SHEKHE Ang’aka; Asema CHADEMA si Chama cha Wakristo

SHEKHE Ang’aka; Asema CHADEMA si Chama cha Wakristo

Status
Not open for further replies.
Mungu ambariki huyu Shekhe, aendeleze mapambano yeye binafsi na kuwaambia ndugu zake.
 
Kwani naona hapo anachanganya Dini na Siasa. Kwa mlio Tanzania Vipi Sheikh Mtopea ameishia wapi siku hizi?

Sasa wewe haupo Tanzania....wayatakia nini ya Tanzania? Huyo mtopea si mulimchukua nyiye CCM?

Kunako 2000...

Mgombea urais kupitia CCM, Mh. Benjamin William Mkapa amesema, ameongoza kwa haki, uwazi, ukweli na uadilifu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Mh. Mkapa ameyasema hayo alipokuwa akizindua kampeni za uchaguzi katika viwanja vya Jangwani Jumamosi.

Aidha katika mkutano huo, mtu mmoja aliyeitwa sheikh Mtopea alisoma aya aliyodai ni ya Qur'ani lakini isiyopatikana popote katika msahafu.Mtopea alisoma aya hiyo, akiwashambulia waislamu huku akitiwa mori na wana CCM walionadi, "waambie hao" na wengine wakipiga takbira za kejeli.Akiwa jukwaani alimokuwa Mh. Mkapa na Rais mstaafu Ali Hassani Mwinyi, Mtopea alisema, "INNA LLAHA LA YUGHAYYIRU NIIMATIHI, HATTA YUGHAYYIRU MA BIANFUSIKUM"


Mashekh mbalimbali walioongea na gazeti hili wamesema, hakuna 'aya'.kama hiyo katika msahafu.Labda "wakati Rais Mkapa akizindua kampeni za chama chake, sheikh Mtopea alikuwa akizindua Qur'an yake", amesema sheikh Bassaleh katika taarifa yake ya maandishi.
 
Well!
Hayo ni maoni na msimamo wake binafsi!

...Chadema kama wakitaka wanaweza kufanya survey kujua kati ya Waislamu kumi ni wangapi wanaiona Chadema kuwa ni ya Wakristo.

mlitaka CHADEMA iweje iwe na viongozo wapagani wasio mjua Mungu? Je ni sababu ipi inayokifanya CHADEMA kuwa chama cha kikristo? Mnataka iweje CHADEMA?
 
Inaelekea unaushahidi "duniani mpaka mbinguni"
msomi wa ilmu dunia na ilmu akhera professor Abdallah Safari atii "amenunuliwa!!!!!!"
kama vipi itungwe sheria ya kuzuia kununuliwa (iwe kosa la jinai lisilo na dhamana) hoja ipelekwe bungeni kibinafsi na ama lusinde au Mwigulu Nchemba

Mkuu upo Sahihi ila unashindwa kujua kwamba kama Sheria hii ya Kununua viongozi wa Chama kingine ikipitishwa kuwa SHERIA mbona watakao Umbuka ni CHAMA CHA MAJANGILI [CCM] kwani ndio Wamebobea ktk Siasa Chafu za Kurubuni na Kuwanunua Wapinzani.

Kwa kufupi tu wako wapi wafuatao. (1)THOMAS NGAWAYA. (2)WHALID KABOROU. (3)MASUMBUKO LAMWAI. (4)SHIMBWEE SHITAMBALA. (5)STEVEN MASATU WASSIRA. (6)JULIANA SHONZA. (7)MWAMPAMBA. (8)NAPE NNAUYE(CCJ).Na wengine wengi.

Sasa hapa ni nani mwenye kuongoza kwa biashara Haramu na Chafu kuliko hata ya Ujumu uchumi kununua Wanachama na Viongozi wa Chama kingine?

CCM ndicho Chama pekee Duniani kinaongozwa na Watu au Viongozi wenye Uwelewa mdogo[Finyu] kama NAPE, MWIGULU nk. Huu sio wakati wa CHADEMA Kuendelea kulumbana na MAJANGILI CCM,bali ni Wakati wa Kujipanga kuhakikisha kuwa chama cha KUNGOA MENO NA KUCHA, CCM hawarudi tena ktk uongozi wa nchi hii.

CCM [GENGE LA WAHUNI] HAIKUBALIKI TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA!!!!
 
Watanzania tuache unafiki.Ni ukweli usiopingika ya kwamba wanachama na wapenzi wengi wa CHADEMA in Wakristo kama ilivyo kwa wanachama wapenzi wengi wa CUF in Waislamu.

