Sheikh Yahya: JK, Dk. Slaa kupatana... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Yahya: JK, Dk. Slaa kupatana...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 1, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,720
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  na Hellen Ngoromera

  MNAJIMU Mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, amemtabiria Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Willbrod Slaa kukaa pamoja.

  Kutokana na hali hiyo, Sheikh Yahya ameitaka jamii kuvuta subira kwani watapata habari njema kuhusu viongozi hao hivi karibuni.

  Mnajimu huyo alitoa utabiri huo juzi usiku jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika kipindi cha Nyota Zenu kinachorushwa hewani na Channel ten.

  "Namsalimu rais mpendwa Kikwete, namsalimu Dk. Slaa kwa kuonyesha juhudi zake katika kuleta amani, kinyota nawaona Dk. Slaa namwona Rais Kikwete wanapeana mikono, nawaona watakuwa pamoja," alisema Sheikh Yahya.

  Aliongeza kuwa kinyota anawaona pia Rais Kikwete na Dk. Slaa na wenzake kuwa watakaa pamoja na kula pamoja.

  Alitabiri pia kuwa CHADEMA kushirikiana na CCM pamoja na Chama cha Wananchi (CUF) na kueleza kuwa Mungu ndivyo anavyotaka.

  Sheikh huyo aliweka wazi kuwa kuanzia Februari 18 mwakani, CHADEMA na Chama cha Mapinduzi (CCM) wataelewana vilivyo lakini amani kubwa itakapatikana Novemba 21 mwakani.

  Aliwataka wananchi kuacha mambo aliyoyaita ya kipuuzi na kuwaambia wavute subira kwani Mwenyezi Mungu anatawala kupitia uchaguzi.
   
 2. s

  seniorita JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyo naye aache upuuzi wake kwa kumtumia Mungu kupata riziki yake; bora afanye kazi nyingine. Hivi anafikiri ni wangapi wanaoamini mambo ya minajimu?

  We believe in the living God, and who already spoke to us and revealed His will in His Word, and not in some unajimu or something. Afanye kazi ya kujenga Taifa, huo ni uvivu na kula kwa kutumia ujanja.

  Anajua kuwa Dr. Slaa ni kiboko na iko siku Chadema itachukua mchi, hivyo analinda maslahi yake pande zote mbili!!!! No one is stupid enough to be fooled by some magical tricks/divination these days of science and technology.
   
 3. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vipi huyo mtangazaji hakumwuuliza mbona uchaguzi ulikuwepo wakati yeye alishasema hakuna uchaguzi??
  Very intersting, itakuwa katumwa na JK tu kuongea hicho alichosema
   
 4. MKURABITA

  MKURABITA JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 311
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hivi huu ni utabiri au anawapa ushauri wapatane? huyu kikongwe anachezea akili zetu, hafai ku...
   
 5. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  alishindwa kutabiri kura zitaibiwaje, anatabiri kuhusu kupatana,
  this's insane.....
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Dec 1, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Eti utabiri, huyu mzee sijui vipi anazidi kuichanganya nchi yetu.
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  He is just playing with our minds. Hana cha nini wala nini. Muongo mkubwa.

  Anatumia psychology anajidai mtabiri.
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Msemaji wa JK huyo
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,720
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Sheikh YahyaJKDkSlaa kupatana
   
   
  na Hellen Ngoromera
   
   
   
  [IMG]http://www.freemedia.co.tz/daima/anime/amka2.gif[/IMG]                                                                                            MNAJIMU Mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh  Yahya Hussein, amemtabiria Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Chama  cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Willbrod Slaa  kukaa pamoja.  Kutokana na hali hiyo, Sheikh Yahya ameitaka jamii  kuvuta subira kwani watapata habari njema kuhusu viongozi hao hivi  karibuni.
   
  Mnajimu huyo alitoa utabiri huo juzi usiku jijini Dar es Salaam wakati  akizungumza katika kipindi cha Nyota Zenu kinachorushwa hewani na  Channel ten.
   
  "Namsalimu rais mpendwa Kikwete, namsalimu Dk. Slaa kwa kuonyesha juhudi zake katika kuleta amani, kinyota nawaona Dk. Slaa namwona Rais Kikwete wanapeana mikono, nawaona watakuwa pamoja," alisema Sheikh Yahya.
     
  Aliongeza kuwa kinyota anawaona pia Rais Kikwete na DkSlaa na wenzake kuwa watakaa pamoja na kula pamoja.
     
  Alitabiri pia kuwa CHADEMA kushirikiana na CCM pamoja na Chama cha Wananchi (CUFna kueleza kuwa Mungu ndivyo anavyotaka.
   
  Sheikh huyo aliweka wazi kuwa kuanzia Februari 18 mwakaniCHADEMA na  Chama cha Mapinduzi (CCMwataelewana vilivyo lakini amani kubwa  itakapatikana Novemba 21 mwakani.
   
  Aliwataka wananchi kuacha mambo aliyoyaita ya kipuuzi na kuwaambia  wavute subira kwani Mwenyezi Mungu anatawala kupitia uchaguzi.
  Sheikh Yahya aliombe taifa msamaha kwa uongo huu..........................hadi leo JK hana mpango wa kukutana na Dr. Slaa na lengo lake ni kumtafutia sababu za kumfunga jela tu.....................................utabiri wa mnajimu huyu ulikuwa ni uongo...............alidai tuvute subira na sasa je.............................yako wapi
   
 10. 911

  911 Platinum Member

  #10
  Mar 5, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Mjasiria mali tu!
   
 11. M

  Msindima JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu wala hachezi na akili zetu maana tumeshamshtukia.
   
 12. k

  kukubata Member

  #12
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa masheikh huwa wamekosa changuzumza hadi waingie kwenye siasa ......yeye aendeleze ushirikina wake ahache habari za ujinga
   
 13. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Precisely!
   
 14. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Naona mzee anazidi kuzeeka vibaya!tumpe pole na kumuombea!!
   
 15. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #15
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Asingeweza kutabili wizi wa kura kwa kuwa yeye ni kada wa CCM!!
   
 16. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #16
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Vipi tena rafiki yangu KATAVI,hata wewe unapinga mambo haya wakati kule ufipani kweni ndipo yalipoanzia!!
   
 17. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #17
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wamfunge,wamtese,lakini ipo siku Tanganyika itakombolewa na kuwa huru!!
   
 18. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #18
  Mar 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Inasemekana Mzee Yahya Hussein aliwahi kuahidi kumpa JK ulinzi wa majini ili aisidhuriwe na wabaya wake kama RA, EL, NzrK na wengine. Je ni kweli? Sasa mishahara yao wanachukulia Benki gani? Huyu mzee naye mtata sana.
   
 19. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #19
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  haka kazee kanazeeka vibaya manake saa kameshindwa kutabiri ukweli kanataka tuamini majini na nyota zake badala ya kuamini maandiko mm naona anatabiri kwa nguvu za Beelzebuli au ibilisi mkuu,mbona hajitabirii atakufa lini hadi watu wakamtabiria kafa kumbe bado.
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Mar 5, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Huyu Sheikh naye aache kutumiwa na TISS, wapatane kwani waligombana?. Wamegundua kuwa njia pekee ya kuua upinzani ni kuwashirikisha katika serikali na kujenga muafaka, CCM wamejua kabisa kuwa watanzania wanataka chama cha upinzani imara ili wakiamini na kukipatia kura ili waitoe CCM waliyoichoka. CHADEMA wanalijua hilo kwani ni chama chenye watu wanaofanya kazi kitaalam kwa kutumia utafiti. Hili la kukaa pamoja na kula ni la kawaida kabisa kwani Dr Slaa na Kikwete si maadui bali ni viongozi wa vyama vinavyoshindania dola hivyo linapokuja suala la kisiasa sidhani kama kutakuwa na urafiki wa kama CCM na CUF. Na kama CHADEMA wataingia kwenye mtego huu basi wajue kuwa the rising share price ya chama chao itazama mpaka karibia na valueless.
   
Loading...