Sheikh Ponda Issa Ponda SIYO Mtanzania....

*wadai damu, mate na nywele
wakati katibu wa jumuiyana taasisi za kiislamu nchini, sheikh ponda issa ponda, akiendelea kuuguza jeraha linalodaiwa kutokana na risasi katika mahabusu ya segerea, jijini dar es salaam, wingu jingine la mashaka limeizunguka familia yake. Mashaka hayoyanatokana na kitendo chamakachero wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakiwemo wale wa uhamiaji kudaiwa kuvamianyumbani kwa wazazi wake, ujiji mkoani kigoma,kwa nia ya kuilazimisha familia yake wachukuliwe damu kwa ajili ya vipimo vya vinasaba (dna).

Mtanzania jumapili limedokezwa kuwa kabla na baada ya tukio la sasa la sheikh ponda kupigwa risasi, makachero hao wamejaribu kuifikia familiahiyo ya ponda kwa takribani mara tano bila mafanikio yoyote.

Mmoja wa wanafamilia hao ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini akihofia usalama wake, amelidokeza mtanzania jumapili kwamba makachero hao baada ya kushindwa kuwashawishi kutoa damu, wakataka wapatiwe mate au nywele kwa ajili ya kufanyia kipimo hicho iwa ajili ya kufanyia kipimo hicho ili kutambua kama ponda ni ndugu yao na pia ni raia wa tanzania.

“tulikwisha shawishiwa sana, wakati fulani walitukatia hadi tiketi za ndege ili tuje dar es salaam kwa ajili ya kipimo hicho pamoja na kufanya mahojiano maalumu, lakinitulikataa, kwa sababu hawa jamaa wanaogopesha,” alisema mwanafamilia huyo.

Alisema baada ya kukataa kutoa damu, ndipo walipofika kwa mara nyingine tena wakitaka kuchukua nywele za mamayake mzazi ponda pamoja na za baadhi ya ndugu zake, lakini hilo nalo likashindikana baada ya wao kugoma.

“tangu sheikh ponda aumizwe mama yake mzazi amekuwa mgonjwa,baada ya kupokea taarifa hizo kwa mshituko, hata hivyo familia kwa ujumla haina uhuru tena kwa sababu imekuwa ikifuatwafuatwana makachero hao pamoja na watu wa uhamiaji.

“kwa kweli hofu imetanda katika familia yetu na hatujui nini kinafuata kutokana na kuendelea kufuatiliwa na makachero, kwa mfano ile hatua ya kupewa tiketi ili kwenda dar es salaam ilitufanya tushituke kwa hofu ya kwamba labda kuna mpango wa kudhuru maisha yetu, wamekwisha kuja mara nyingi, wameomba mpaka kitabu wamekitoa mpaka nakala, alichoandika sheikh ponda,kinaitwa ‘tanu mkoani kigoma mwaka 1954’,” alisema mwanafamilia huyo.

Wakati taarifa hizo zikiibuka sasa, kwa muda mrefu sasa kumekuwapo na habari za kukanganya juu ya asili ya sheikh ponda issa ponda, wengine wakidai kuwa ni raia wa nchini burundi, taifa ambalo linapakana namkoa wa kigoma, sehemu inayoelezwa ndiko alikozaliwa. Hata hivyo ndugu zake wanadai kuwawao ni raia halali wa tanzania.

Wakati huo huo, chanzo kingine cha habari kimelidokezea gazeti hili jinsi sheikh ponda alivyofanikiwa kuwakwepa polisi zanzibar, baada ya kudaiwa kutoa kauli za uchochezi katika mhadhara wa kiislamu wakati wakiwa visiwani humo.

Inadaiwa kwamba sheikh ponda kabla ya kuhutubia mhadhara huo alipita gerezani kumuona kiongozi wa jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu zanzibar, sheikh farid hadi ahmed.

Kwamba baada ya kumaliza kuhutubia mhadhara huo, alianza safari ya kuelekea katika msikiti wa mbuyuni.

chanzo: mtanzania.

hawa wanaotafuta hizo sample za dna ni vilaza watafute wataalam wa surveilance 24/7 wanakupa dna ya binaadamu yeyote.. Source za dna ni nyingii mnoo na huwezi kuzificha... Toothpick, nguo unazovaa, kiti unachokalia, chooo unachotoa, hata kwenye mkojo, chanuo, mswakii, kucha nywelee..

Kiufupi hawa jamaa ni weupe ukikitana na weledi wa hizo shughuli hukatiziii... Na wanafanya kazii kimaandazi sina na uwezo wao is quetionable...

Wasichojua ni kwamba binaadam anashed maisha yake yotee. Ndioo maana hata ukioga vipi bado taulo litachafuka tuuu... Uchafu ni ngozi unayopoteza baada ya nyingine mpaya kuota....

Am not conviced with agility of these guys in this line of work..

Story imekaa kama ya kutungwa kijiweniii
 
Breaking news :ponda apandishwa kizimbani morogoro.asafirishwa kwa helikopta ya polis
 
Ameshapandisha kizimbani morogoro .usafiri aliotumia bajaji ya said mwema
 
Si kila kinachoandikwa magazetini ni cha ukweli. Siunajua wanataka kuuza gazeti! Ndiyo maana wanashtakiwa mara kwa mara "for Libel". Tusiamini kila kitu kinachoandikwa magazetini. Hata kama tunadiffer na vitu fulani fulani vinavyofanywa na serikali wakati mwingine inabambikiwa!! Serikali ikitaka kujua uraia wa Ponda si lazima wachunguze DNA ambayo haithibitishi uraia bali inathibitisha kama mhusika ni mtoto wa nani. Mtanzania haikufanya uchunguzi wa kina wa hii hadithi!!!
taarifa imetoka gazeti la Mtanzania na wanafamilia wamethibitisha hilo.
 
Kwahiyo hatoitaji mtu yoyote hasa hao vibaraka walo pewa kofia na uji kusema leo hawamjui Ponda support ya Mola inatosha Ponda endelea kutetea haki za wanyonge kwa amani
 
Kwahiyo hatoitaji mtu yoyote hasa hao vibaraka walo pewa kofia na uji kusema leo hawamjui Ponda support ya Mola inatosha Ponda endelea kutetea haki za wanyonge kwa amani
Yesu atamsaidia huko alipo! maana serikali imemuandama sana huyu mzee,mm naamini akimkubali bwana kuwa mwokozi wa maisha yake basi haya yote yataisha

mapendo daima

 
Jaman wa tz mnaishaangaa serikari yenu kwa kuwabambikia wa2 kesi!? Ponda hayupo ivyo anavyo hubiliwa na serikari! Kwa lip hasa? Sema anaongea ukwel ndo maana serikari na mafisad wanamchukia! Wa tz tuamke tusikul kugawa kwa misingi ya din Tuunga wote kwa pomoja kuwaondoa hawa ccm!
 
Kama si mtanzania ,kama mnakumbuka dar es salaam wizara ya uhamiaji ilitoa details za kutosha kuthibitisha kua ni mtz??

Cheti cha kuzaliwa,shule ya msingi,sekondari(o level+a level) na vitambulisho vingine kama kura na vya kidini

Sasa we mtoa mada haya umeyapata wapi?
Kati ya wewe na wizara ya uhamiaji tumwamini nani??
Acha kujikoroga mkuu!!

'' Nan-sens on yua brein''
Try to put forward your effort on true stories
Badilika mkuu,,SHEIKH PONDA ni mtanzania halisi

Kuna ile ya Said Maulid nayo cjui iliisha vp
 
DNA inaweza kukupa ishara ya mtu ana asili ya kabila gani, au watu gani kwa maana ya "ethnic group". Kwa mfano, DNA inaweza kusema kwamba mtu fulani ana vinasaba vya wamasai. Lakini kwa kuwa wamasai wapo Uganda, Kenya na Tanzania; DNA haiwezi kusema kama mtu huyu mwenye vinasaba vya wamasai anatoka nchi gani.

Hili la sheikh Ponda sasa ni gumu kidogo kwa sababu hata rais Mkapa tukimpima tukamkuta na chembe chembe za wamawiya/wamahiwa; mtu utaweza kujenga hoja kwamba rais Mkapa ni mtu wa Msumbiji. Kwa ufupi DNA haitaweza kumtimua Ponda na kumpeleka Burundi.
Aangaliwe amezaliwa wapi na amesoma shule gani. Msingi/madrasa/n.k. Kisha atajulikana kwao wapi.

Tukimaliza na Ponda tunakuja na Padre. Watu wa Karatu wamehamia kutoka Kenya.Timua hii mbu irudi kenya ikaendeleze ngono nzembe kwao.

Hata Said Ally Mwema sio raia wa Tanzania
 
Haya mambo ya kutofautiana mtizamo kuitana kuwa siyo watanzania na wengine wakienda mbali kusema hata Mwalim J.K nyerere siyo mtanzania basi tukubaliane kuwa hakuna mtanzania sisi wote ni wakuja..

Na huu ni ujinga hasa kwa aliyeleta thread, serikali ijipu madai ya Ponda na kuelesha umma kama Ponda anapotosha.. me nimemsoma Ponda naona ana madai ya msingi kwa uislam, na si vyema wakristu kubeza ila kuacha waislam wamalizane na serikali vinginevyo tutaishia kujenga chuki ya kidini, jambo ambalo si nzuri kabsa. Ponda asikilizwe na kama madai yake ni uchochezi basi mahakama ndo itoe hukumu ila si JF wala mleta thread, hii ni kutaka kujenga chuki zisizo na msingi.
 
Ndugu Wanabodi,

Napenda kuwaambia Watanzania wapenda AMANI na UTULIVU kuwa Sheikh Ponda Issa Ponda SIYO Mtanzania na kuwa ni Mtu wa Burundi aliyeingilia Kigoma na kuzamia Dar es salaam. Bw. Ponda analipwa na baadhi ya Watanzania walioko nje ya nchi kuratibu shughuli zote za vurugu kupitia mgongo wa dini ya Kiislmu ambayo hata siku mmoja mafundisho yake hayaelekezi watu kufanya vurugu na mauaji bali AMANI.

Bw. Ponda, anafadhiliwa na watu hao walioko USA, UK na nchi za Uarabuni. Nawathibitishia hili manake hata wakati wa sensa Bw. Ponda kupitia pesa hizo hizo aliweza kutoa machapisho tena za gharama akazisambaza nchi nzima kwa kutumia vijana ambao anawalipa yeye na yeye mwenyewe akiwa anazunguka katika baadhi ya mikoa kama ya Kigoma na Tanga. Wafadhili wake wengine tunawafahamu hadi kwa majina, akibisha tutamwaga hapa...!

Nimeona niwaambie hili ili mjue kuwa Ponda siyo kuwa natetea maslahi ya Waislamu bali TUMBO lake, pili, hana uchungu na vurugu ambazo anaziendesha hapa nchini. Tumekuwa tukirudi nyuma kwa uchumi siyo tu kwa sababu ya Rais wetu lakini pia kutokana na watu wachache kama hawa wakina Ponda.

Nina imani kuwa vyombo vya USALAMA vinafahamu hili lakini wameshindwa kuchukua hatua.

NOTE:
Ponda amelelewa toka Serikali ya Mwinyi, kuanzia vurugu za Mwembe Chai, Kiongozi Mkubwa wakati huo aliingilia kati kukamatwa Bw. Ponda na kumficha, unajua ni kwa nini?
Ameendelea kutoa AMRI kwa Serikali ya KIKWETE na serikali hiyo KUTII amri za Bw. Ponda! Wajua ni kwa nini?

==============
Agosti 18, 2013

Kwa hiyo wewe ni afisa wa Uhamiaji???. Hebu tupe ushahidi wako kwanza kama wewe ni Raia halali wa nchi hii!
 
tukiwaambiwa watu makafiri wamesoma sana tunatukanwa sasa mbona hata Mawakili mnawachukuwa wasio ya DINI ya Ponda je Kesi wakishindwa lawama mtampa nani
Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Sheikh Ponda anayetetewa na mawakili Bartholomew Tarimo na Ignas Punge, alikana mashtaka yote na hivyo upande wa mashtaka kupinga dhamana kwa madai kuwa Sheikh Ponda anatumikia kifungo cha nje na kwamba hakutakiwa kufanya kosa, hata hivyo anakabiliwa na makosa mengine.
Hata hivyo, upande wa utetezi ukiongozwa na Punge ulishindwa kuwasilisha maombi ya dhamana kwa madai kuwa kuomba dhamana kuna hatua nyingi,
 
Katika vyoote nilivyosoma hapa nimesikitishwa na hiyo mbinu ya usalama wa taifa kujifanya sijui uhamiaji ili kupata data za wazazi wake kama damu na nywele ili kupima DNA! Sidhani kama usalama wetu wa taifa umekosa mbinu kiasi ukaombe "damu na nywele"... Ina maana hao ndugu wa Shehe Ponda hawaumwi,hawendi saluni kunyoa na kusuka? Kweli kama kupata damu na nywele za ndugu wa Shehe Ponda ili kuthibitisha DNA yake mpaka sasa imekua ngumu,sasa wanaweza nini???
 
Katika vyoote nilivyosoma hapa nimesikitishwa na hiyo mbinu ya usalama wa taifa kujifanya sijui uhamiaji ili kupata data za wazazi wake kama damu na nywele ili kupima DNA! Sidhani kama usalama wetu wa taifa umekosa mbinu kiasi ukaombe "damu na nywele"... Ina maana hao ndugu wa Shehe Ponda hawaumwi,hawendi saluni kunyoa na kusuka? Kweli kama kupata damu na nywele za ndugu wa Shehe Ponda ili kuthibitisha DNA yake mpaka sasa imekua ngumu,sasa wanaweza nini???
Hao ni waongo.kupata damu kwa ajili ya uchunguzi wa DNA ipo kisheria katika process za uchunguzi.kukatata kutoa damu ilii itumeke katika uchunguzi wa jinai ni sawa sawa na kukataa kuhojiwa na polisi.Utafunguliwa shtaka la kuzuia sheria kufanya kazi yake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom