SHEKHE Ang’aka; Asema CHADEMA si Chama cha Wakristo

SHEKHE Ang’aka; Asema CHADEMA si Chama cha Wakristo

Status
Not open for further replies.
Hauhitaji kuwa na degree kujua CHADEMA ni chama cha udini, ukabila na ukanda. Huyu, shehe ni wale wanao nunuliwa na CHADEMA ili kuondoa hili doa, km walivyo fanya kwa Prof. Safari. Kwa hili la udini CHADEMA haisafishiki hata chembe hata mlete thread ngapi humu ndani.

SHEKHE wa Msikiti wa Nunge Dodoma, Shabani Kitilla, Hapo tu ameshajionesha alikotokea na ushabiki wake upo wapi asitake kubisha kwani Yeye asiwang'akie Viongozi ila aseme ukweli tu kuwa Ngozi ikiwambwa huvutwa ...Ndugu yake Kitilla au Mkumbo au mnyiramba yeyote ni lazima amtetee SIASA NI MCHEZO MCHAFU NA MGUMU
.
 
kwani ndugu yangu Selemani wewe ujuavyo udini ni nini? je! unadhani udini ni kitu kuzuri? je! unafahamu sifa za mtu anayeweza kugombea urais nchini kwa mujibu wa sheria? je! unadhani sheria za uchaguzi zina mapungufu na zinahitaji marekebisho?

Ukweli ni kwamba, waislam wengi wa nchi hii hawawezi kumchagua Padre mstaafu. Hawawezi kusema hadharani, lakini mioyoni mwao ndio wanavyowaza.

Na kama Slaa angekuwa Imam wa Kiislam au Sheikh aliyestaafu mwenye PhD ya Islamic Law basi nina uhakika wakristo wasingemchagua.

These are the realities, na ndio maana Slaa kamwe hataweza kuwa rais wa nchi hii.
 
Watanzania tuache unafiki.Ni ukweli usiopingika ya kwamba wanachama na wapenzi wengi wa CHADEMA in Wakristo kama ilivyo kwa wanachama wapenzi wengi wa CUF in Waislamu.

Ushauri wangu kwa Watanzania Wakristo wote wahamie CHADEMA na Waislamu wote wahamie CUF baada ya hapo CCM itakuwa imekufa kifo cha kawaida kwani itakuwa imebakiwa na wapagani tu,na tutakuwa tumebakiwa na vyama viwili vikubwa vya Kidini hapa Tanzani,yaani:
  • CHADEMA ya Wakristo
  • CUF ya Waislmu

Ukifanyika uchaguzi ndio utatoa majibu magumu waliyokimbia JK na timu yake wakati wa sensa 2012,nani wengi Waislamu au Wakristo?
Mkuu chukua
Like japo ya kichina
 
Ukweli ni kwamba, waislam wengi wa nchi hii hawawezi kumchagua Padre mstaafu.
mkuu kuna utafiti wa kitaalamu umefanya ili tuweze ku share data?Na kama ndio hivyo unadhani ni utaratibu sahihi na wakutamanika hivyo kila mwenye nia njema anatakiwa aupigie chapuo, au ni utaratibu mbaya hivyo inabidi kupingwa na watu wote?
Hawawezi kusema hadharani, lakini mioyoni mwao ndio wanavyowaza.
Sasa kama hawawezi kusema wazi, wewe umejuaje yaliyo ndani ya mioyo yao? mbona mimi nijuavyo anayejua yaliyoko ndani ya nyoyo za wanadamu ni Mwenyezimungu pekee (au uelewa wangu huu si sahihi! tusaidiane bwana.)
Na kama Slaa angekuwa Imam wa Kiislam au Sheikh aliyestaafu mwenye PhD ya Islamic Law basi nina uhakika wakristo wasingemchagua.
Sasa mkuu wewe hili unaweza kulijua je hata ukawa na uhakika licha ya wewe kutumia neno "angekuwa"Je kwa hili nalo unautafiti (na kama unao wewe unaweza kutusaidi kwa mambo mengi kwa kuwa unaweza hata kuwa na taarifa za vitu ambavyo havipo na ukawa na uhakika navyo).

