Sheikh Ponda akamatwa Dar!

.. safi sana sasa wasimcheleweshe kwa kuwa hakuna cha upelelezi kukamilika wala dhamana yeye moja kwa moja mahakamani na ushahidi upo ... maana ana makosa mengi sana .........hukumu isicheleweshwe labda tutapumzika..........
 
Yamekuwa yakisemwa mengi kwa muda mrefu juu ya harakati hizi za kiislamu Tanzania lakini imekuwa ni bahati mbaya sana mara zote yamekuwa yakichukuliwa kisiasa zaidi. At least, kwa hili la Mbagala na kule Zanzibar it is now obvious about the agenda behind these movements. Mwenye ufahamu na afahamu sasa.
 
Ni taarifa za kweli na aliwindwa kwa siku tatu... huenda hatua kubwa zaidi zitachukuliwa kwa Redio Imani.

Waache ujinga, tumeshapiga sana kelele kuhusu double standards za hii serikali. Serikali yenyewe inaangalia masuala ya uvunjaji sheria kidini dini, mbona Mwanahalisi walilifungia tena kwa kutumia sheria za kikandamizaji na bila ushahidi? M
bina Mch Mtikila wamemkamata mara kadhaa kwa makosa kama ya Sheikh Ponda?
Wanaudhi kweli hawa viongozi wetu, ni waoga kama nini.
 
katika uislam kufungwa ni sunna ya nabii yusuph a.s, kuuwawa katika kuipiginia dini ya haki ni kuwa unajitengenezea free pass yako ya JANNAH (pepo) so wamkamate wamfunge wamuue wanachofanya ni kumtengenezea pepo yake tu,umma mkubwa upo nyuma yake na harakati zinaendelea kwani hata ponda tunamfata kwa kuwa anafata mafundisho ya quran, so ponda kakamatwa ila quran (mwongozo) umebaki tena sio kwenye makaratasi tu bali vifuani.
 
THANKS GOD I"V BORN A MUSLIM N INSHALLAH I WILL DIE A MUSLIM
I LOVE THIS RELIGION MORE THAN JUST MY LIFE
ALSO THANKS GOD FOR HAVIN A STRONG MAN LIKE PONDA
GO PONDA,TUPO NYUMA YAKO BROTHER...!!!
:tea::amen:
 


Mkuu Lukolo, tAtizo si kumpa uongozi Muislamu. Kuna waislamu waelewa na waislamu wenye IQ za Kuku. Tatizo linakuja mnapompa uongozi Muislam mwenye IQ ndogo, yaan asiye na upeo mpana wa mambo. Muislam ambaye elimu kubwa sana aliyopata ni haki ya kuona wake wengi na kufuga majini hatajua religious tolerance inakuwaje. Muislam mwenye akili tosha anajua Uislamu na Ukristo ni dini ndugu. Kwa hiyo hapa swali gumu ni hili: tumeweka Waislam wa aina gani katika uongozi. Tumeweka Waelewa? au wenye IQ za kuku? Na ni chama gani kimetufikisha hapo?
 

Acha kushabikia ujinga. Kwa hiyo Quran inaruhusu mauaji?
Inaruhusu unafiki na uchochezi? Inaruhusu ugaidi na wizi?
Maana kila wanapochoma makanisa au kufanya vurugu
nasikia huwa wanapora vitu. Msitake kuhalalisha maasi kwa
kutumia kivuli cha dini au kitabu...
 
Ikifungwa radio Iman ujue nchi haitatawalika milele.
So ondoa povu lako.
Ukitaka kumtawala mtu, basi mtie hofu, hofu ikimtawala mtu, atakuwa mtumwa wa hofu.
Nchi gani imeshindwa kutawalika kwa sababu ya Waislamu? Tupe mfano basi.
 
Sidhani kama kumkamata huyu shehk ni suruhisho la mgogolo huu tukumbuke matukio mbali mbali yaliyotokea

1. Kule Mbagala sidhani kama alikuwepo
2. Tumesikia Makanisa yamechomwa moto kule Kigoma sidhani kama alikuwepo
3. Pia kuna Uamsho kule Zenji nako sijui tunasemaje

** Tatizo hapa ni utawala mbovu wa CCM ambao kwa njia moja unataka kutugawa watanzania katika matabaka ili tusiwe na umoja na wao waendelee kututawala. Tumesikia viongozi mbali mbali wa CCM wakisema CDM ni chama cha Kidini, Kikabila na cha kikanda, CUF nao wakaja na msemo kama CDM kinabagua Waislam basi waislam wote kwa umoja wenu njooni mjiunge CUF na CCM ikabaki ikijinadi kuwa ni chama kisichobagua jamii yote ya watanzania.**

Kitendo cha kumkamata Huyu Shehk akina matokeo yeyote tofauti mwisho wa siku ataachiwa huru kwani sidhani kama kuna kosa lolote litakalomtia hatiani pindi atakapopandishwa kizimbani.
 
Kiukweli serikali yetu haina pa kukwepea lawama za uchochezi wa kidini kwani kila wakati wamefumbia macho mambo hayo tazama yaani kila siku maeneo mbalimbali ya nchi kuna mihadhara inayokashfu dini za watu na hao hawachukuliwi hatua yoyote. Kiukweli serikali yetu ni dhaifu.
 
Ume-argue vyema. Ila bado ninaona kuna point una-miss kuielewa mkuu. Je kufunga kwako mlango kutarudisha wale mbuzi walioliwa na chui? Je mbuzi waliobahatika kubaki, watakuwa na mtazamo gani juu yako wewe? wakati wao wanaona kabisa hakukuwa na sababu ya msingi ya kuacha zizi wazi. Kibaya zaidi zizi la ng'ombe jirani ya hili la mbuzi ulikuwa umelifunga very intact. Nini cha kufanya sasa? Inabidi kushughulika na mzizi wa tatizo. Msimamizi wa zizi awe answerable. Uwajibikaji. Tukienda kuwauwa chui, nakuhakikishia upepo ukipita zizi litaachwa wazi tena. Hebu tuiangalie hii picha.
 
Sasa ni muda mwafaka kwa waislam kutambua kuwa quran ni kitabu cha kawaida, tumesikia sehemu mbalimbali duniani qurani ikichomwa moto lakini hakuna madhara yanayowapata wahalifu zaidi ya hasira za wanadamu.

Tuwafundishe watoto wetu kuwa qurani ni kitabu kitakatifu na cha kuheshimiwa ila hakina maajabu yoyote...wakristu tunafundishwa kuwa Biblia ni ni maandiko matakatifu ila hayana miujiza, mkazo upo kwenye imani hivyo mkristu ukikojolea au kuchoma biblia yeye hapaniki kwa sababu umeweza kuchoma biblia lakini huwezi kuchoma imani yake ndani ya moyo wake.!!
 
Huyu jamaa aweza kuwa mwanaharakati!!Naomba mnijuze hiv ponda huyu ndio yule wa mwembechai 1998 mkapa akiwa president?
 
Naungana na wewe Mkuu, Mwanakijiji kwa hoja yake kachemka. Serikali inatakiwa kumchukulia hatua kali za kisheria pale itakapogundulika amefanya uchochezi wowote wa kuchafua amani ya nchi.

Huwezi kumwacha mtu kuendelea kuharibu amani ya nchi kwa sababu tu ya kosa la kwanza la kutokumshughulikia mtu huyo.

Hilo lilikuwa ni kosa na serikali wameliona na kuanza kulishughulikia. Kituko cha ajabu kitakuwa tu pale watakapogundua ana makosa then waache kumchukulia hatua za kisheria.
 
Walifanya Zanzibar tukawaangalia, sasa wamenogewa na wakaamua kuliendeleza mpaka Tanganyika. Serikali ilikosea kutoa kauli nyepesi kwa wale wezi na wapumbavu waliochoma makanisa Zanzibar.
Hawa waliokamatwa kuhusu mbagala inabidi wawe mfano kwa wengine watakaopata hamu ya kufanya upumbavu kama wao. Wafungwe na walipe fidia.
Haki za mtoto Emmanuel zizingatiwe, kesi yake ikasikilizwe katika mahakama za watoto kama Lulu anavyopigania.
NB: Sifurahii kitendo cha kukojolea kitabu cha waislamu bali inakasirisha kuona watu walivyojichukulia hatua bila kutumia akili. Yaani katoto kadogo kamewavua nguo watu wazima!
Nawaheshimu waislamu na nitaendelea kuwapenda (ukiondoa hawa wapuuzi wachache)
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…