Shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee

Shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee

Mkuu, nadhan hilo swala ni dogo sana endapo ukiamua shirikisha akili kidogo

Huko mnakotembea wakat wa kwenda kazini na kurudi ni muda mzuri sana wa kujadili mambo ya maisha, hasa yakwake yeye, usije mwambia direct "Hama" utaleta ugomvi, unaweza ongea nae indirect ukamfungua akili kwa kumchallenge kwa maswali mtego ya hapa na pale, baada ya muda atajielewa na yeye mwenyewe ataanza kukuambia habari za kutaka kuondoka akapange

Pengine huenda hata yeye anawaza kuondoka ila anawasiwasi, hv nikiondoka watanifikiriaje, ama wataanza maneno kupata tu kazi basi nikajiona nishapata kila kitu na kuondoka, so changamoto za ujana n nying sana, na kuhusu kaka yake, inategemea wakoje, kama hawako karibu sana usidhan itakua rahisi kaka mtu kumwambia mdogo mtu, na pengine unaweza ukute mdogo mtu anatabiwa ya kutafsiri mambo in negative way, unamwambia jambo kwa nia nzuri tu na kwafaida yake, ila akili yake inatafsiri, wamenichoka, wamenifukuza, kaka kazidiwa akili na mkewe, so kaka mtu anakwepa

Nenda nae taratibu, usimchoke, mm niliwah kidgo kuondoka nyumban, nikiwa na miaka 20, at first wazee walifurah mtoto kaenda jitegemea, ila sasa... nilikaa mwaka na kidgo sijarud wala simu hakuna, na tunaishi mkoa mmoja, mwaka jana mwshon ndio nimeanza rud home, alafu nikaja gundua nilikua nafanya ujinga mno, zote hizo n changamoto za ujana, mtu anakua hajui n lipi sahihi kwake kufanya
 
Lakini Jana si tuliyamaliza pale sebulen na jamaa alikubali kupanga
 
Muite,Muulize kwanza anaplan gani na maisha yake maana huwenda ikawa ye anahic anachokifanya ni sahihi hvy bila kumwambia hawez jua,ongea nae vizur kana kwamba unampa ushaur yeye saiz ameshakuwa muda c mref atakuwa baba mwambie tu kwa upole ili ajue kwamba unafanya hvy kwa faida yake
Huwenda ikawa hapati mtu wa kumshaur

Usimchoke huyo ni ndugu wa mumeo mvumilie tu
Ushaur mzur sana
 
Habari wana jamvini,

Niende moja kwa moja kwenye hoja kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Mimi nimekaa na shemeji yangu toka yupo sekondari, amemaliza sekondari kamaliza chuo na ni nimemsaidia kapata kazi na analipwa milioni 2 na sasa kamaliza master.

Ila huyu shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee na mimi nahisi nimemchoka jamani, mpaka lifti asubuhi kazini nampa na mwacha kazini na jioni nampitia na hana aibu na kishoka mbele anakaa kwa kweli mimi nimemchoka kabisa.

Ila kumwambia ndo siwezi, na nikijaribu kumchomekea kaka ake naona ananipotezea hapa nafikiria nimwambie live shemeji kapange sababu kwakweli nahisi nimemchoka kama fadhira nimeshamfanyia.

Au nyie wanawake wenzangu mnawavumiliaga mpaka na kuozesha mnawaozesha? Hata mkate wenyewe kununua hanunui ela yake anajua mwenyewe inakoishia, mimi hata asiponunua sina shida ila shida yangu sasa ni haondoke akapange. Mimi kwa upande wangu sina hata ndugu yangu ninaye kaa nae na hajawai kukaa.

Kwakweli bwana shemeji nimekuchoka, na nyie mashemeji mlioko humu mnaokaa kwa kaka zenu siyo mnakaa kama mmefika mwisho wa reli.
Jifanye umejisahau siku moja unapita sebuleni na chupi tu bila kitu kwenye maziwa wakiwa kaka na mdogo wake wamekaa wanaangalia tv, unapita sebuleni mpaka jikoni unachukua maji ya kunywa unarudi chumbani.
 
hahaha iyo sitaki kufanya
 
Habari wana jamvini,

Niende moja kwa moja kwenye hoja kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Mimi nimekaa na shemeji yangu toka yupo sekondari, amemaliza sekondari kamaliza chuo na ni nimemsaidia kapata kazi na analipwa milioni 2 na sasa kamaliza master.

Ila huyu shemeji yangu hataki kuhama nyumbani akajitegemee na mimi nahisi nimemchoka jamani, mpaka lifti asubuhi kazini nampa na mwacha kazini na jioni nampitia na hana aibu na kishoka mbele anakaa kwa kweli mimi nimemchoka kabisa.

Ila kumwambia ndo siwezi, na nikijaribu kumchomekea kaka ake naona ananipotezea hapa nafikiria nimwambie live shemeji kapange sababu kwakweli nahisi nimemchoka kama fadhira nimeshamfanyia.

Au nyie wanawake wenzangu mnawavumiliaga mpaka na kuozesha mnawaozesha? Hata mkate wenyewe kununua hanunui ela yake anajua mwenyewe inakoishia, mimi hata asiponunua sina shida ila shida yangu sasa ni haondoke akapange. Mimi kwa upande wangu sina hata ndugu yangu ninaye kaa nae na hajawai kukaa.

Kwakweli bwana shemeji nimekuchoka, na nyie mashemeji mlioko humu mnaokaa kwa kaka zenu siyo mnakaa kama mmefika mwisho wa reli.
Tuma namba yake hapa tukusaidie kumwambia ahame akajitegemee,ukitupa tu namba na wewe ukae kimya uendelee tu na hizo ratiba za kumbeba na kumrudisha,muda c mrefu utaona anaanza mwenyewe kusema sema anataka kuondoka n ataondoka.leta namba tumwabie maneno ya kiume sisi asituaibishe bana.mwanaume kugangamala

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Back
Top Bottom