Sherehe za harusi/ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sherehe za harusi/ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by M'Jr, Sep 24, 2012.

 1. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Kumekuwa na na wimbi la mashindano kwenye ukubwa wa sherehe za harusi (send off, reception, kitchen parties) ambazo nyingi zimekuwa zinategemea sana michango mbalimbali ya watu. Sasa je nini umuhimu wa shere hizi kubwa na za kifahari? Je zina umuhimu wowote na uimara wa ndoa inayofungwa? Kama bado hujaoa/kuolewa unataka ya kwako iweje? Na kama tayari umeoa/kuolewa je yako iilikuwaje?

  Nimesemanhaya coz now it seems like one of my normal monthly bill kama zingine,
  1. Bill ya umeme
  2. Bill ya maji,
  3. Kodi ya nyumba,
  4. DSTV nao wanataka hela yao kila mwezi,
  5. michango ya harusi kila mwezi,
  6. Pesa ya kuhonga,
  7. N.K........Khaaa nachoka asee
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Pesa ya kuhonga?
  Anyway. kimsingi ukubwa wa sherehe hauna uhusiano wowote na kudumu kwa ndoa.
  Ila kwa uzoefu wangu watu ambao wanacomplicate ukubwa wa sherehe wala sio wanandoa, mara nyingi wapambe, ndugu jamaa na marafiki(ambao ndio wachangiaji wa pesa za sherehe) ndio hu'determine ukubwa wa sherehe.
   
 3. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  hivi huwa mnaweka na bajeti ya kuhonga kwa mwezi?kha!ahsante sana mama yangu kwa kunizaa mwanamke!
   
 4. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Michango ni moja ya shughuli za kijamii, kacha kuchangia ije siku na wewe una shughuri utaona umhimu wake.
   
 5. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,856
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  me like this!
   
 6. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Shughuli hazina umuhimu....ni jadi ambao tumeweka sisi au tumezikopy kwa mataifa mengine. Kama kuna ulazima wa sherehe iwe ya kawaida na sio kufuru wapi kwenye vitabu vya dini vimesema lazima ifanywe sherehe.

  Nilishawahi kupiga ban suala la michango, so stress free.
   
 7. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Nini role ya wahusika wenyewe (Muoaji kwenye reception na muolewaji kwenye send off) katika kuamua shughuli yake itakuwaje?
   
 8. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Nimewahi kuwatch sinema nyingi sana za ulaya na marekani zenye harusi ndani yake na i tend to like them, they are simple na nyingi zinafanyika hapo hapo home na watu wanasherehekea kwa muda mfupi (kama ni lazima) then wanasambaa. Huku kwetu mpaka watu wakamuane weeeee kha! Hapa nina kadi za zaidi ya 200,000 si watanilaza njaa hawa haki ya nani?
   
 9. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  sherehe kubwa inatia heshima kubwa mjini mkuu.....na ukizingatia most cases it happens once a time in lifetime.....
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  naongea kutokana na uzoefu wangu. mimi wakati naoa kwanza sikutaka ifanyike sherehe na kama ingebidi nilitaka ifanyike sherehe simple sana lakini nilipata upinzani mkubwa sana kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki mpaka mwisho wa siku ikafanyika sherehe.
  So unaweza ukaona muoaji/muolewaji wana nafasi kubwa juu ya sherehe yao lakini ndugu nao wanaushawishi mkubwa zaidi.
  All in all kama muoaji ataweka 'huruma' pembeni na kuwa na msimamo thabiti bila kujali kama atawaudhi ndugu, akitaka sherehe (kubwa) isifanyike, haiwezi kufanyika.
   
 11. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Umesahau kibao kata, bridal shower etc...
   
 12. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Heshima gani wakati mtu anakaa Gombolamboto harusi anaenda kufanya Jangwani see breeze Kunduchi, majirani zake hawana hata kianzio cha mchango so hawahudhurii. Wanakuja watu wa kazini ambao wengi hata mshahara wako wanaujua, sasa utawatisha nini watu wanaojua kipato chako?
   
 13. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Kaka nimeielewa hii kwa kina sana na nimeiexperience pia baada ya kuanza kuhudhuria kwenye kamati za Harusi. But headache wanayoipata kwenye kutafuta michango made me hate the whole thing
   
 14. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Hahahahaaa ile wanayocheza "kanga moko"
   
 15. unknown animal

  unknown animal JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hapo kwenye kuhonga mjumbe we are not together
   
 16. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Nyinyi achen masikhara, yaan wamama wa mjini wakubali kufanya sherehe za watoto wao...bila shangwe wapi na wapi?

  Mama anachangisha watu wake ofisin na vikundi alivyopo, unakuta mzee nae anasapotiwa na washkaji zake kwenye mihangaiko, kijana nae anachangisha washkji zake job na xul mates bila kusahau sister nae anachangisha mashost hapo harus lazima iwe kubwa tu hata kama bwana harus hutaki iwe kubwa,,

  Yaan mtoto wa town primary umepiga olimpio, forodhan, bunge, muhimbili etc yaan downtown uolewe au uoe kimya kimya,, hutakua hujatendea haki marafiki hata kama hutaki..

  Lazima watu wale, wacheze na wafurah kukuaga kamanda kwenye kwenye chama la mabachelor

  Michango muhimu sema unachanga kwa mtu uliye karibu nae sana to show some love
   
 17. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mkuu hayo ni matumiuzi ya kawaida ya mwanaume. Kuna ambao wanahonga ila wenyewe hawajui kuwa wanahonga...
   
 18. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Dah yaani umetaja shule zote hizo umesahau shule yangu? Ushindi Primary School pale Maiko cheni!
   
 19. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hiyo ndiyo sera yangu. i dont let down my people but I dont entertain kuchangia mtu ambaye hata sirname yake siijui!!!
   
 20. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Tena hao wasiojua kama wanahonga ndio wanahonga kweli kweli, keep records of everything you do (every transaction you do)
   
Loading...