Sheikh Ponda aanza tena kuchafua hali ya hewa

Sheikh Ponda aanza tena kuchafua hali ya hewa

Status
Not open for further replies.
Ndugu wana JF nimesoma magazeti ya leo yameripoti habari ya huyu Sheikh Ponda Issa Ponda kuchochea fujo na uvunjifu wa amani kule Zanzibar. Je kwanini asifungwa hata miaka 20 kwa manufaa ya umma??
Hayo ni maoni yangu. I am stand to be corrected

source magazeti ya leo; Habari leo, Mwananchi , Tanzania daima n.k.

cheer
halihali

Kesi yake ya mwisho alipewa kifungo cha nje kwa masharti kwamba asifanye tena mambo ya uchochezi. Suala ni kuangalia kama amekiuka masharti aliyopewa.

Juu ya hilo kuna ukweli gani gani kwamba huyu jamaa ni mrundi?
 
Kama imethibitika kavunja sheria za nchi kwa mujibu wa katiba anafungwa tuh,sasa kama unaona hilo halifanyiki iulize serikali yako,unless otherwise kila mtu ana haki ya kuongea kile anachoona kinafaa ili mradi tuh havunji sheria za nchi,wengine wakisema kile wanachokiamini huitwa wachochez,so usiamini kila unachokisoma kwenye magazaeti,especially kama haya ya uhuru,mzalendo,tanzania daima,mwananchi & likes,wengi wao wako na doublestandards sana....
 
Sheikh Ponda alisha sema wazi kuwa yeye hata akifanya jambo gani hawezi kufungwa, sanasana watampumzisha tu lupango kwani yeye ana nguvu ya ushawishi, na hao watu wake watiifu akifungwa watafanya nchi isitawalike.

ndo maana ana kiburi sana huyo Ponda Sheikh?
 
Ndugu wana JF nimesoma magazeti ya leo yameripoti habari ya huyu Sheikh Ponda Issa Ponda kuchochea fujo na uvunjifu wa amani kule Zanzibar. Je kwanini asifungwa hata miaka 20 kwa manufaa ya umma??
Hayo ni maoni yangu. I am stand to be corrected

source magazeti ya leo; Habari leo, Mwananchi , Tanzania daima n.k.

cheer
halihali

rekebisha hiyo "I am" kwanza kisha nitachangia
 
Ingekuwa ni Emanuel angekuwa ndani mida hii,hata ivyo huwa magamba wanamtumi kisiasa
 
Maccm wapeni waislam HAKI zao mlizo zibaka.
ahahahahaha haki gani za waslamu zilizobakwa ??? serikali haina dini ukisema eti imebaka unakosea na kuifanya ionekane inakandamiza jamii ya dini flani....mimi sio mwana ccm, ni mtanzania na tanzania hamna udini.
 
Ndugu wana JF nimesoma magazeti ya leo yameripoti habari ya huyu Sheikh Ponda Issa Ponda kuchochea fujo na uvunjifu wa amani kule Zanzibar. Je kwanini asifungwa hata miaka 20 kwa manufaa ya umma??
Hayo ni maoni yangu. I am stand to be corrected

source magazeti ya leo; Habari leo, Mwananchi , Tanzania daima n.k.

cheer
halihali
Lipumba na Cuf yake walifanya jitihada nyuma ya pazia asifungwe kwa sababu za udini. Kama inavyodhihirika Issa Ponda ni mtu hatari kwa mstakabali na umoja wa taifa. Ni mchochezi wa kidini mzoefu na hajawahi kuishi kwa jasho ila ulaghai na uchochezi wa kidini kuleta mfarakano kwa waislaam na jamii kwa ujumla. Kifungo cha nje kwa Issa Ponda sio haki. Stahiki ni kwa yeye kua jela. Kwa kua amevunja sharti la kifungo cha nje akina lipumba wakae pembeni wakati issa ponda anawekwa lupango.
 
rekebisha hiyo "I am" kwanza kisha nitachangia

Scramble - we changia tu. Unajua tena matatizo yetu ya lugha za watu Bongo! Nadhani umepata hoja yake, ndiyo la msingi. Unaweza pia kuandika kwa lugha hiyo ukajikuta nawe pia unafanya makosa.
 
Serikali iache kuingilia taasisi za Kiislamu na kulazimisha wote wawe chini ya BAKWATA.Suluhisho sio kukamata watu

Inategemea tafsiri ya neno tusi ni nini!

Tunajua mko nyuma ya huu upuuzi ndo maana mnashabikia.
 

[TD="bgcolor: #FFFFFF"]CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar kimemtuhumu Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, kuwa anaendesha kampeni za uchochezi wa kidini.
Uchochezi huo umedaiwa kuhatarisha amani ya nchi, hivyo kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumchukulia hatua za kisheria.
Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu (NEC) Zanzibar, Itikadi na Uenezi, Waride Bakari Jabu, alisema jana kuwa ni wiki moja sasa tangu Ponda afanye mihadhara kwenye misikiti ya Mbuyuni, Kwarara na Nungwi kisiwani Unguja.
Waride alisema kuwa hotuba za Sheikh Ponda alizozitoa kwa nyakati tofauti kwenye misikiti hiyo zinapandikiza mbegu ya chuki, kuondosha upendo na kuhatarisha amani.
Alisema matamshi yake ni hatarishi kwa amani na utulivu uliopo, kwani anawataka Waislamu kupigana vita ya dini (Jihad) na kushiriki harakati za kuikomboa Zanzibar, kwa madai kuwa serikali iliyoko madarakani inawakandamiza na kuwanyanyasa wananchi.
“Sheikh Ponda ni hatari, anapanda shari na chuki miongoni mwa wananchi, anahamasisha wananchi wafanye uasi, kulipiza visiasi na kutaka waingie barabarani kwa maanadano ya kutetea haki kama inavyotokea Misri,” alisema.
Aidha, alisema CCM imeshangazwa na ukimya wa vyombo vya ulinzi na usalama wa raia kumtazama kiongozi huyo bila ya kumchukulia hatua za kisheria wakati akiwatukana matusi ya nguoni viongozi wa serikali na chama tawala.
Aliongeza kuwa Sheikh Ponda huenda anatumiwa na mtandao wa vurugu ili kuharibu na kuvuruga amani ambapo hamu yake ni kuona damu ya wananchi ikimwagika na nchi ikiingia kwenye machafuko.
Kwa mujibu wa Waride, kitendo cha Ponda kulitumia jukwaa la dini na kufanya siasa misikitini hakikubaliki na kwamba kikiachiwa kiendelee kinaweza kuleta madhara na mgawanyiko.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alisema jeshi hilo limeanza kumtafuta Sheikh Ponda tangu walipopokea taarifa za kuendesha mihadhara ya uchochezi katika baadhi ya misikiti, ikiwa na lengo la kuibua chuki.
Mussa alisema kitendo anachokifanya kinakwenda kinyume cha sheria, hivyo kumtaka popote alipo ajisalimishe kwa hiari yake.
Tangu kuingia visiwani Zanzibar, Sheikh Ponda amekuwa akifungamana na viongozi wa Jumuiya ya Uamsho wakipinga kitendo cha viongozi wa jumuiya hiyo kuendelea kubakia mahabusu baada ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uharibifu wa mali na kuhatarisha usalama wa taifa.
Viongozi hao wa Uamsho wako mahabusu baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, kuwasilisha ombi la kufunga dhamana yao kwa kutumia sheria ya Usalama wa Taifa na marekebisho yake ya mwaka 2002


[TD="bgcolor: #ffffff"]


na Hassan Ali Ame, Zanzibar


[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #ffffff, align: center"] <a href="http://adserver.adtech.de/adlink/3.0/1332/4486816/0/357/ADTECH;loc=300" target="_blank"><img src="http://adserver.adtech.de/adserv/3.0/1332/4486816/0/357/ADTECH;loc=300" border="0" width="200" height="600"></a> [/TD]
[/TD]
 
Kama wameshindwa kumpata Shehe Ilunga mpaka leo wataweza kumkamata Ponda tena!!

Shehe Ponda na Ilunga wanapata ufadhili kupitia fedha zinazotoka na hiyo huduma yao ya Islamic Banking-hizi pesa ndo wanazofanyia kampeni chafu dhidi ya dini ya Kikristo na kutengeneza CD za uchochezi.
 
Hivi wenye kifungo cha nje wanaruhusiwa kuvuka mipaka ya nchi?
 
Ponda jembe la wasilam,na watanzania walala hoi kiujumla haogopi wala nini chezea ponda wewe? Huo ndiyo msimamo unaotakiwa na allah.
 
Serikali iache kuingilia taasisi za Kiislamu na kulazimisha wote wawe chini ya BAKWATA.Suluhisho sio kukamata watu

Inategemea tafsiri ya neno tusi ni nini!

ben saanane huo sasa inahitaji mtindio wa ubongo kusapoti, harakati za mpu..mba..vu Ponda
 
Wewe haliali ponda hawapondi wakristo yeye anawaponda ccm na serikali yake jinsi inavyowabagua wasilamu wa tz na kuwapaisha wakristo yani serikali kuweka
 
Ponda jembe la wasilam,na watanzania walala hoi kiujumla haogopi wala nini chezea ponda wewe? Huo ndiyo msimamo unaotakiwa na allah.

huuu sasa wehu. utamsapoti vp mcheza karate na mteka.misikiti. ponda ni mwe.huuuu na anatakiwa kutokomezwa kama.wale wengine wa UAMSHO
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom