Sheikh Ponda aanza tena kuchafua hali ya hewa

Status
Not open for further replies.
Zanzibar. Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimeitaka Serikali kumtiambaroni na kumchukulia hatua za kisheria Sheikh Ponda Issa Ponda kwa madai ya kukichafua chama hicho na kuhatarisha amani.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Idara ya Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu aliwaambia waandishi wa habari jana mjini hapa kuwa Ponda anapita misikitini mjini Zanzibar akieneza chuki na kuwachochea wananchi ili wafanye vurugu.

“Katika siku za hivi karibuni tukiwa katika Mfungo wa Ramadhan, mtu anayejiita Sheikh Ponda Issa Ponda kutoka Tanzania Bara ameamua kuweka kambi Zanzibar, akijaribu tena kuasisi ghasia, vurugu na kueneza hasama na chuki miongoni mwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla,”alidai Waride.

Waride alisema Ponda amekuwa akiwakashifu viongozi wakuu wa Serikali, kutaka CCM isichaguliwe na kuwataka wananchi waandamane kama wanavyofanya wenzao wa Misri.

“Ponda anapitapita kwenye baadhi ya Misikiti Zanzibar, akitoa mihadhara na mada zenye taswira ya uchochezi kwa lugha laini ya dini na kufanya siasa, anaishambulia Serikali, chama tawala CCM na kutukana vingozi wa Serikali akilenga kuamsha vurugu na kushawishi maandamano haramu,” alisema Katibu huyo.

Alidai kuwa amepita maeneo ya Nungwi, Kwarara na Muyuni ambako inasemekana wamewataka waumini wafanye uasi, vya kulipiza visasi na kutangaza Jihad ambayo ni vita vya kidini.

Alitaka vyombo vya Serikali vimkamate na kumchukulia hatua Ponda kwa madai kuwa anahatarisha amani ya Zanzibar wakati akiwa katika kifungo cha nje alichopewa na mahakama hivi karibuni katika kesi ya kuvamia eneo huko Chang’ombe , Dar es Salaam.SOURCE MWANANCHI
 
Chama kimezeeka hata hakijui kama kinasubiri kufa kizikwe bado kinafikiri kitawaongoza watanzania zama hizi
 
Ponda aleta hofu Zanzibar
• Polisi wamsaka, wamtaka ajisalimishe

na Hassan Ali Ame, Zanzibar



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) visiwani Zanzibar kimemtuhumu Mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, kuwa anaendesha kampeni za uchochezi wa kidini.
Uchochezi huo umedaiwa kuhatarisha amani ya nchi, hivyo kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumchukulia hatua za kisheria.
Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu (NEC) Zanzibar, Itikadi na Uenezi, Waride Bakari Jabu, alisema jana kuwa ni wiki moja sasa tangu Ponda afanye mihadhara kwenye misikiti ya Mbuyuni, Kwarara na Nungwi kisiwani Unguja.
Waride alisema kuwa hotuba za Sheikh Ponda alizozitoa kwa nyakati tofauti kwenye misikiti hiyo zinapandikiza mbegu ya chuki, kuondosha upendo na kuhatarisha amani.
Alisema matamshi yake ni hatarishi kwa amani na utulivu uliopo, kwani anawataka Waislamu kupigana vita ya dini (Jihad) na kushiriki harakati za kuikomboa Zanzibar, kwa madai kuwa serikali iliyoko madarakani inawakandamiza na kuwanyanyasa wananchi.
“Sheikh Ponda ni hatari, anapanda shari na chuki miongoni mwa wananchi, anahamasisha wananchi wafanye uasi, kulipiza visiasi na kutaka waingie barabarani kwa maanadano ya kutetea haki kama inavyotokea Misri,” alisema.
Aidha, alisema CCM imeshangazwa na ukimya wa vyombo vya ulinzi na usalama wa raia kumtazama kiongozi huyo bila ya kumchukulia hatua za kisheria wakati akiwatukana matusi ya nguoni viongozi wa serikali na chama tawala.
Aliongeza kuwa Sheikh Ponda huenda anatumiwa na mtandao wa vurugu ili kuharibu na kuvuruga amani ambapo hamu yake ni kuona damu ya wananchi ikimwagika na nchi ikiingia kwenye machafuko.
Kwa mujibu wa Waride, kitendo cha Ponda kulitumia jukwaa la dini na kufanya siasa misikitini hakikubaliki na kwamba kikiachiwa kiendelee kinaweza kuleta madhara na mgawanyiko.
Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alisema jeshi hilo limeanza kumtafuta Sheikh Ponda tangu walipopokea taarifa za kuendesha mihadhara ya uchochezi katika baadhi ya misikiti, ikiwa na lengo la kuibua chuki.
Mussa alisema kitendo anachokifanya kinakwenda kinyume cha sheria, hivyo kumtaka popote alipo ajisalimishe kwa hiari yake.
Tangu kuingia visiwani Zanzibar, Sheikh Ponda amekuwa akifungamana na viongozi wa Jumuiya ya Uamsho wakipinga kitendo cha viongozi wa jumuiya hiyo kuendelea kubakia mahabusu baada ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uharibifu wa mali na kuhatarisha usalama wa taifa.
Viongozi hao wa Uamsho wako mahabusu baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, kuwasilisha ombi la kufunga dhamana yao kwa kutumia sheria ya Usalama wa Taifa na marekebisho yake ya mwaka 2002.


 
Panya bado wanajadili nani mwenye ubavu wa kwenda kumfunga paka kengele?Hadi madhara yakitokea ndipo tutasikia matamko ya kulaani na kutishia hatua kali za kisheria,utadhani sheria hizo bado zinatungwa, kumbe zipo ila waoga tu wa kuzitumia.Baada ya kusema hayo:Mwacheni Sheikh Ponda ajinafasi tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom