Haki ipi aliyozungumz hapo? Acheni unafiki.Kabisa... kama ni haki anazungumza
Ngosha hataki mchezo,kazi kwanza,kama hufanyi kazi unataka kukaa kwenye kibaraza halafu unataka kuchinja kwenye eid utakuja kuchinja nyanya chungu zako,mwenyezi mungu amlinde na ampe mwisho mwema. amiin
Huna ulijualo kaa kimya... au kipofu nini wewe..?Haki ipi aliyozungumz hapo? Acheni unafiki.
hebu elezea huo unafiki mkuu?Nimeshuhudia kiwango cha juu cha unafiq wa baadhi ya wana JF kupitia Uzi huu
Watu ambao wamemkejeli Ponda kwa kumwita majina yote dhalili, waliofurahia alipokuwa mahabusu na waliofurahia kupigwa kwake risasi eti leo wanamsupport Ponda na kumwita shujaa. Ni unafiq wa kiwango cha mwendo kasihebu elezea huo unafiki mkuu?
Lazima uangalie na binadamu wenzako sio unakula vizuri af wengine wanateseka, ndo alichomaanisha sio kwamba yy ana maisha magumuNgosha hataki mchezo,kazi kwanza,kama hufanyi kazi unataka kukaa kwenye kibaraza halafu unataka kuchinja kwenye eid utakuja kuchinja nyanya chungu zako,
Hapa kazi tu!
Acheni kumvika shekhe kilemba cha ukoka kwa unafiki wenu uliyopindukia.Huna ulijualo kaa kimya... au kipofu nini wewe..?
Hivi tunalamika kwa kukosa pesa kwa majukumu halali tuliyokuwa tukitekeleza ama majukumu ya ujanjaujanja. Tunahitaji kubadilika na si kulalamika hakuna hela huku umelala ama kukaa vijiweni bila ishu ya msingi. Mimi ninachokiona sio tu hakuna pesa ila wengi wetu tulizoea kupata pesa
Furaha itoke wapi wakati Mungu wa Ikulu anadhani kuongoza nchi ni kutoa kauli zilizojaa mihemuko na vitisho kila kukicha, mihemuko na vitisho ambavyo vinaharibu umoja na mshikamano nchini.
Kawaruhusu polisiccm wafanye mazoezi yao uraiani pamoja na kuwa wana makambi yao ili tu kuongeza hofu kubwa miongoni mwa Watanzania na kuuvuruga uchumi wa nchi kwa kipindi kifupi sana, ni lazima furaha nchini ipotee.
Endelea kuishi kwa shemeji yako, siku ukifukuzwa utatia akili na kujua kilichokuwa kinamaanishwa hapa ni nini hasa.Hivi tunalamika kwa kukosa pesa kwa majukumu halali tuliyokuwa tukitekeleza ama majukumu ya ujanjaujanja. Tunahitaji kubadilika na si kulalamika hakuna hela huku umelala ama kukaa vijiweni bila ishu ya msingi. Mimi ninachokiona sio tu hakuna pesa ila wengi wetu tulizoea kupata pesa
FURAHA tuliyokuwanayo Watanzania, sasa haipo tena. Ni wakati wa kuhoji, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?, anaandika Faki Sosi.
Ni kauli ya Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taaisi za Kiislam Tanzania aliyoitoa leo akizungumza na mwandishi wa habari hii wakati akitoa salamu zake kuelekea Sikukuu ya Eid El Hajj.
Kesho duniani kote, waumini wa Dini ya Kiislam wanatarajia kusherehekea Sikukuu ya Eid el Hajj ikiwa ni sehemu ya ibada kwa mujibu wa imani ya dini hiyo. Sheikh Ponda amesema, pamoja na kuwepo kwa sherehe hiyo lakini kuna hali ya masikitiko kwa Watanzania kutokana na vipato vya kushukwa jambo ambalo limeonda furaha ndani ya mioyo na familia zao.
