SHEKHE Ang’aka; Asema CHADEMA si Chama cha Wakristo

SHEKHE Ang’aka; Asema CHADEMA si Chama cha Wakristo

Status
Not open for further replies.

Azizi Mussa

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2012
Posts
9,198
Reaction score
7,539
SHEKHE wa Msikiti wa Nunge Dodoma, Shabani Kitilla, amewang'akia watawala na Viongozi wanaopotosha ukweli, akipinga kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) si Chama cha Kikristo, Kikabila au Kiukanda.


Kitilla alisema hayo jana slipohojiana na Gazeti hili, alipotakiwa kutoa msimamo wake kuhusu vurugu zinazodaiwa za kidini zinaoendelea kutokea nchini, yakiwemo matamko ya wanasiasa wanaoshindana kisera, na Mwingine akishindwa anadai Chama cha mwenzake ni cha Kidini, Kikabila na Kiukanda.

Akijibu Maswali, Kitilla alisema, Kama Viongozi wa Dini wanavyowafahamu waumini wanaozingatia Ibada za Dini zao, Ndivyo tunavyovifahamu Vyama na Wanasiasa walivyo, maana Wahusika hao ni waumini wetu; Lakini CHADEMA si Chama cha Wakristo na kinavyotajwa, mbona wamo na Wa-Islamu?.

"Kama Chadema ni cha Kikristo, Kikabila na Kikanda, Basi Msajili wa Vyama kabla ya kushitakiwa kuachia Ngazi maana alikiuka Sheria za kusajili Vyama na amekiacha kikue katia Uongo huu hadi kinakuwa na Wabunge 48" alisema Kitilla akisisitiza, Waislamu na makabila mengine waliomo ni nani?.

Aliongeza kusema, Uongo huo ndio uliopandwa kwa Chama cha Wananchi (CUF) ukaota, ukamwagiliwa mpaka mavuno yakavunwa kwa sababu kilikuwa kinaimalika.leo tena Uongo uleule ndio unaotaka kutumika kuwapumbaza watanzania. Ninachoamini, mtu hadanganywi mara Mbili.; Viongozi waache!

Kuhusu Udini alisema, "Tunapougua na kuhitaji damu tunauliza ni ya Dini ya Kikristo au Mu- Islamu? Je Hewa tunayovuta tunauliza kama ni ya Mkristo au Mu-Islamu? Nawashauri Wakristo na Wa-Islamu wasidanganywe, Amani yetu ikatoweka kwa sababu ya watu wachache wenye Uroho wa Madaraka.

Aidha Kitilla aliyetaja namba zake 0754-512347 alidai, anawamatafuta Viongozi wakuu wa CHADEMA wasio Wakristo Mbunge Said Arfi, Zitto Kabwe (MP), Prof. Abdalah Safari, Halima Mdee (MP), Hamad Yusuph, Issa Mohamed na wengine ili awaulize M4C kuna udini? Wakisema hakuna atajiunga huko!

My take;Wote kwa pamoja tukijitahidi kuwa wakweli tutaweza kusonga mbele.
 
Mbona unatukumbusha movie ya zamani? Ukabila na udini tumeshaziona na ya ugaidi ilikuwa juzijuzi tu.,sasa hivi nimesahau tunaangalia movie gani... Aaaaah ya Lema na binti wa UK.
Thanx Mwigulu kwa kunipa something to watch kila siku
 
Bora huyu kaliona hili maaana vijana makini CCM wameisha wamebaki mazuzu tu,kwanza hawaja jibu maswali ya mh.Tundu Lissu ni lini CUF imeacha kuwa chama kiislamu wenye msimamo mkali??na ni lini CHADEMA imeacha kuwa chama cha wakatoliki???
 
SHEKHE wa Msikiti wa Nunge Dodoma, Shabani Kitilla, amewang'akia watawala na Viongozi wanaopotosha ukweli, akipinga kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) si Chama cha Kikristo, Kikabila au Kiukanda......

