Sheikh Ponda: Furaha imetoweka, tutafakari upya

Sheikh Ponda: Furaha imetoweka, tutafakari upya

Kwa kauli hii ya Sheikh Ponda, usikute masheikh wa BAKWATA wanaandaliwa kuja kujibu mapigo. Sijui uislam huu wa BAKWATA ni wa wapi! Wallah hakuna Sheikh wa BAKWATA atakayeiona Firdaus (Allah Subhannah wa Ta'allah anipe msamaha)
Mkuu umenichekesha saana , ingawa inauma
 
AMA kwa hakika JK atakumbukwa daima! baraka na neema vimetoweka vyote

ah ah team JK kt ubora wake.... siioni tofauti ndani ya ccm kwan walituahidi kuwa tutaisoma namba ila thanks God kwan na wao ccm wanaiso namba yao kama dawa
 
Huyu ndie sheikh pekee Tanzania anaejitambua na alieamua kusema haki bila kujali anamfurahisha binadamu wa madaraka gani aliyonayo ni mtu wa Mungu na anasema kutimiza amri za Mungu, haya ya kufurahisha wanasiasa amewaachia bakwata.
 
Sheikh Ponda ndio alitakiwa kuwa Mfuti Mkuu wa Tanzania
 
FURAHA tuliyokuwanayo Watanzania, sasa haipo tena. Ni wakati wa kuhoji, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?, anaandika Faki Sosi.

Ni kauli ya Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taaisi za Kiislam Tanzania aliyoitoa leo akizungumza na mwandishi wa habari hii wakati akitoa salamu zake kuelekea Sikukuu ya Eid El Hajj.

Kesho duniani kote, waumini wa Dini ya Kiislam wanatarajia kusherehekea Sikukuu ya Eid el Hajj ikiwa ni sehemu ya ibada kwa mujibu wa imani ya dini hiyo.

Sheikh Ponda amesema, pamoja na kuwepo kwa sherehe hiyo lakini kuna hali ya masikitiko kwa Watanzania kutokana na vipato vya kushukwa jambo ambalo limeonda furaha ndani ya mioyo na familia zao.

Amesema, sikukuu zilizopita katika kipindi kama hiki watu waliweza kutoa sadaka, kulisha masikini, kuchinja kwa ajili ya ibada na kufanya ibada zingine zilizohusisha kipato.

Lakini kutokana na maisha kubadilika, waumini wa dini hiyo wameshindwa kutekeleza yale waliyokuwa wakiweza kuyatekeleza siku za nyuma jambo ambalo linahitaji kutafakari upya mtindo wa maisha ulivyo kwa sasa.

“Tunaelekea kwenye sikukuu lakini jambo ninaloliona kwa sasa ni kwamba, tunapaswa kutafakari upya, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?

“Siku za nyuma kulikuwa na furaha kubwa hasa wakati wa sikukuu kama huu lakini sasa mambo yamebadilika kwa kiwango kikubwa.

“Watu hawana furaha, maisha yamekuwa magumu. Ni kipindi cha kutafakari kwa mwaka mzima uliopita, tatizo ni nini zaidi?” amesema Sheikh Ponda.

Akizungumzia falsafa ya Hijja Sheikh Ponda amesema, yapo mambo mengi yanayopatikana pale watu wanapotekeleza ibada hiyo.

Amesema, miongoni mwa hayo ni pamoja na kuonesha umoja “kuvaa mavazi ya aina moja, ni kiashirio cha umoja kwamba, pamoja na kuwa watu wanatoka kwenye mataifa mbalimbali, bado wanaunganisha na Uislam.

“Watu wanakutana wakiwa na wadhifa tofauti, mataifa tofauti na uwezo tofauti lakini ndani ya mavazi yake, kila mmoja yupo sawa na mwingine, tunapaswa kuishi maisha ya namna hii,” amesema na kuongeza;

“Falsafa ya kurusha mawe kumpiga shetani ni kiashirio cha kujenga ujasiri katika kukabiliana na yale yote yanayoweza kumyumbisha muumini.”

Hata hivyo amewataka Waislam na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu kwa njia ya amani sambamba na kuchunga miiko na taratibu za dini hiyo popote watakapokuwa.

Akizungumzia tukio la tetemeko lililotokea jana Kanda ya Ziwa (Kagera, Mwanza, Mara, Shinyanga) na kusababisha vifo pia hasara Sheikh Ponda amewapa pole waliofikwa na mkasa huo.

“Nikiwa kama Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, natumia nafasi hii kuwapa pole wale wote waliofikwa na mkaza wa tetemeko la ardhi lililotokea jana Kanda ya Ziwa na nchi jirani.

“Yote yanayotokea yanaletwa na Mungu hivyo hatuna budi kujiandaa kwa kutenda mambo mema ili yatufae kwenye maisha baada ya dunia hii,” amesema.
Ukijiuza kwa wale wanao nunua Mali za waaislamu basi utakuwa na furaha !! Uwanja ni wako
 
Akiwa kama sheikh anatakiwa atambue na kuwaelewesha waja wa mwenyezi mungu kwamba ni heri maisha magumu ya kipato halali kuliko maisha ya raha ya kipato kisicho halali(magumashi)kwani kipato cha magumashi furaha yake ni ya muda tu,na pia furaha ya kweli na ya kudumu duniani na akhera hupatikana kwa kumcha mwenyezi mungu huku ukifanya kazi kwa bidii na kuchuma kupitia njia halali.
 
Huyu bwana ni ndumila kuwili. Si ndo huyu amlimdhihaki rais Kikwete eti rais gani anachekacheka tuu, tena kwa kebehi. Leo amesahau na watu mnajitoa kumbukumbu. Rais Magufuli, moja ya watu unaotakiwa kuwadhibiti kwa makini ni huyu mchochezi mkubwa. Kama vipi tupa nje ya mipaka yetu. Nchi hii tunataka upendo, amani na utulivu.
 
Furaha itoke wapi wakati Mungu wa Ikulu anadhani kuongoza nchi ni kutoa kauli zilizojaa mihemuko na vitisho kila kukicha, mihemuko na vitisho ambavyo vinaharibu umoja na mshikamano nchini.

Kawaruhusu polisiccm wafanye mazoezi yao uraiani pamoja na kuwa wana makambi yao ili tu kuongeza hofu kubwa miongoni mwa Watanzania na kuuvuruga uchumi wa nchi kwa kipindi kifupi sana, ni lazima furaha nchini ipotee.
Of course mtu kama Sheikh Ponda atasema nini naye najuwa kuwa Rais hajaribiwi? LAzima hatakuwa na furaha!
 
Hivi umewasoma Watanzania mbali mbali wanavyosema kuhusu awamu hii!? Usiishi kama unaishi chini ya jiwe au labda unaukimbia ukweli ambao uko hadharani kweupe.

Of course mtu kama Sheikh Ponda atasema nini naye najuwa kuwa Rais hajaribiwi? LAzima hatakuwa na furaha!
 
Hivi umewasoma Watanzania mbali mbali wanavyosema kuhusu awamu hii!? Usiishe kama unaishi chini ya jiwe au labda unaukimbia ukweli ambao uko hadharani kweupe.
Mimi ni Mtanzania na ninaishi Tanzania. Tatizo la watanzania wengi wao wanapendapesa haramu. Yaani ilifikia to the extent mwenye fedha haramu ndio bingwa. Mwenye fedha alizopata kihalali hata akifanya nini anaonekana hana mipango. Back to the topic. Sasa hivi mifumu inaimarisha nk. lazima kutakuwa na matatizo. We una exposure ya kutosha hebu soma historia ya the big 5 ( nchi zile 5 zilizoendelea ikiwemo Malasia, Indonesia Nk.) waliko pitia. Ilipigwa marufuku kuagizia sijui luxury cars ( hata kwa wale wenye pesa) kutoka nchi za nje. Ukitaka mafanikia katika kitu chochote hata Kusoma tu say elimu ya juu lazima usacrifice baadhi ya mambo ila matunda yake utayaona baadae. Sasa Watanzania hawataki/ hawajazoeya hayo sababu ya kuzoea pesa ambayo mtu hajaifanyia kai. Let us be fair mnajudge mtu hata mwaka haujaisha. Tuvunilie kwa sasa in three years tutamuelewa Mh. Rais!
 
Wanaopenda pesa haramu ni wanasiasa wa CCM ikiwemo Magufuli na huu hapa ni ushahidi EPA, Radar, Kukwapua nyumba, Richmond/Dowans, Meremeta, Kagoda, Kuuzwa kwa NBC, Kuiba Kiwira Coal Mining, Lugumi, MV UFISADI, IPTL, ESCROW n.k. Haya yote yamefanywa na watu wakubwa sana Serikalini na ndani ya CCM na baadhi walishika nafasi ya URAIS lakini hakuna hata mmoja aliyepandishwa kizimbani wanahangaika na vidagaa tu lakini mapapa na manyangumi ya ufisadi nchini hayaguswi wanaendelea kukingiana kifua.

Mimi ni Mtanzania na ninaishi Tanzania. Tatizo la watanzania wengi wao wanapendapesa haramu. Yaani ilifikia to the extent mwenye fedha haramu ndio bingwa. Mwenye fedha alizopata kihalali hata akifanya nini anaonekana hana mipango. Back to the topic. Sasa hivi mifumu inaimarisha nk. lazima kutakuwa na matatizo. We una exposure ya kutosha hebu soma historia ya the big 5 ( nchi zile 5 zilizoendelea ikiwemo Malasia, Indonesia Nk.) waliko pitia. Ilipigwa marufuku kuagizia sijui luxury cars ( hata kwa wale wenye pesa) kutoka nchi za nje. Ukitaka mafanikia katika kitu chochote hata Kusoma tu say elimu ya juu lazima usacrifice baadhi ya mambo ila matunda yake utayaona baadae. Sasa Watanzania hawataki/ hawajazoeya hayo sababu ya kuzoea pesa ambayo mtu hajaifanyia kai. Let us be fair mnajudge mtu hata mwaka haujaisha. Tuvunilie kwa sasa in three years tutamuelewa Mh. Rais!
 
Mwenye akili ni lazima ajiulize.......why life is difficult?
maana mpaka mkulima nae anasema maisha ni magumu!....hivi nae alikuwa fisadi? au mzunguko wa pesa za kifisadi ulikuwa unamfikia na kufurahia maisha?
Au mishahara imeshuka? kwanini maisha yawe magumu?
Kama serikali inabana matumizi.....pesa zinazopatikana zinalingana na ujenzi wa uchumi wetu au kasi ni sawa na kipindi kilichopita?
 
FURAHA tuliyokuwanayo Watanzania, sasa haipo tena. Ni wakati wa kuhoji, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?, anaandika Faki Sosi.
Ni kauli ya Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taaisi za Kiislam Tanzania aliyoitoa leo akizungumza na mwandishi wa habari hii wakati akitoa salamu zake kuelekea Sikukuu ya Eid El Hajj.

Kesho duniani kote, waumini wa Dini ya Kiislam wanatarajia kusherehekea Sikukuu ya Eid el Hajj ikiwa ni sehemu ya ibada kwa mujibu wa imani ya dini hiyo. Sheikh Ponda amesema, pamoja na kuwepo kwa sherehe hiyo lakini kuna hali ya masikitiko kwa Watanzania kutokana na vipato vya kushukwa jambo ambalo limeonda furaha ndani ya mioyo na familia zao.

Amesema, sikukuu zilizopita katika kipindi kama hiki watu waliweza kutoa sadaka, kulisha masikini, kuchinja kwa ajili ya ibada na kufanya ibada zingine zilizohusisha kipato. Lakini kutokana na maisha kubadilika, waumini wa dini hiyo wameshindwa kutekeleza yale waliyokuwa wakiweza kuyatekeleza siku za nyuma jambo ambalo linahitaji kutafakari upya mtindo wa maisha ulivyo kwa sasa.

“Tunaelekea kwenye sikukuu lakini jambo ninaloliona kwa sasa ni kwamba, tunapaswa kutafakari upya, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?
“Siku za nyuma kulikuwa na furaha kubwa hasa wakati wa sikukuu kama huu lakini sasa mambo yamebadilika kwa kiwango kikubwa.

“Watu hawana furaha, maisha yamekuwa magumu. Ni kipindi cha kutafakari kwa mwaka mzima uliopita, tatizo ni nini zaidi?” amesema Sheikh Ponda.
Akizungumzia falsafa ya Hijja Sheikh Ponda amesema, yapo mambo mengi yanayopatikana pale watu wanapotekeleza ibada hiyo.

Amesema, miongoni mwa hayo ni pamoja na kuonesha umoja “kuvaa mavazi ya aina moja, ni kiashirio cha umoja kwamba, pamoja na kuwa watu wanatoka kwenye mataifa mbalimbali, bado wanaunganisha na Uislam.

“Watu wanakutana wakiwa na wadhifa tofauti, mataifa tofauti na uwezo tofauti lakini ndani ya mavazi yake, kila mmoja yupo sawa na mwingine, tunapaswa kuishi maisha ya namna hii,” amesema na kuongeza;

“Falsafa ya kurusha mawe kumpiga shetani ni kiashirio cha kujenga ujasiri katika kukabiliana na yale yote yanayoweza kumyumbisha muumini.”
Hata hivyo amewataka Waislam na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu kwa njia ya amani sambamba na kuchunga miiko na taratibu za dini hiyo popote watakapokuwa.

Akizungumzia tukio la tetemeko lililotokea jana Kanda ya Ziwa (Kagera, Mwanza, Mara, Shinyanga) na kusababisha vifo pia hasara Sheikh Ponda amewapa pole waliofikwa na mkasa huo.

“Nikiwa kama Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, natumia nafasi hii kuwapa pole wale wote waliofikwa na mkaza wa tetemeko la ardhi lililotokea jana Kanda ya Ziwa na nchi jirani.

“Yote yanayotokea yanaletwa na Mungu hivyo hatuna budi kujiandaa kwa kutenda mambo mema ili yatufae kwenye maisha baada ya dunia hii,” amesema.
Asiefanya kazi hatapata chakula,endeleeni kunywa kahawa na kashata kuanzia SAA 11 asubuhi mpaka saa tatu usiku
 
Wanafki wakubwa nyie. Mbona alipopigwa risasi mlipenda angeuliwa kabisa. Leo kawa sio gaidi kwenu? Mwaka huu mtapanda mpaka mpapai kujikinga na hasira za tembo.
Big up mkuu! kwa kuliona hilo,eti wanasema shekhe sio mnafiki tangu utawala uliopita hali yakuwa wao ndo wanafik kuanzia utawala huu na uliyopita.
 
Back
Top Bottom