au kijamii.
 
Kuna mtu nilimuambiaga "umeshindaje" akajibu kwa penalti

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Shikamoo si salam ya kiungwana,wala haina maana ya heshima bali ni salam ya kitwana. Ni salaam iliyokuwa ikitumiwa na watumwa enzi ya ukoloni wa waarabu kuonyesha utii kwa master. In fact hata waarab hawatumii hii (shikamoo) ambayo sisis tunaona kama ni heshima. Shikamoo maana yake ni 'Niko chini ya miguu yako'
 
Shikamooo ni utumwaaa

Ova
 
Swali muhimu kuliko yote..
Ulifanikisha mchakato wa kupata mke bila kutoa shikamoo kwa shemeji!?
Au walikutilia ngumu mkuu.
Walinipa tena hata sikumaliza mahari (ila siku ya kwanza kwa kuweka heshima na kuogopa kunyang'anywa mke ukizingatia ni siku ya utambulisho nilimwamkia, nikampiga biti Zito awe ananiamkia mi sio mdogo kwake kuanzia hapo akawa ananiamki daily)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wewe acha ukuda kwani salamu nani amekuambia ni lazima useme shikamoo, hata kama ulikua mbali nae si ungepunga mkono tu, tatzio vijana wa siku hizi mnadharau sana, unajua salamu haiombwi lakini kuna muda unaitaka kabisa ili kuona heshima ipo...
 
Sasa mambo gani haya ya kumwambia MTU "nipo chini ya miguu yako"
 
Hahahahahaaaa basi hyo mila na desturi ni ya hatari kuliko zote.....mkoa gani huo aisee
 
Na wewe acha ukuda kwani salamu nani amekuambia ni lazima useme shikamoo, hata kama ulikua mbali nae si ungepunga mkono tu, tatzio vijana wa siku hizi mnadharau sana, unajua salamu haiombwi lakini kuna muda unaitaka kabisa ili kuona heshima ipo...
Daah mwanangu ukuda gn bhana mtu yupo mbali kabisa....
 
Hiyo issue shikamoo,umenikumbusha kipindi hicho ndio nimekuja Mwanza, niliwakuta wazee wa kabila kisukuma wamekaa wengi wengi wanaongea story zao, mie sasa nikawaamkia "SHIKAMOONI WAZEE", wale wazee wakaniangalia kwa dharau na mshangao, na mie nikawashangaa. Wakaniita, wee binti hebu njoo hapa, nilivyofika wakanihoji "SISI UMETUONA NI TENGA LA NYANYA ETI?" nikamuuliza kwanini mzee unasema hivyo? akajibu "hivi sisi unaweza kutupatia shikamoo ya jumla kwa wote?"

Kumbe walitaka niwasalimie mmoja mmoja, tena kwa kupiga magoti, kwa mfano:

1. Shikamoo Mzee Mabula
2. Shikamoo Mzee Manoni
3. Shikamoo Mzee Mpuya
4. Shikamoo Mzee Masanja

yaani hadi wote waishe kila mmoja na shikamoo yake, tena kwa kumtaja jina!!!! (ukiwa umepiga magoti)
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…