Hauhitaji kuwa na degree kujua CHADEMA ni chama cha udini, ukabila na ukanda. Huyu, shehe ni wale wanao nunuliwa na CHADEMA ili kuondoa hili doa, km walivyo fanya kwa Prof. Safari. Kwa hili la udini CHADEMA haisafishiki hata chembe hata mlete thread ngapi humu ndani.
 
Huyu sio Sekhe ni Shehena..hawa wapo wengi tu ni jukumu letu kuwatambua anatafuta ulaji huyo!
 
Hauhitaji kuwa na degree kujua CDM ni chama cha udini, ukabila na ukanda. Huyu, shehe ni wale wanao nunuliwa na cdm ili kuondoa hili doa, km walivyo fanya kwa Prof. Safari. Kwa hili la udini cdm haisafishiki hata chembe hata mlete thread ngapi humu ndani.

Shehe anauzwa shilingi ngapi nami nimnunue?
 
Well!
Hayo ni maoni na msimamo wake binafsi!

...CHADEMA kama wakitaka wanaweza kufanya survey kujua kati ya Waislamu kumi ni wangapi wanaiona CHADEMA kuwa ni ya Wakristo.
 
Mbona unatukumbusha movie ya zamani? Ukabila na udini tumeshaziona na ya ugaidi ilikuwa juzijuzi tu.,sasa hivi nimesahau tunaangalia movie gani... Aaaaah ya Lema na binti wa UK.
Thanx Mwigulu kwa kunipa something to watch kila siku


Kuna thread Mwigulu anasema karudi na mbinu mpya, ngoja tutege masikio, usijekuta next victim ni wewe!
 
Well said, hizo propaganda zao tulishazizoea, asante shehe kwa kulitambua hili.
 
Hauhitaji kuwa na degree kujua CDM ni chama cha udini, ukabila na ukanda. Huyu, shehe ni wale wanao nunuliwa na cdm ili kuondoa hili doa, km walivyo fanya kwa Prof. Safari. Kwa hili la udini cdm haisafishiki hata chembe hata mlete thread ngapi humu ndani.
Mkuu Igunga tuliona Shekhe akiamuru waislamu wasipigie kura CHADEMA, wenye akili wanaona nani mdini hapo.



Dar es Salaam tulishukudia vipeperushi na vikaratasi vilivyokuwa vinampigia kura mgombea wa CCM kwa vigezo vya dini. Watu wamchague kwa kuwa ni muislamu, na wakiwaambia waumini kuwa kuchagua muislamu ni Jihad.

attachment.php




CCM haijawahi kuzikataa kampeni hizo, na wala haijawahi kuzikemea.

Kama huo sio Udini ni nini?
 
Last edited by a moderator:
Hata CCM wakisema nini nimeshafanya maamuzi teyari ni nani nitampigia kura 2015 bora uzima.
 
Hauhitaji kuwa na degree kujua CDM ni chama cha udini, ukabila na ukanda. Huyu, shehe ni wale wanao nunuliwa na cdm ili kuondoa hili doa, km walivyo fanya kwa Prof. Safari. Kwa hili la udini cdm haisafishiki hata chembe hata mlete thread ngapi humu ndani.

Inaelekea unaushahidi "duniani mpaka mbinguni"
msomi wa ilmu dunia na ilmu akhera professor Abdallah Safari atii "amenunuliwa!!!!!!"
kama vipi itungwe sheria ya kuzuia kununuliwa (iwe kosa la jinai lisilo na dhamana) hoja ipelekwe bungeni kibinafsi na ama lusinde au Mwigulu Nchemba
 
Last edited by a moderator:
kuna haja sasa itungwe sheria juu ya elimu ya viongozi wa dini? maana matatizo mengi kama haya ni elimu duni.
Usiende huko FUSO utawaudhi watawala!

Maana maneno yako ni sawa na kusema Mufti wa BAKWATA awe na ilmu akhera na dunia kitu ambacho kitawaletea maslahi makubwa Waislamu, na hilo ni kosa kubwa nchi hii.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom