Sheikh Mazinge ukiona mtu mwanasiasa anamtukana Rais Samia basi ujue kachanganyikiwa

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,365
12,823
Friends and Enemies...

Sheikh Machachari wa minakasha na makongamano nayeye amevunja ukimya DHIDI ya wanasiasa na wale ambao wamekuwa vinara wa kauli chafu na matusi DHIDI ya Rais Samia.

Sheikh MAZINGE ameendelea kusema kwamba wengine ndani ya nchi hii walikuwa wakimbizi wakaihama nchi pasipo kupenda.

Kuna wengine walishambuliwa na risasi na kuachiwa ulemavu wa Maisha,yeye akawa wa Kwanza mwenye ujasiri wa kukimbia kwenda kumjulia Hali,kumfariji,kumuombea na kumtia moyo.

Kuna wengine walifungiwa akaunt zao za bank Kwa dhulma,lakini Samia kaja na kuzifungulia.

Kuna wengine walikuwa jela miaka mingi Kwa kesi zingine za uzushi lakini Samia kawafungulia.

Uhuru wa kuongea na WA kufanya siasa za mikusanyiko Kwa uhuru halikuwepo,Leo wanaona Hana maana.

Ameendelea kusema kwamba Haki ya kukosoa na siasa ni ya Kila Mtanzania ila inakuaje mtu aache kujenga hoja akimbilie kwenye kashfa na matusi?hiyo ni ishara tosha ya kukosa hoja na kujiamini.

My take: Nampongeza sana sheikh MAZINGE kwa maneno yake ya uzalendo Kwa nchi,hakika Rais Samia ni chaguo la Mungu na kazi yetu kubwa iliyobakia kwetu sisi ni kumuombea Kila aina ya Dua ili mahasidi,wazandiki na wachawi wakae nae mbali.
 
Ye ana uhakika gani kama walisingiwa?? Kwani nani asiyejua huyo mama alipindua meza ili aonekane ye mwema?
 
Kwamba ndo tiketi ya kufanya Mkataba mbovu na waarabu ?

Mazinge kashambulia mtoa hoja, anapaswa atetee hoja.

Bambaf
 
Mazinge hana hata moja analojua...kipindi kile watu wanauliwa lilikuwa kimyaaa. Bandari inauzwa linachomoa ndimi zake hovyo kbs hili shekhe.
 
Back
Top Bottom