-Je unadhani ni sahihi kwa mtu mwenye dini (yoyote ile) kugombea uongozi?
These are the realities,
Huwa ni vigezo gani wewe hutumia kuujua ukweli?
na ndio maana Slaa kamwe hataweza kuwa rais wa nchi hii.
je? unataka kusema mtu asiyekuwa wa dini yako hawezi kuwa kiongozi wa nchi hii (kwa maana ni wa dini yako tu wanaofaa kuwa viongozi) je! huoni huu ni ubaguzi na ubaguzi ni tabia isiyokuwa ya kiungwana?
 
SHEKHE wa Msikiti wa Nunge Dodoma, Shabani Kitilla, amewang'akia watawala na Viongozi wanaopotosha ukweli, akipinga kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) si Chama cha Kikristo, Kikabila au Kiukanda.


Kitilla alisema hayo jana slipohojiana na Gazeti hili, alipotakiwa kutoa msimamo wake kuhusu vurugu zinazodaiwa za kidini zinaoendelea kutokea nchini, yakiwemo matamko ya wanasiasa wanaoshindana kisera, na Mwingine akishindwa anadai Chama cha mwenzake ni cha Kidini, Kikabila na Kiukanda.

Akijibu Maswali, Kitilla alisema, Kama Viongozi wa Dini wanavyowafahamu waumini wanaozingatia Ibada za Dini zao, Ndivyo tunavyovifahamu Vyama na Wanasiasa walivyo, maana Wahusika hao ni waumini wetu; Lakini CHADEMA si Chama cha Wakristo na kinavyotajwa, mbona wamo na Wa-Islamu?.

"Kama Chadema ni cha Kikristo, Kikabila na Kikanda, Basi Msajili wa Vyama kabla ya kushitakiwa kuachia Ngazi maana alikiuka Sheria za kusajili Vyama na amekiacha kikue katia Uongo huu hadi kinakuwa na Wabunge 48" alisema Kitilla akisisitiza, Waislamu na makabila mengine waliomo ni nani?.

Aliongeza kusema, Uongo huo ndio uliopandwa kwa Chama cha Wananchi (CUF) ukaota, ukamwagiliwa mpaka mavuno yakavunwa kwa sababu kilikuwa kinaimalika.leo tena Uongo uleule ndio unaotaka kutumika kuwapumbaza watanzania. Ninachoamini, mtu hadanganywi mara Mbili.; Viongozi waache!

Kuhusu Udini alisema, "Tunapougua na kuhitaji damu tunauliza ni ya Dini ya Kikristo au Mu- Islamu? Je Hewa tunayovuta tunauliza kama ni ya Mkristo au Mu-Islamu? Nawashauri Wakristo na Wa-Islamu wasidanganywe, Amani yetu ikatoweka kwa sababu ya watu wachache wenye Uroho wa Madaraka.

Aidha Kitilla aliyetaja namba zake 0754-512347 alidai, anawamatafuta Viongozi wakuu wa CHADEMA wasio Wakristo Mbunge Said Arfi, Zitto Kabwe (MP), Prof. Abdalah Safari, Halima Mdee (MP), Hamad Yusuph, Issa Mohamed na wengine ili awaulize M4C kuna udini? Wakisema hakuna atajiunga huko!

My take;Wote kwa pamoja tukijitahidi kuwa wakweli tutaweza kusonga mbele.
Hapo kwenye nyekundu ni kweli! lakini ujue walinda utawala! TISS wanakutafuta wakung'oe kucha, meno na macho shehe wangu!! Wataanza kukupinga na kukutukana lakini ukweli ndio huo!! UDINI unapandikizwa na majangili na majambazi yanayotaka kuendelea kupukuta raslimali zetu zote!. Tatizo siyo Uislamu au Ukristo tatizo ni majangili kuacha ujangili au kudhibitiwa hayataki!!
 
pia ndugu yangu Selemani ningependa kama ungenijibu hili; je! unadhani kwa kitendo cha Dr.W.Slaa kuwahi kuwa kiongozi wa dini, basi ilikuwa ni kosa kijamii, kisheria au kibinadamu? na kama haikuwa kosa miongoni mwa niliyoyataja; kwa nini udhani kwamba anastahili kupoteza haki zake za kibinanamu, kijamii au kisiasa!

-Mh Jakaya Kikwete alikuwa ni kiongozi mkubwa jeshini kabla ya kuwa mwanasiasa na leo hii ni rais; je! unadhani kwa kuwa alishawahi kuwa mwanajeshi; basi nchi hii kwa sasa anaiongoza kijeshi?

-Hapo chini kwenye signature yako umeandika "Fikiri" nami nakusihi "Fikiri"
 
Last edited by a moderator:
Udini unawa sumbua watanganyika ngoja tuone mwisho wa tamthilia itakuwaje
 
Aisee wewe unaweza kutusaidia sana katika upelelezi wa alietupa bomu Arusha.

Mkuu aliyelipua BOMU Arusha ni siasa za maji taka za CDM na CCM.

Swali la kizushi tu:
Kwani FBI wameshatoa Report ya mauaji ya Padre Mushi kule Zanzibar?

Mkuu unataka kuukataa ukweli kwamba CDM ini y Wakristo na CUF ni ya Waislamu,na huko tunakoelekea CCM itabaki na Wapagani tu,wewe subiri tu pengine ikiwa 2015,vinginevyo CCM wasimamishe mtu wa Kaskazini Mkristo tena mkatoliki.
 
karibu sana shekhe kwenye chama cha mungu na sauti za walala hoi waliochoka na serikali dhalimu ya magamba.
 
mdee sio muislam, hilo ni jina la bibi yake namfahamu nimefanya nae kazi na nimefanya kazi na baba yake mzazi huko moshi.......huyu shekhe ubwabwa ameingia choo cha k..ke
 
pia ndugu yangu Selemani ningependa kama ungenijibu hili; je! unadhani kwa kitendo cha Dr.W.Slaa kuwahi kuwa kiongozi wa dini, basi ilikuwa ni kosa kijamii, kisheria au kibinadamu? na kama haikuwa kosa miongoni mwa niliyoyataja; kwa nini udhani kwamba anastahili kupoteza haki zake za kibinanamu, kijamii au kisiasa!

-Mh Jakaya Kikwete alikuwa ni kiongozi mkubwa jeshini kabla ya kuwa mwanasiasa na leo hii ni rais; je! unadhani kwa kuwa alishawahi kuwa mwanajeshi; basi nchi hii kwa sasa anaiongoza kijeshi?

-Hapo chini kwenye signature yako umeandika "Fikiri" nami nakusihi "Fikiri"

Nani atakubali kuwa karatsi la chooni mara mbili,wakati wa Uhuru na sasa labda Mohammedi Mtoi na wenzake kama huyu Shekhe ubwabwa.
 
Binafsi kama muumin, namuunga mkono sheikh wangu kwa hayo aliyosema! Ccm ni hatari kwa usalama na mshikamano kwa taifa letu! Allah atatuongoza katika kuushinda uovu wa maccm!
 
karibu sana shekhe kwenye chama cha mungu na sauti za walala hoi waliochoka na serikali dhalimu ya magamba.

Mkuu ebu kuwa wazi basi ni Mungu gani unayemkusudia?Maana miungu wapo wengi,wengine mpaka ng'ombe wanaamini ni Mungu.
 
ukweli kwamba cdm ini y wakristo na cuf ni ya waislamu,na huko tunakoelekea ccm itabaki na wapagani tu,wewe subiri tu pengine ikiwa 2015.
ndugu yangu acha kuchochea udini tena kwa makusudi huku ukijua.elewa kwamba unachokifanya hakiwezi kukusaidi wewe, dini yako wala chama chako. Sasa sana utaishia kutoa mchango kamili katika kuivuruga nchi yako.ni bora ukaamua kubadilika na kushika njia iliyo sahihi, njia ya kujenga na si kuchochea.natumai umenielewa kwa kuwa nina uhakika unachokifanya na wanachokifanya watu wa dizaini yako;hawakifanyi kwa bahati mbaya bali kwa sababu maalum.
 
Huyu sheikh anatafuta pakutokea tu, ndo maana kajipa promo kaweka na namba ya simu ili mradi wake ukamilike, nani asiejua cdm msimamo wao?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom