Dr Slaa mwaka gani alikuwa askofu? Jimbo gani hilo alikuwa askofu?
Msipoteze muda wenu kufanya argument na mtu ambaye inaonekana hajui chochote zaidi ya kusoma na kuandika.
Kwa hoja ya huyu bwana, hata Desmon Tutu alistahili kuacha kuwa Askofu Mkuu kwa sababu alikuwa akipinga wazi sera za ubaguzi wa rangi.
Kiongozi yeyote wa dini, ambaye kweli ni kiongozi wa dini, kamwe hawezi kuacha kukemea uonevu katika jamii. Kiongozi wa kweli wa dini ni lazima asimame na awe sauti ya wanyonge wanaodhulumiwa, na awe tayari kuteseka na hata kufa kwaajili ya kuwatetea.
Ponda kama angetaka kuwa mbunge, kazi ambayo ina mshahara, asingekosa, lakini ameamua daima kuwa sauti ya wasio na uwezo wa kusema. Ameteseka, amefungwa, amenusurika kuuawa lakini hakutoka kwenye yale anayoyaamini. Huyo ndiye kiongozi wa dini.
Papa Francisco, alipohutubia zaidi ya waumini milioni moja kwenye kongamano la vijana wakatoliki kule Brazil, alisema, 'Kanisa ni lazima lisimame na watu wanyonge maskini, liache kujishikamanisha na matajiri na watawala hata watu wakaona Kanisa ni sehemu ya watawala'. Viongozi wa Kanisa Katoliki wanatakiwa kuiishi kauli hii ya kiongozi mkuu ambaye ni Mama Kanisa. Na kwa mwongozo wa Kanisa Katoliki, Mama Kanisa ndiye mwenye kauli ya mwisho kuhusu uongozi na imani ya Kanisa Katoliki.