Miongozo ya utunzaji wa Kadet isipauke haraka

Mimi nina kadeti tatu zina zaidi ya miaka 3. Masharti hayo siyafuati, lakini bado ziko bomba, isipokuwa moja ndio imeanza kupauka.

NB: Kadeti hizi nilinunua kitambaa dukani na kushonesha kwa fundi.
Duh, kitambaa cha kadert dukani mkuu?
 
Shida rangi labda, kadet nyeusi au blue au dam ya mzee kupauka jadi ila kaki utasotea miaka hata 5.
 
Weka na aina ya kadet pia

Kuna grades za 45,000 or 55,000 kwenda juu hazina hayo masharti
Mkuu kama hutojali naomba bland na jina ya kuzitambua quality ya hizo bei maana mtu anaweza kukuuzia cardet kwa 55k alafu ukifua kama umechemsha. Chainizi
 
Izo kadeti ambazo huwezi rusha mateke ni izo kadeti za kumi Na nane Na kariakoo ni 13 Kwa jumla lakini kadeti zenyewe huwa zinakua Zinavutika
Na mimi najua cardet za ciku hiz ni stretcherble za zaman zile. Ngum ndo ulikuwa msala inachanika kama umemwagia maji ya betri
 
Hii ni miongozo kwa wanaopenda kuvaa kadeti, fanya haya ili isipauke mapema.

☆Tumia sabuni ya kipande unapoifua usitumie sabuni ya unga

☆Igeuze nje ndani unapoifua

☆Usiianike kwenye jua anika kwenye kimvuli

☆Usiipige pasi ikibidi ipige ikiwa imegeuzwa

☆Usiiloweke muda mrefu kwenye maji

☆Usiikamue maji unapoianika iache ikiwa na maji

☆Usitumie maji chumvi katika kufua

Hizo ni baadhi ya sheria chache kati ya nyingi, kuifanya nguo yako isichakae mapema
Nawasilisha ndugu zangu.

Nimejitahidi kufuata masharti hayo lkn wapi!,Kadeti zangu zimepauka zote.
 
Nguo nazo zina masharti yake jinsi ya kutumia ili zisipauke
Nyingine zinaandikwa do not bleach
Usianike kwenye labda 30 degree c
 
Back
Top Bottom