Sheria juu ya ndoa hii inasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria juu ya ndoa hii inasemaje?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by gregsanga, Oct 18, 2012.

 1. g

  gregsanga Member

  #1
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 80
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  wana jamii habari za leo?
  kuna ndugu mmoja alioa miaka 7 iliyopita kwa ndoa ya kanisaniakaishi na mkewe kwa kipindi cha miaka minne.baada ya hapo kukaanza matatizo katika ndoa hiyo ambayo alipelekea ugomvi wa kawaida kati ya wana ndoa wakafikia hatua wakapigana siku hiyo. binti akaamua aende kwao wazazi wakamshauri ampeleke mumewe polisi huku nyuma yule binti baada ya kumpeleka mumewe polisi akarejea nyumbani na kubeba kula kitu ndani ya nyumba na kuacha nyeupe akaacha ujumbe kuwa kuazia leo kila mtu aishi kwake na mimi ninarudi kwetu. wazazi wa binti hawakuchukua hatua yoyote juu ya ujio wa binti yao wa miaka miwili walikaa kimya mume nae akaishi muda wote akisubiri pengine wazazi wangeweza kuchukua hatua ya kuita watoto wale na kushauri kilichotokea hakukuwa na hatua yoyote miaka miwili ilipopita yule mume akaamua kufunga ndoa na mwanamke mwingine miezi michache baadae wazazi wale pamoja na binti wakamtafuta yule mume kutaka suluhu na pengine kumpa talaka mke wa kwanza. kumtaka mume awajibike na malezi ya watoto na matumizi ya mke wa kwanza ambaye bado anaishi kwa wazazi wake. je sheria inasemaje kwenye hili tujaribu kumshauri ndugu yetu huyu? katika kipindi chote hiki mume alikuwa haruhusiwi hata kuona watoto.
   
 2. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Aisee wewe kweli ulikimbia jee sasa umerudi rasmi? tangia 2007 una post tatu tu!!!!!
  Haya watu wa sheria karibuni, ila mimi ningependa kuuliza jee wazee wa mwanaume wao walitoa wazo gani mda wote
  huo? na jee huyo mwanaume alikwenda kuwaona wazee wa mji au viongozi wa kanisa aliko fungia ndoa?
   
 3. S

  Sir M.D.Andrew JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Miaka miwili bila mawasiliano haimaanishi kuwa ndoa imevunjika,impliedly inaweza kuitwa SEPARATION,yaani muda wanandoa wanakaa tofauti,haimaanishi taraka hata kidogo,kwa mpango huo kesi ipelekwe kwa m'kiti wa mtaa/kitongoji,awaandikie barua ya kufungua kesi ya kudai taraka,kabla ya mahakama kuitoa itaangalia maisha ya baadaye ya watoto pamoja na mgawanyo wa mali mliyochuma pamoja:naomba kama sijakupata sawa uniandikie namba zako hapa halafu nikutafute kwa ushauri zaidi
   
 4. NGOGO CHINAVACH

  NGOGO CHINAVACH Verified User

  #4
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 797
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  unasema ndoa ya kanisani wewe ni dhehebu gan, watoto wanamiaka mingap. kitaratibu ndoa huvunjika inapotoka talaka hivyo huwez kuoa wakati upo kwenye ndoa unless wakati unafunga ndoa yako na mke wa kwanza mlikuwa na intention iwe ndoa ya wake wengi, fuata utaratibu upate talaka wakati unafile petition for divorce omba custody of children na uonyeshe kwamba unaweza kuwalea(mahakama inatumia welfare principle of the children), pia kama kuna mali omba equal division of matrimonial property kama mali mlizichuma kipind cha ndoa.
  N.B
  Kama hamna talaka kwa ndoa yako ya kwanza then ndoa ya pili haitambuliki kisheria
   
 5. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  sheria za ndoa za nchi ni tofauti kwa Mlutheri na Mlokole?
   
 6. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndio maana waislam wana ndoa nne moja ikizingua tatu zinazamini pambano

  Mnajidai mkoana hakuna kuachana uku vijumba vidogo vya kumwaga mkizinguana ile akondoa mguu mwengine huyo

  Ushauri kwa ndoa za kigalatia,,Peleka shauri kwa wazazi wako ili wakutane na wazazi wa mwenzako mtatue tatizo
   
 7. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jibu ndio sheria tofauti...Kwanza unatakiwa kujua kwa nini ukawa Mlutherani
  ..................................Na ni kitu gani kinakufanya ukwa mlokole,,,au Utajijuaje wewe ni Mlokole sio kulilia ovyo ovyo
   
 8. g

  gongolamboto JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 509
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Hata nyie mnaoa wake wanne bado mna vinyumba vidogo kibao? Halafu wake wanne bado hamuwezi kuwatunza. Full matatizo
   
 9. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  sheria ya ndoa ni moja ila kwa masuala ya talaka kabla hamjaenda mahakaman kudai talaka lazima uanze marriage counciliation board
   
 10. NGOGO CHINAVACH

  NGOGO CHINAVACH Verified User

  #10
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 797
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  sheria ya ndoa ni moja LAW OF MARRIAGE ACT ila ufungaji wa ndoa ndiyo tofauti. kwa masuala ya talaka lazima uanze marriage conciliation board. Mimi ni muislamu hivyo naanza Bakwata kwa wakristo sijui maana huwa nasikia baba paroko, mchungaji ila kwa kifupi nenda kwenye lile kanisa kwa mtu aliyewafungisha ndoa kwa upatanishi akishindwa atoe taarifa rasmi ya maandishi kwamba kashindwa halafu hiyo taarifa ndiyo mnaenda nayo mahakamani. Nadhani hapo utakuwa umeelewa kwanini nimemuuliza dhehebu lake maana wewe umefunga ndoa kwenye kanisa lakilokole hauwezi kwenda kwa ajili ya upatanishi kwenye kanisa la mlutheran
  N.B
  Kaeni chini nyie wanandoa pamoja na wazai wenu myatatue
   
 11. S

  Sir M.D.Andrew JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tatizo la hapa watu wako makini ni hoja ambazo hazilengi kutatua tatizo la mtu,malumbano ya hoja ambazo si za msingi hapa..cha msingi ndugu yangu kama wewe ni mkristo hiyo ndoa ya pili ni void ab initio yaani hakuna ndoa kabisa sababu umeingia kwenye contract of marriage while there is an existing marriage,file petition ya divorce,omba mahakama ikupe ruhusa ya kulea wanao-child custody na pia mgawane kile mlichochuma by joint effort inaitwa matrimonial properties ambapo mara nyingi mahakama hutumia precedent case ya BI HAWA MOHAMED V,...SEIF pamoja na mambo mengine mahakama ilisema kuwa,hata kukaa nyumbani kwa mwanamke na kutunza familia inahesabiwa kuwa ni mchango ktk uchumi wa familia,hivyo mwanamke anayo haki kupata sehemu ya mali mlizonazo,zaidi ndugu yangu sheria ya ndoa (R:E 2002)it sets out rights and duties of married couples after divorce including children welfare-best interest of children:ahsante sana
   
 12. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Okay, kwa hiyo uwe Mkatoliki, Mujahidina, M-Sunni, Mpaganani, Mlokole, M-Shiite na dini ya kienyeji wote kwa sheria moja ya nchi, kabla ya kwenda mahakamani, ni lazima uanze kwenye bodi ya upatanishi!

  Kwa hiyo hoja yako ya kumbana mtu ambae hakutaja dini was moot, haikuwa na sababu, haina nguvu, it is useless and meaning kutaja dini yako kwa sababu kila kiumbe, Tanzania, kinachotaka talaka, lazima kianzie bodi ya upatanishi.

  Counciliation ndio nini?
   
 13. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  sasa mtu kaomba msaada wa ushauri wa kisheria ina maana hana taaluma ya sheria, wanataaluma mmekuja na kuanza kutumia maneno ya kisheria ambayo yanaongeza tatito badala ya kulimaliza. tumieni kiswahili rahisi au kingereza rahisi kilichotafsiriwa
   
 14. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,746
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Kwanza ndoa hiyo ya pili ni batili(void) kwani huwezi kufunga ndoa nyingine kabla ya kuvunja ndoa ya kwanza hasa kwa wakristo. Inge kuwa kwa muislam ingekuwa hakuna tatizo.

  Kisheria huyo mke wa pili hatambuliki anaye tambulika ni mke wa kwanza.

  Swala la kuona mtoto ni haki yake sababu watoto ni wake pia, hivyo asafishe kwanza tatizo lake la ndoa hili aweze kudai haki yake vizuri.

   
 15. NGOGO CHINAVACH

  NGOGO CHINAVACH Verified User

  #15
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 797
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  1. rekebisha hapo kwenye bluu haileti maana.
  2. hiyo si councilliation board ilitakiwa kuwa conciliation board.
  3. Nadhani huelewi umuhimu wa kujua dini ya mtu kwenye mambo ya talaka. kabla hujamshaur mtu kwenda bodi ya upatanishi ni lazima ujue dini yake ili uweze kujua una mshauri ni kwenye bodi gani ya upatanishi aende. kuna bodi za upatanishi nyingi ambazo zimetambuliwa na waziri wa sheria ambazo zimepewa nguvu kisheria ili ziweze kusuluhisha mambo ya talaka, mfano Bakwata. sasa wewe hujui mtu dini gani utamshaur vipi aende Bakwata?
   
 16. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Utamshauri aende kwenye bodi ya upatanishi ya dini yake. Yeyote ile. Si lazima ujue dini yake.
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Wazazi wanahusikaje kwenye hili, ndoa ni makubaliano kati ya mume na mke. Wazazi walihusika wakati wa kupokea mahari tu, kama ilikuwepo that is, otherwise ni jukumu lao kuweka mahusiano yao sawa.

  Ukishafikia umri wa kuoa/kuolewa wewe ni mtu mzima huhitaji mwongozo wa wazazi.
   
 18. NGOGO CHINAVACH

  NGOGO CHINAVACH Verified User

  #18
  Oct 21, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 797
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  ndugu nadhani unapoaamua kumsaidia mtu kiushauri unabidi utoe ushauri wakujenga na usiyokuwa na utata wala maswali yoyote. Pia naomba ujue kwamba siyo watu wote uenda kwenye bodi za upatanishi za kidini. Yeye kaomba ushauri ni lazima uulize maswali ili ufahamu utaanzia wapi kumshuri mtu. Sasa unamwambia mtu nenda kwenye bodi ya upatanisho kutokana na dini yako, we unadhani umemshauri vya kutosha huyo mtu?mimi sikufundishwa kwa hela za walipa kodi wa Tanzania so that i can render partial legal service ila kutoa legal service kwa uelewa na moyo wangu wote ndiyo maana nauliza hayo maswali, kama maswali yamemkwanza muomba ushauri samahani
   
 19. Viva89

  Viva89 JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 1,224
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  kwanza,hii ndoa ya pili ni void kabisaaa,haitambuliki kisheria meaning kisheria mke wako wa kwanza ndio anayetambulika kuwa wife wako,kama unataka kuachana rasmi nae,divorce inahusika..yeye si ndio aliondoka from the marital home,tena for 2years,file for divorce petition,kuhusu watoto,hata kama hukuwaona,its your duty kuwalea,toa maintainance charges utakazoambiwa ukienda court.lakini pia mbona umechelewa,ungetafuta suluhisho la kisheria mapema,sana sana kuhusu watoto kwa sababu ni wako pia,hatakiwi kukukatalia kuwaona,umelala sana ndugu yangu
   
Loading...