Sheikh Ponda: Furaha imetoweka, tutafakari upya

Sheikh Ponda: Furaha imetoweka, tutafakari upya

Furaha itoke wapi wakati Mungu wa Ikulu anadhani kuongoza nchi ni kutoa kauli zilizojaa mihemuko na vitisho kila kukicha, mihemuko na vitisho ambavyo vinaharibu umoja na mshikamano nchini.

Kawaruhusu polisiccm wafanye mazoezi yao uraiani pamoja na kuwa wana makambi yao ili tu kuongeza hofu kubwa miongoni mwa Watanzania na kuuvuruga uchumi wa nchi kwa kipindi kifupi sana, ni lazima furaha nchini ipotee.

bro yale mazoezi yanaendelea au ?
 
Wanafki wakubwa nyie. Mbona alipopigwa risasi mlipenda angeuliwa kabisa. Leo kawa sio gaidi kwenu? Mwaka huu mtapanda mpaka mpapai kujikinga na hasira za tembo.
Kama ulitamani binadamu mwenzio afe kwasababu yoyote ile wewe huna tofaiti na wanao waua Albino ili wapate uongozi Wa kisiasa.shame!
 
Achana na wale wanaowafananisha Maswahaba wetu vipenzi na wanasiasa.
Huyu ndiye hasa kiongozi asiye na chembe ya unafiki.
Sijui kwanini hakupewa Usheikh mkuu wa Tanzania baada ya kifo cha Simba.
Hivi alikuwa kifungoni bado au alikuwa keshaachiwa?
Hangepewa cheo kwa sababu angewagawa Watanzania kulingana na itikadi zao.Angeamura wafuga nguruwe wote wauwawe na kuchoma moto makanisa yote.Bora abaki kama alivyo ili amani iweze kudumishwa.
 
Wengi wanaolalamikia ugumu wa maisha wanasahau kwamba miradi mingi ya maendeleo ilikuwa inasimama kutokana na ukata kabla hata ya awamu ya sasa, kwa sasa miradi mingi ipo hai na mingine ipo njiani kuja itakayoweza kutoa ajira kwa maelfu kwa watanzania.
 
Hivi tunalamika kwa kukosa pesa kwa majukumu halali tuliyokuwa tukitekeleza ama majukumu ya ujanjaujanja. Tunahitaji kubadilika na si kulalamika hakuna hela huku umelala ama kukaa vijiweni bila ishu ya msingi. Mimi ninachokiona sio tu hakuna pesa ila wengi wetu tulizoea kupata pesa
Hii kauli/dhana mbaya sana. Wanaolalamika ni mission town tu? Tunaofanya kazi halali pia tumepigika. Vituoni vya serikali OC haziji ili tulipwe stahiki zetu wewe unaongea utumbo eti tunaolalamika hatufanyi kazi. Watu wamelima nyanya kwa bidii sana, watejs hawapo eti unawatusi kwamba hawafanyi kazi.
 
Furaha imetoweka kwake na watu wa aina yake. Mi na familia yangu tunafuraha. Waliokuwa wakiishi kwa kutumia maruhani lazima furaha itoweke.
Kama mtu alikuwa na wafanya kazi wake hewa 5 kila mwisho wa mwez anachukua salary yao.unategemea nini?

Biashara ya madawa ya kulevya imesimama ambayo ilishika umaarufu sana awamu iliyopita. Sasa haipo. Unadhan furaha itatoka wapi? Tujiulize je watu wameshushiwa mshahara kusema sasa wanapata pungufu na zaman?

Unafiki utatufikisha pabaya. Nani hajui kuwa watu walikuwa wanapitishia makontena hapa bila kulipa ushuru na ndo maana yalikuwa mengi sana? Kama viongoz wa dini wanashiriki unafiki kwa kiasi hiki basi shetan ataanza kuwa mwema.

Kuna mambo ya kupinga nami ntayapinga katika utawala huu lakini suala la kuruhusu ufisadi ule wa kwanza sikubaliani nao hata kidogo. Nmekaa kwenye system nmeona pesa za walalahoi zilivyokuwa zikitajirisha wachache. Siwez taman hali ile irudi tena. Ntakuwa sawa na shetani kabisa.
FURAHA tuliyokuwanayo Watanzania, sasa haipo tena. Ni wakati wa kuhoji, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?, anaandika Faki Sosi.

Ni kauli ya Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taaisi za Kiislam Tanzania aliyoitoa leo akizungumza na mwandishi wa habari hii wakati akitoa salamu zake kuelekea Sikukuu ya Eid El Hajj.

Kesho duniani kote, waumini wa Dini ya Kiislam wanatarajia kusherehekea Sikukuu ya Eid el Hajj ikiwa ni sehemu ya ibada kwa mujibu wa imani ya dini hiyo.

Sheikh Ponda amesema, pamoja na kuwepo kwa sherehe hiyo lakini kuna hali ya masikitiko kwa Watanzania kutokana na vipato vya kushukwa jambo ambalo limeonda furaha ndani ya mioyo na familia zao.

Amesema, sikukuu zilizopita katika kipindi kama hiki watu waliweza kutoa sadaka, kulisha masikini, kuchinja kwa ajili ya ibada na kufanya ibada zingine zilizohusisha kipato.

Lakini kutokana na maisha kubadilika, waumini wa dini hiyo wameshindwa kutekeleza yale waliyokuwa wakiweza kuyatekeleza siku za nyuma jambo ambalo linahitaji kutafakari upya mtindo wa maisha ulivyo kwa sasa.

“Tunaelekea kwenye sikukuu lakini jambo ninaloliona kwa sasa ni kwamba, tunapaswa kutafakari upya, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?

“Siku za nyuma kulikuwa na furaha kubwa hasa wakati wa sikukuu kama huu lakini sasa mambo yamebadilika kwa kiwango kikubwa.

“Watu hawana furaha, maisha yamekuwa magumu. Ni kipindi cha kutafakari kwa mwaka mzima uliopita, tatizo ni nini zaidi?” amesema Sheikh Ponda.

Akizungumzia falsafa ya Hijja Sheikh Ponda amesema, yapo mambo mengi yanayopatikana pale watu wanapotekeleza ibada hiyo.

Amesema, miongoni mwa hayo ni pamoja na kuonesha umoja “kuvaa mavazi ya aina moja, ni kiashirio cha umoja kwamba, pamoja na kuwa watu wanatoka kwenye mataifa mbalimbali, bado wanaunganisha na Uislam.

“Watu wanakutana wakiwa na wadhifa tofauti, mataifa tofauti na uwezo tofauti lakini ndani ya mavazi yake, kila mmoja yupo sawa na mwingine, tunapaswa kuishi maisha ya namna hii,” amesema na kuongeza;

“Falsafa ya kurusha mawe kumpiga shetani ni kiashirio cha kujenga ujasiri katika kukabiliana na yale yote yanayoweza kumyumbisha muumini.”

Hata hivyo amewataka Waislam na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu kwa njia ya amani sambamba na kuchunga miiko na taratibu za dini hiyo popote watakapokuwa.

Akizungumzia tukio la tetemeko lililotokea jana Kanda ya Ziwa (Kagera, Mwanza, Mara, Shinyanga) na kusababisha vifo pia hasara Sheikh Ponda amewapa pole waliofikwa na mkasa huo.

“Nikiwa kama Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, natumia nafasi hii kuwapa pole wale wote waliofikwa na mkaza wa tetemeko la ardhi lililotokea jana Kanda ya Ziwa na nchi jirani.

“Yote yanayotokea yanaletwa na Mungu hivyo hatuna budi kujiandaa kwa kutenda mambo mema ili yatufae kwenye maisha baada ya dunia hii,” amesema.
 
Hawa ndo ma sheikh wenye akili na mungu amewaonyesha tunaelekea wapi si kama yule mwingine anayefanya siasa za tumbo
 
Wengi wanaolalamikia ugumu wa maisha wanasahau kwamba miradi mingi ya maendeleo ilikuwa inasimama kutokana na ukata kabla hata ya awamu ya sasa, kwa sasa miradi mingi ipo hai na mingine ipo njiani kuja itakayoweza kutoa ajira kwa maelfu kwa watanzania.
Miradi gani inafanyika ebu tuache ujuha na kufanya siasa za matumbo.
Mpaka leo wanafunzi vyuo vikuu hawajapata pesa ya PT/TP unategemea huko wanaishije?ujenzi wa uwanja wa jk nyerere terminal3 serikali imeshindwa kutoa hela ili uendelee alafu wanajifanya kuja na kigezo cha kitoto kama kile cha wanafunzi hewa,watu mtaani maisha magumu labda wewe mwenzetu unafaidika moja kwa moja kutoka kwa magu na umepigwa upofu kabisa na hautaki kuona wala kusikia matatizo yanayolikumba taifa
 
Achana na wale wanaowafananisha Maswahaba wetu vipenzi na wanasiasa.
Huyu ndiye hasa kiongozi asiye na chembe ya unafiki.
Sijui kwanini hakupewa Usheikh mkuu wa Tanzania baada ya kifo cha Simba.
Hivi alikuwa kifungoni bado au alikuwa keshaachiwa?
Mkono wa serikali ungekubali kuona hilo linatokea ?
 
Aisee sijawahi ona hii, sheikh analilia upigaji dili urudi ili watu wawe na furaha? Hakika huko mbinguni wataenda wachache.
 
Kwa kauli hii ya Sheikh Ponda, usikute masheikh wa BAKWATA wanaandaliwa kuja kujibu mapigo. Sijui uislam huu wa BAKWATA ni wa wapi! Wallah hakuna Sheikh wa BAKWATA atakayeiona Firdaus (Allah Subhannah wa Ta'allah anipe msamaha)
 
Hivi tunalamika kwa kukosa pesa kwa majukumu halali tuliyokuwa tukitekeleza ama majukumu ya ujanjaujanja. Tunahitaji kubadilika na si kulalamika hakuna hela huku umelala ama kukaa vijiweni bila ishu ya msingi. Mimi ninachokiona sio tu hakuna pesa ila wengi wetu tulizoea kupata pesa
Majukumu halali gani unayoyasema ? , watu wengine wameachishwa kazi , ww unabaki kukariri kwambwa wanaolalamika ni wavivu, biashara zimedorora
 
Back
Top Bottom