Sheria ya kumpa mimba mwanafunzi wa chuo!

uhalali wa mahusiano hauanzii tu mtu (binti) anapofikisha umri wa miaka 18 na kuendelea, mfahamu kuwa sheria bado zinakataza kuwa na mahusiano na mwanafunzi hata kama ana zaidi ya miaka 18, issue ni mwanafunzi yupi?

wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanalindwa na sheria kwa yoyote atakaye kuwa ana mahusiano ya kimapenzi, atakaye wapa ujauzito na kuoa na ifahamike hili ni kosa la jinai ambalo adhabu yake ni 30 yrs hata kama yupo above 18.

zaidi ya hapo, kama ni chuo, itategemea na sheria za chuo hicho hasa kwa vyuo vya awali (colleges) vyuo vikuu havina hizo sheria zinazozuia mahusiano ya kimapenzi. vyuo kama Butimba teachers college, ambacho wanafunzi wanalelewa kama sekondari naweza kuamini kuwa suala la mimba ni kosa, maana pale hawaruhusiwi hata kutoka nje, na uniform wanavaa kwa hiyo nashawishika kuwa kuna vyuo vingi kama hivi vyenye sheria zinazobana mahusiano.

Ni jinsi gani unaweza shitakiwa hapa,
Umempa ujauzito binti wa chuo cha awali ngazi ya cheti, kwa namna moja utakuwa umeingilia mwenendo wake wa kimasomo hata kupelekea kushindwa kuendelea na chuo wakati wa ujauzito au mara anapojifungua na kuanza kumlea mtoto, hapa wazazi au ndugu, au binti mwenyewe ana/wanaweza kukupeleka mahakamani kwa kosa la madai, wanaweza tengeneza madai ya aina yoyote ile yatakayotokana na ujauzito huo.

Na mfahamu ya kwamba, kesi za madai zinaweza kukufunga.
 
Back
Top Bottom