Polisi wazingira Msikiti wa Kichangani, Sheikh Walid hajatokea

Polisi wazingira Msikiti wa Kichangani, Sheikh Walid hajatokea

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,079
Reaction score
17,138
Askari wa Jeshi la Polisi nchini, wameuzingira Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni, ambao awali ilidaiwa aliyekuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Omari Kawambwa, angekwenda kuswali Swala ya Ijumaa.

1784289356219.png

Katika mitandao ya kijamii kulisambazwa taarifa za waumini kujikusanya katika msikiti huo kwenda kufanya ibada na kumwona kiongozi huyo wa kidini aliyesimamishwa siku nne zilizopita.

Sheikh Kawambwa, alisimamishwa uongozi na Baraza la Ulamaa la Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), pamoja na masheikh wengine wawili wa Mkoa wa Singida na Kigoma, kwa tuhuma za ukiukaji wa maadili.

Tofauti na ljumaa nyingine zisizo ndani ya Mwezi wa Ramadhan, Ibada ya leo ilikuwa na idadi kubwa ya waumini kiasi cha wengine kukosa nafasi ndani na wakaswali nje ya jengo.

Soma: Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Walid Omar Kawambwa atenguliwa kwa kukiuka 'misingi' ya Uongozi

Pia, kulikuwepo minong'ono kutoka kwa baadhi ya waumini wakisema wanasubiri kumwona Sheikh Walid kwenye mimbari akitoa neno lolote baada ya hatua zilizochukuliwa dhidi yake.

Hata hivyo, Swala ya Ijumaa ilianza saa 6:30 mchana na Sheikh Walid hakuwa miongoni mwa walioongoza swala wala kuhutubia na hakuwepo.

IMG_0106.jpeg

Chanzo: Mwananchi
 
Kidogo kidogo mambo yatalipuka Mwaipopo amekuwa msemaji wa bakwata yupo live akiitetea bakwata huyu jamaa wasipokuwa makini ni bomu linasubiri kulipuka, waislam walimkalia kimya na wengine kumpongeza pale alivyokuwa anamsakama Kitima sasa amewageukia wao.
 
Utetezi kwamba amevutia watu wengi hasa vijana kushiriki katika dini kikamilifu hauna mashiko.

Utetezi pia kwamba kila mtu ana madhambi kwa hiyo asihukumiwe sio sawa, kama kuna ushahidi alitishia kumuua mwanamke aliyezaa naye na mtoto wake pia ashughulikiwe.

Kusiwepo ni double standards.

Screenshot_20260717-151856~2.jpg
Screenshot_20260715-111959~2.jpg
 
Back
Top Bottom