Sherehe za miaka 48 ya Muungano 2012

Ni raha sana kuona hivi vikosi wanavyopita hapa mbele kwa mwendo wa kawaida na kasi.
 
Mbona mistar ilikua imenyooka jaman,au ni askari wa kenya ndo wanaozungumziwa hapa?
 
hawa maafande kesho utasikia hawajalipwa posho za gwaride.
 
nipo nafuatilia kwa ukaribu sana....ila kuna kitu kimenichanganya...
wakati rais anakagua vikosi.....kuna jamaa mmoja amevaa suti alikuwa nae anapita pita zig zag ....huyu ni nani hasa....? mbona sijawahi kumuona tena siku nyingine....? kazi yake pale ilikuwa ni nini...? kwa sababu rais alikuwa amefuatana na wanajeshi wawili tayari
......

swali zuri sana hili...rejao atakujibu punde si punde...
 
hawa watoto mwakajana walidhumiwa pesa nakumbuka ni kule kigoma kama sikosei.
 
Hawa vijana wa halaiki nimewapenda sana. Wamefanyiwa maandalizi mazuri
 
hawa vijana nimewapenda hofu yangu watachakachuliwa tu na ccm.
 
hawa vijana nimewapenda hofu yangu watachakachuliwa tu na ccm.
Wasiwasi wa nini mkuu? Wazazi wenye akili siku hiz mtoto akianza tu shule anatafutiwa kadi ya CCM. CCm ndio kila kitu TZ hii
 
Hiyo ni signal tosha kwa serikali kuwa wanajeshi siku hizi wana mgomo baridi. Huo ndo ukweli. Uzalendo jeshini ulishakwisha siku nyingi. Watu wanataka maisha bora. Utakula magwaride? wanajeshi wanamchukia kikwete kama nini sijui.
 
Hatufuatilii ng'oo.hakuna jipya hapo..wanaohudhuria wengi wanapigwa p/diem zao so wananufaika na mfumo.KAMA WANGEKUWA HAWALIPANI POSHO SHEREHE ZA MAADHIMISHO YOYOTE YANGEFUTWA SIKU NYINGI.
 
Wasiwasi wa nini mkuu? Wazazi wenye akili siku hiz mtoto akianza tu shule anatafutiwa kadi ya CCM. CCm ndio kila kitu TZ hii

wapi huko mkuu.? Hii mpya hata enzi za mwalimu haikuepo.!
 
Kuna mdanganyika nimekaa naye hapa eti anasema nchi imeendelea sana kisa hii show watoto wa halaiki.
Hapo wadanganyika wamerizika kabisa hata kumshinikiza waziri mkuu kujiuzuru na madudu ya mawaziri wameshasahau.Burudani kwa kodi yako inaendelea enjoy umelipia hiyo show.
 
Angalia maadhimisho ya miaka 48 ya Muungano kwenye TV Live halafu utoe maoni yako.
 
Leo ni Sikukuu ya Muungano. Lakini hebu tujiulize ni muungano baina ya nchi gani?

1. Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
2. Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
3. Tanganyika na Zanzibar.

Kwa jibu lolote baina ya majibu matatu,Tafadhali toa Sababu.

Bazazi ni Bazazi.
 
Back
Top Bottom