Sheikh Ponda: Furaha imetoweka, tutafakari upya

Sasa nimepata jibu la misukosuko iliyomkumba Sheikh Ponda, na Mungu kwa kuonesha utukufu wake yote mabaya yaliyolengwa kwa mja wake huyu yaligonga mwamba.
Ama kweli nimeamini msema mkweli ni mpenzi wa Mungu.
Ishi maisha marefu Sheikh Ponda...

Nami niwatakie Eid El Hajj waislam wenzangu kote ulimwenguni.
Sijawahi kujuta kukupenda we mama unaakili nyingi na unagonga ku nako
 
lini maisha yalikuwa rahisi, Maandiko matakatifu yanasema, Mwanadamu atakula kwa jasho, Nabii Ayubu anasema siku za mwanadamu si nyingi nazo zimejaa shida
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Uislam hauruhusu sigara ijekuwa shisha?
Kweli BAKWATA hii ya Lumumba kiboko!
Naona zile pesa haramu mkipewaga zimepotea mmejikita mitandaoni kulalamika. Tafuta kazi au jiajiri hazirudi tena. Sheikh wenu anataka kuhalalisha fedha haramu kwa furaha wakati dini yetu ya Kiislam kwenye suuratil baqra imetamka kukatazwa kwa ufisadi. Pesa haramu ndio zilizokuwa kwenye mzunguko hata Mungu hazipendi hivyo JPM anatekeleza amri ya Allah SW na kama utaipinga basi utakuwa umeikana Quran na umemkana Allah SW. Pesa chafu pesa za shetani ndizo zilizokuwa zinawapa furaha mitaani. Allah SW atamlinda Rais wetu kipenzi na mahasidi kama nyie na mafisadi
 
Achana na wale wanaowafananisha Maswahaba wetu vipenzi na wanasiasa.
Huyu ndiye hasa kiongozi asiye na chembe ya unafiki.
Sijui kwanini hakupewa Usheikh mkuu wa Tanzania baada ya kifo cha Simba.
Hivi alikuwa kifungoni bado au alikuwa keshaachiwa?
Si rahisi kupewa hicho cheo kwa sababu si mnafiki na ana misimamo thabiti.
na mtetea haki za waislam hao mashekh vilemba wa huko bakwata wasingemkubali.
 
FURAHA tuliyokuwanayo Watanzania, sasa haipo tena. Ni wakati wa kuhoji, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?, anaandika Faki Sosi.

Ni kauli ya Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taaisi za Kiislam Tanzania aliyoitoa leo akizungumza na mwandishi wa habari hii wakati akitoa salamu zake kuelekea Sikukuu ya Eid El Hajj.

Kesho duniani kote, waumini wa Dini ya Kiislam wanatarajia kusherehekea Sikukuu ya Eid el Hajj ikiwa ni sehemu ya ibada kwa mujibu wa imani ya dini hiyo.

Sheikh Ponda amesema, pamoja na kuwepo kwa sherehe hiyo lakini kuna hali ya masikitiko kwa Watanzania kutokana na vipato vya kushukwa jambo ambalo limeonda furaha ndani ya mioyo na familia zao.

Amesema, sikukuu zilizopita katika kipindi kama hiki watu waliweza kutoa sadaka, kulisha masikini, kuchinja kwa ajili ya ibada na kufanya ibada zingine zilizohusisha kipato.

Lakini kutokana na maisha kubadilika, waumini wa dini hiyo wameshindwa kutekeleza yale waliyokuwa wakiweza kuyatekeleza siku za nyuma jambo ambalo linahitaji kutafakari upya mtindo wa maisha ulivyo kwa sasa.

“Tunaelekea kwenye sikukuu lakini jambo ninaloliona kwa sasa ni kwamba, tunapaswa kutafakari upya, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?

“Siku za nyuma kulikuwa na furaha kubwa hasa wakati wa sikukuu kama huu lakini sasa mambo yamebadilika kwa kiwango kikubwa.

“Watu hawana furaha, maisha yamekuwa magumu. Ni kipindi cha kutafakari kwa mwaka mzima uliopita, tatizo ni nini zaidi?” amesema Sheikh Ponda.

Akizungumzia falsafa ya Hijja Sheikh Ponda amesema, yapo mambo mengi yanayopatikana pale watu wanapotekeleza ibada hiyo.

Amesema, miongoni mwa hayo ni pamoja na kuonesha umoja “kuvaa mavazi ya aina moja, ni kiashirio cha umoja kwamba, pamoja na kuwa watu wanatoka kwenye mataifa mbalimbali, bado wanaunganisha na Uislam.

“Watu wanakutana wakiwa na wadhifa tofauti, mataifa tofauti na uwezo tofauti lakini ndani ya mavazi yake, kila mmoja yupo sawa na mwingine, tunapaswa kuishi maisha ya namna hii,” amesema na kuongeza;

“Falsafa ya kurusha mawe kumpiga shetani ni kiashirio cha kujenga ujasiri katika kukabiliana na yale yote yanayoweza kumyumbisha muumini.”

Hata hivyo amewataka Waislam na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu kwa njia ya amani sambamba na kuchunga miiko na taratibu za dini hiyo popote watakapokuwa.

Akizungumzia tukio la tetemeko lililotokea jana Kanda ya Ziwa (Kagera, Mwanza, Mara, Shinyanga) na kusababisha vifo pia hasara Sheikh Ponda amewapa pole waliofikwa na mkasa huo.

“Nikiwa kama Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, natumia nafasi hii kuwapa pole wale wote waliofikwa na mkaza wa tetemeko la ardhi lililotokea jana Kanda ya Ziwa na nchi jirani.

“Yote yanayotokea yanaletwa na Mungu hivyo hatuna budi kujiandaa kwa kutenda mambo mema ili yatufae kwenye maisha baada ya dunia hii,” amesema.
Kwa kauli hiii Sheikh wangu nitakuheshimu maisha yangu yote na kuhaidi kula sikuku kwa kuwasaidia watu wasiojiweza.....NYie ndio viongiz wa din tunaowataka kwan kwa maneno yenu mnaisaidia serikali
 
Huyu ndio kiongozi wa waisilamu ninayemjua,sio wale wa ccm bakwata maana sii chombo cha waisilamu
Kama BAKWATA sio chombo cha Waislamu si muachane nacho? Nyie undeni vyombo mnavyoona ni vya Waislamu, simple and clear!
 
Achana na wale wanaowafananisha Maswahaba wetu vipenzi na wanasiasa.
Huyu ndiye hasa kiongozi asiye na chembe ya unafiki.
Sijui kwanini hakupewa Usheikh mkuu wa Tanzania baada ya kifo cha Simba.
Hivi alikuwa kifungoni bado au alikuwa keshaachiwa?
Unadhani ni rahisi tuuu kupewa usheikh mkuu kwa mtu yeyote

Wale ni zaidi ya usheikh mkuuuu.....usiulize swali jiongeze tuuu
 
Hivi tunalamika kwa kukosa pesa kwa majukumu halali tuliyokuwa tukitekeleza ama majukumu ya ujanjaujanja. Tunahitaji kubadilika na si kulalamika hakuna hela huku umelala ama kukaa vijiweni bila ishu ya msingi. Mimi ninachokiona sio tu hakuna pesa ila wengi wetu tulizoea kupata pesa
Hivi nitakwambia uniziburie mitaro yangu wakati cha kukulipa sina

Hakuna mwenye nafuu
 
FURAHA tuliyokuwanayo Watanzania, sasa haipo tena. Ni wakati wa kuhoji, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?, anaandika Faki Sosi.

Ni kauli ya Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taaisi za Kiislam Tanzania aliyoitoa leo akizungumza na mwandishi wa habari hii wakati akitoa salamu zake kuelekea Sikukuu ya Eid El Hajj.

Kesho duniani kote, waumini wa Dini ya Kiislam wanatarajia kusherehekea Sikukuu ya Eid el Hajj ikiwa ni sehemu ya ibada kwa mujibu wa imani ya dini hiyo.

Sheikh Ponda amesema, pamoja na kuwepo kwa sherehe hiyo lakini kuna hali ya masikitiko kwa Watanzania kutokana na vipato vya kushukwa jambo ambalo limeonda furaha ndani ya mioyo na familia zao.

Amesema, sikukuu zilizopita katika kipindi kama hiki watu waliweza kutoa sadaka, kulisha masikini, kuchinja kwa ajili ya ibada na kufanya ibada zingine zilizohusisha kipato.

