Well done Ponda! Polisi na CCM ni sawa Kopo na Mfuniko.!! Ingekuwa ni Shekhe mkuu wa Bakwata Tanzania (taasisiya Ccm) ndio amezungumza kukosoa CUF au CDM,tusingesikia ikisemekana akamatwe kwa kuchochoea uasi. Lakini kwa kuwa Shekhe Ponda anawananga CCM chama ambacho ndio Adui mkubwa wa Watanzania basi lazima ataitwa mchochezi.
Mwigulu Nchemba ni mara mangapi amezungumza maneno ya Uchochozi na hakuchukuliwa hatua zozote? Kunya anye kuku,akinya Bata ni Kuhara!!
Binafsi namuunga Ponda mkono kuendelea kuwatangazia Watanzania ubaya wa CCM.
Waliposimama viongozi wa Dini na kumtaja kiongozi wa mmoja sasa wa CCM kuwa ni Chaguo la Mungu mbona hatukusikia CCM wakipinga,ila leo akisimama kiongozi wa Dini km yule mwingine na kuikosoa CCM ndio tunaambiwa ni mchochezi au anataka watu Waasi!? Ama kweli ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huwezi!! Shame on CCM!