Kipara Kipya,
Unajaribu kumtazama
Sheikh Ponda katika sura ya siasa ukiaminni kuwa
kwa kuwa ni sheikh hastahili kuwa mwanasiasa.
Uhuru wa Tanganyika una mashujaa wengi katika siasa ambao walikuwa
masheikh.
Hawa walikuwa mstari wa mbele katika kupambana na dhulma za wakoloni.
Kulikuwa na
Sheikh Hassan bin Amir na
Sheikh Said Chaurembo katika
TAA - Political Subcommittee.
Hii ilikuwa 1950.
Kulikuwa na
Sheikh Mohamed Ramiyya wa Bagamoyo katika TAA na TANU.
Kulikuwa na
Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa
TANU.
Kulikuwa na
Sheikh Yusuf Badi wa Lindi katika TANU.
Kulikuwa na
Sheikh Rashid Sembe shujaa wa Kura Tatu katika mkutano wa
TANU kujadili Uchaguzi Mkuu wa mwaka wa 1958.
Mifano iko mingi inachotakiwa ni kwa wewe kuisoma historia ya TANU na
uhuru wa Tanganyika itakudhihirikia kuwa masheikh siku zote wamekuwa
mstari wa mbele katika kupambana na dhulma ya aina yoyote katika jamii.
Kushoto kwa Baba wa Taifa ni Sheikh Suleiman Takadir katika mkutano wa TANU wakati wa kupigania uhuru wa
Tanganyika