Lakini kutokana na maisha kubadilika, waumini wa dini hiyo wameshindwa kutekeleza yale waliyokuwa wakiweza kuyatekeleza siku za nyuma jambo ambalo linahitaji kutafakari upya mtindo wa maisha ulivyo kwa sasa.

“Tunaelekea kwenye sikukuu lakini jambo ninaloliona kwa sasa ni kwamba, tunapaswa kutafakari upya, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?

“Siku za nyuma kulikuwa na furaha kubwa hasa wakati wa sikukuu kama huu lakini sasa mambo yamebadilika kwa kiwango kikubwa.

“Watu hawana furaha, maisha yamekuwa magumu. Ni kipindi cha kutafakari kwa mwaka mzima uliopita, tatizo ni nini zaidi?” amesema Sheikh Ponda.

Akizungumzia falsafa ya Hijja Sheikh Ponda amesema, yapo mambo mengi yanayopatikana pale watu wanapotekeleza ibada hiyo.

Amesema, miongoni mwa hayo ni pamoja na kuonesha umoja “kuvaa mavazi ya aina moja, ni kiashirio cha umoja kwamba, pamoja na kuwa watu wanatoka kwenye mataifa mbalimbali, bado wanaunganisha na Uislam.

“Watu wanakutana wakiwa na wadhifa tofauti, mataifa tofauti na uwezo tofauti lakini ndani ya mavazi yake, kila mmoja yupo sawa na mwingine, tunapaswa kuishi maisha ya namna hii,” amesema na kuongeza;

“Falsafa ya kurusha mawe kumpiga shetani ni kiashirio cha kujenga ujasiri katika kukabiliana na yale yote yanayoweza kumyumbisha muumini.”

Hata hivyo amewataka Waislam na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu kwa njia ya amani sambamba na kuchunga miiko na taratibu za dini hiyo popote watakapokuwa.

Akizungumzia tukio la tetemeko lililotokea jana Kanda ya Ziwa (Kagera, Mwanza, Mara, Shinyanga) na kusababisha vifo pia hasara Sheikh Ponda amewapa pole waliofikwa na mkasa huo.

“Nikiwa kama Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, natumia nafasi hii kuwapa pole wale wote waliofikwa na mkaza wa tetemeko la ardhi lililotokea jana Kanda ya Ziwa na nchi jirani.

“Yote yanayotokea yanaletwa na Mungu hivyo hatuna budi kujiandaa kwa kutenda mambo mema ili yatufae kwenye maisha baada ya dunia hii,” amesema.
Hakuna mtu aliyeng'anywa kipato halali. Watu wamezuiliwa vipato kharamu. Hivyo basi, wajifunze kuishi kutokana na vipato halali. Kama mnategemea au mnaomba Rais aruhusu watu waibe ili wawe na furaha sahauni!
 
Hawa jamaa si unamjua yule mnyama akielekea mmoja wote ndio hukohuko hata kama kuna maafa? Hata Rais JPM akitoka Ccm kwenda kwao wataanza kumsifia. Huyu Sheikh tumuombee kwa Mungu msamaha anataka kuhalalisha fedha haramu kwa furaha. Fedha haramu za wizi ndizo zilizokuwa kwenye mzunguko sasa zimedhibitiwa. Rais JPM atapata baraka za Mungu kupambana na maovu na mafisadi nchini kwani dini zote zinahubiri hivyo
Usini quote kisha kuweka upupu kama huu. Nani alikwambia wote walikuwa wanaishi kwa fedha haramu? Wewe huoni kila leo watu wanaachishwa kazi huko? Ndio uchumi gani huo? Wewe unaona taifa lina furaha yake iliyozoeleka miaka yote? Au unataka kumlisha maneno si yake sheikh ponda. Umuombee msamaha wewe huo wa kwako hujaweza kujiombea. Sray away!
 
Kama BAKWATA sio chombo cha Waislamu si muachane nacho? Nyie undeni vyombo mnavyoona ni vya Waislamu, simple and clear!
tumeunda Islamic foundation taasisi makini ndani ya mda mchache tu tuna radio imaan,TV imaan,morogoro Muslims university (mum) na mashule yskumwaga
 
Back
Top Bottom