Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Sheikh Yahya: JK, Dk. Slaa kupatana
na Hellen Ngoromera
[IMG]http://www.freemedia.co.tz/daima/anime/amka2.gif[/IMG] MNAJIMU Mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, amemtabiria Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Willbrod Slaa kukaa pamoja. Kutokana na hali hiyo, Sheikh Yahya ameitaka jamii kuvuta subira kwani watapata habari njema kuhusu viongozi hao hivi karibuni.
Mnajimu huyo alitoa utabiri huo juzi usiku jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika kipindi cha Nyota Zenu kinachorushwa hewani na Channel ten.
"Namsalimu rais mpendwa Kikwete, namsalimu Dk. Slaa kwa kuonyesha juhudi zake katika kuleta amani, kinyota nawaona Dk. Slaa namwona Rais Kikwete wanapeana mikono, nawaona watakuwa pamoja," alisema Sheikh Yahya.
Aliongeza kuwa kinyota anawaona pia Rais Kikwete na Dk. Slaa na wenzake kuwa watakaa pamoja na kula pamoja.
Alitabiri pia kuwa CHADEMA kushirikiana na CCM pamoja na Chama cha Wananchi (CUF) na kueleza kuwa Mungu ndivyo anavyotaka.
Sheikh huyo aliweka wazi kuwa kuanzia Februari 18 mwakani, CHADEMA na Chama cha Mapinduzi (CCM) wataelewana vilivyo lakini amani kubwa itakapatikana Novemba 21 mwakani.
Aliwataka wananchi kuacha mambo aliyoyaita ya kipuuzi na kuwaambia wavute subira kwani Mwenyezi Mungu anatawala kupitia uchaguzi.
Hivi huu ni utabiri au anawapa ushauri wapatane? huyu kikongwe anachezea akili zetu, hafai ku...
Precisely!Huyo naye aache upuuzi wake kwa kumtumia Mungu kupata riziki yake; bora afanye kazi nyingine. Hivi anafikiri ni wangapi wanaoamini mambo ya minajimu? We believe in the living God, and who already spoke to us and revealed His will in His Word, and not in some unajimu or something. Afanye kazi ya kujenga Taifa, huo ni uvivu na kula kwa kutumia ujanja. Anajua kuwa Dr. Slaa ni kiboko na iko siku Chadema itachukua mchi, hivyo analinda maslahi yake pande zote mbili!!!! No one is stupid enough to be fooled by some magical tricks/divination these days of science and technology.
Vipi huyo mtangazaji hakumwuuliza mbona uchaguzi ulikuwepo wakati yeye alishasema hakuna uchaguzi??
Very intersting, itakuwa katumwa na JK tu kuongea hicho alichosema
alishindwa kutabiri kura zitaibiwaje, anatabiri kuhusu kupatana,
this's insane.....
Eti utabiri, huyu mzee sijui vipi anazidi kuichanganya nchi yetu.
PHP:Sheikh Yahya: JK, Dk. Slaa kupatana na Hellen Ngoromera [IMG]http://www.freemedia.co.tz/daima/anime/amka2.gif[/IMG] MNAJIMU Mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, amemtabiria Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Willbrod Slaa kukaa pamoja. Kutokana na hali hiyo, Sheikh Yahya ameitaka jamii kuvuta subira kwani watapata habari njema kuhusu viongozi hao hivi karibuni. Mnajimu huyo alitoa utabiri huo juzi usiku jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika kipindi cha Nyota Zenu kinachorushwa hewani na Channel ten. "Namsalimu rais mpendwa Kikwete, namsalimu Dk. Slaa kwa kuonyesha juhudi zake katika kuleta amani, kinyota nawaona Dk. Slaa namwona Rais Kikwete wanapeana mikono, nawaona watakuwa pamoja," alisema Sheikh Yahya. Aliongeza kuwa kinyota anawaona pia Rais Kikwete na Dk. Slaa na wenzake kuwa watakaa pamoja na kula pamoja. Alitabiri pia kuwa CHADEMA kushirikiana na CCM pamoja na Chama cha Wananchi (CUF) na kueleza kuwa Mungu ndivyo anavyotaka. Sheikh huyo aliweka wazi kuwa kuanzia Februari 18 mwakani, CHADEMA na Chama cha Mapinduzi (CCM) wataelewana vilivyo lakini amani kubwa itakapatikana Novemba 21 mwakani. Aliwataka wananchi kuacha mambo aliyoyaita ya kipuuzi na kuwaambia wavute subira kwani Mwenyezi Mungu anatawala kupitia uchaguzi.
Sheikh Yahya aliombe taifa msamaha kwa uongo huu..........................hadi leo JK hana mpango wa kukutana na Dr. Slaa na lengo lake ni kumtafutia sababu za kumfunga jela tu.....................................utabiri wa mnajimu huyu ulikuwa ni uongo...............alidai tuvute subira na sasa je.............................yako wapi
Sheikh Yahya: JK, Dk. Slaa kupatana
na Hellen Ngoromera
MNAJIMU Mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, amemtabiria Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Willbrod Slaa kukaa pamoja. Kutokana na hali hiyo, Sheikh Yahya ameitaka jamii kuvuta subira kwani watapata habari njema kuhusu viongozi hao hivi karibuni.