Amesema, sikukuu zilizopita katika kipindi kama hiki watu waliweza kutoa sadaka, kulisha masikini, kuchinja kwa ajili ya ibada na kufanya ibada zingine zilizohusisha kipato. Lakini kutokana na maisha kubadilika, waumini wa dini hiyo wameshindwa kutekeleza yale waliyokuwa wakiweza kuyatekeleza siku za nyuma jambo ambalo linahitaji kutafakari upya mtindo wa maisha ulivyo kwa sasa.
“Tunaelekea kwenye sikukuu lakini jambo ninaloliona kwa sasa ni kwamba, tunapaswa kutafakari upya, kwanini maisha yamekuwa magumu kiasi hiki?
“Siku za nyuma kulikuwa na furaha kubwa hasa wakati wa sikukuu kama huu lakini sasa mambo yamebadilika kwa kiwango kikubwa.
“Watu hawana furaha, maisha yamekuwa magumu. Ni kipindi cha kutafakari kwa mwaka mzima uliopita, tatizo ni nini zaidi?” amesema Sheikh Ponda.
Akizungumzia falsafa ya Hijja Sheikh Ponda amesema, yapo mambo mengi yanayopatikana pale watu wanapotekeleza ibada hiyo.
Amesema, miongoni mwa hayo ni pamoja na kuonesha umoja “kuvaa mavazi ya aina moja, ni kiashirio cha umoja kwamba, pamoja na kuwa watu wanatoka kwenye mataifa mbalimbali, bado wanaunganisha na Uislam.
“Watu wanakutana wakiwa na wadhifa tofauti, mataifa tofauti na uwezo tofauti lakini ndani ya mavazi yake, kila mmoja yupo sawa na mwingine, tunapaswa kuishi maisha ya namna hii,” amesema na kuongeza;
“Falsafa ya kurusha mawe kumpiga shetani ni kiashirio cha kujenga ujasiri katika kukabiliana na yale yote yanayoweza kumyumbisha muumini.”
Hata hivyo amewataka Waislam na Watanzania kwa ujumla kusherehekea sikukuu kwa njia ya amani sambamba na kuchunga miiko na taratibu za dini hiyo popote watakapokuwa.
Akizungumzia tukio la tetemeko lililotokea jana Kanda ya Ziwa (Kagera, Mwanza, Mara, Shinyanga) na kusababisha vifo pia hasara Sheikh Ponda amewapa pole waliofikwa na mkasa huo.
“Nikiwa kama Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam Tanzania, natumia nafasi hii kuwapa pole wale wote waliofikwa na mkaza wa tetemeko la ardhi lililotokea jana Kanda ya Ziwa na nchi jirani.
“Yote yanayotokea yanaletwa na Mungu hivyo hatuna budi kujiandaa kwa kutenda mambo mema ili yatufae kwenye maisha baada ya dunia hii,” amesema.
watu wanakuja na majibu rahisi kwa maswali magumu, wanasema tumezoea pesa za deal, ni tabu kweli kweliLeo mida ya saa tano asubuhi nilikuwa ninasomba tumifuko twangu twa saruji kwenye kabaiskeli, njiani nikawakuta watu wamesimama wanajadili hali ilivyongumu, wakawa wanasema "Kwa jinsi hali ilivyongumu, nibora kufukuza mke mmoja aende kwao ubaki na mmoja mpaka hali itakapo kuwa nzuri" niliwaza sana japo nilisikia kidogo sana. Nikasema mimi mwenyewe nimenunua vimifuko 10 vya saruji nikaona nisombe kwa baiskel ku-save 10,000/= kumbe hali si "taiti" kwangu tu. Jamani mambo magumu saanaa.
tatizo letu wabongo ni chuki, utakuta mtu anamchukia mwingine kwa sababu sio kabila au dini yake,Watu ambao wamemkejeli Ponda kwa kumwita majina yote dhalili, waliofurahia alipokuwa mahabusu na waliofurahia kupigwa kwake risasi eti leo wanamsupport Ponda na kumwita shujaa. Ni unafiq wa kiwango cha mwendo kasi