Ushauri wangu kwa Watanzania Wakristo wote wahamie CHADEMA na Waislamu wote wahamie CUF baada ya hapo CCM itakuwa imekufa kifo cha kawaida kwani itakuwa imebakiwa na wapagani tu,na tutakuwa tumebakiwa na vyama viwili vikubwa vya Kidini hapa Tanzani,yaani:
  • CHADEMA ya Wakristo
  • CUF ya Waislmu

Ukifanyika uchaguzi ndio utatoa majibu magumu waliyokimbia JK na timu yake wakati wa sensa 2012,nani wengi Waislamu au Wakristo?
 
Big up Sheikh kwa kuwa mkweli na muwazi Kama CHADEMA ni chama cha wakristo hao wakristo walioko CCM wanasubiri nini kwann wasijiunge kwenye chama chao,Hakika dhambi hii ya udini waliipandikiza CCM na aitawaacha itawatafuna.
 
=nguvukazi mikono;6367347]Ushauri wangu kwa Watanzania Wakristo wote wahamie CDM na Waislamu wote wahamie CUF tumebakiwa na vyama viwili vikubwa vya Kidini hapa Tanzani,yaani:
  • CDM ya Wakristo
  • CUF ya Waislmu
Aisee wewe unaweza kutusaidia sana katika upelelezi wa alietupa bomu Arusha.
 
Hauhitaji kuwa na degree kujua CDM ni chama cha udini, ukabila na ukanda. Huyu, shehe ni wale wanao nunuliwa na cdm ili kuondoa hili doa, km walivyo fanya kwa Prof. Safari. Kwa hili la udini cdm haisafishiki hata chembe hata mlete thread ngapi humu ndani.

Comment yako haiendani na hili jina "ulilo jipachika" GeniusBrain!
 
Hauhitaji kuwa na degree kujua CDM ni chama cha udini, ukabila na ukanda. Huyu, shehe ni wale wanao nunuliwa na cdm ili kuondoa hili doa, km walivyo fanya kwa Prof. Safari. Kwa hili la udini cdm haisafishiki hata chembe hata mlete thread ngapi humu ndani.

NJOO HAPA lumumba nikupe 7,000= unitafutie SHEKHE ..POOR BRAIN
 
hahaha huyu sio shekh ni shehena anunuliwa hivihivi na watu wanochukia na kupinga uislam waziwazi bungeni...


 
Hauhitaji kuwa na degree kujua CDM ni chama cha udini, ukabila na ukanda. Huyu, shehe ni wale wanao nunuliwa na cdm ili kuondoa hili doa, km walivyo fanya kwa Prof. Safari. Kwa hili la udini cdm haisafishiki hata chembe hata mlete thread ngapi humu ndani.
Kwa ujangili, ufisadi, kungoa watu meno kucha na macho, rushwa, na wizi, MACCM hawasafishiki hata utumie jick na omo!!!

 
nimeipenda hiyo point ya kuongezwa damu; maana kweli ukiwa na mgonjwa huulizi hii damu ni ya mla kitimoto au mlokole au mywa viroba au anayeswali adhuhuri.
Wote nidugu MOJA, big up SHEKH
 
Huyu Sheikh kapewa mshiko na Tundu Lissu

Kwa kuwa wewe umezoea kupewa (hadi umeuza utu wako na uwezo uliopewa wa kufikiri bila kushikiwa akili) unadhani kila mtu ananunuliwa? You (and the likes of you) are pathetic shameless turncoats!
 
Kama kweli haya kayasema Shekhe basi binafsi namwombea kwa Mungu aliye hai aweze kukua kiroho na kiimani ili aweze kuwaeleza Watz wengine kuhusu mambo haya.

Lakini Shekhe nikusahihishe tu kidogo, Halima Mdee siyo Muislam ni Mkristo hilo ni jina la bibi yake alilopewa. Lakini hilo haliniumizi sana, na wala wewe huna haja ya kuwaita hao uliowataja. Wewe angalia je; ni chama kipi angalao kwa asilimia zaidi ya 50% KINAZUNGUMZA, KINATETEA KWA VITENDO na KINATEKELEZA yale ambayo kinayaamini ni MASLAHI ya Taifa. Hicho ndicho chama cha kukisaidia kimawazo, kimkakati, na hata kifedha. Karibu shekhe
 
aislamu wa nchi hii hawawezi kuchagua Padre mstaafu kuwa Rais. Sio udini wala nini, ni reality. Sheikh Kitilla anajiongopea tu.
 
Waislamu wa nchi hii hawawezi kuchagua Padre mstaafu kuwa Rais. Sio udini wala nini, ni reality. Sheikh Kitilla anajiongopea tu.
kwani ndugu yangu Selemani wewe ujuavyo udini ni nini? je! unadhani udini ni kitu kuzuri? je! unafahamu sifa za mtu anayeweza kugombea urais nchini kwa mujibu wa sheria? je! unadhani sheria za uchaguzi zina mapungufu na zinahitaji marekebisho?
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom