Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.
Daraja LA balozi mwivi!!!!!

Ni afadhali huyu, pamoja na wizi wake wote aliofanya hadi kufikia " KUINUNUA NEWCASTEL YA UK kama mnavyozua" lakini japo kidogo alijificha kwa kufanya mazuri na miongoni mwa hayo mazuri ni hilo "DARAJA LA BALOZI MWIVI, MAJENGO YA PPF NA NSSF"

Tuje kwa wasomi wa kikristo aka hela ya MBOGA na VIJISENTI waliyofanya ni haya: kununua RADA MBOVU, NDEGE YA RAISI MBOVU tena kwa gharama za kuwalisha watanzania majani, kuuza dhabu kwa $3, kununua Meli MBOVU, kujiuzia nyumba za Serikali kwa BURE kugawana hela ya escrow hadi viongozi wao wa imani nao wakawagawia n. k
 
Watu wasome na kisha waonyeshe uwezo kazini watapata vyeo...rais hachagui watu kwenda kufanya kazi ya dini bali ni kufanya kazi ya serekali full stop
 
Watu wasome na kisha waonyeshe uwezo kazini watapata vyeo...rais hachagui watu kwenda kufanya kazi ya dini bali ni kufanya kazi ya serekali full stop
Elewa ulivyoelewa, hizo siasa za maji taka hazitusumbui.
 
Ni afadhali huyu, pamoja na wizi wake wote aliofanya hadi kufikia " KUINUNUA NEWCASTEL YA UK kama mnavyozua" lakini japo kidogo alijificha kwa kufanya mazuri na miongoni mwa hayo mazuri ni hilo "DARAJA LA BALOZI MWIVI, MAJENGO YA PPF NA NSSF"

Tuje kwa wasomi wa kikristo aka hela ya MBOGA na VIJISENTI waliyofanya ni haya: kununua RADA MBOVU, NDEGE YA RAISI MBOVU tena kwa gharama za kuwalisha watanzania majani, kuuza dhabu kwa $3, kununua Meli MBOVU, kujiuzia nyumba za Serikali kwa BURE kugawana hela ya escrow hadi viongozi wao wa imani nao wakawagawia n. k
Vyote meli,rada,ndge na daraja vinaonekana ila sasa gharama zake zinatofautiana,dau kapiga ndefu na kaacha Nssf hoi
 
Mgen,
Wanaonifahamu ni hawa wafuatao:
Oxford University Press Nairobi na New York wamenishirikisha katika miradi na kuchapa kazi zangu. Mradi wa kusomesha Kiingereza Afrika ya Mashariki na Dictionary of African Biography.

Wanaonifahamu ni University of Ibadan, Kenyatta University, University of Iowa, Northwestern University, Zentrum Moderner Orient (Berlin), University of Johannesburg. Hawa ni katika mikutano natoa paper na kwengine kama visiting scholar.

Tusimame hapa kwanza na ukitaka tutaendelea kufahamishans.
wapi ndani ya ilimu isilamu hao ndio rejea yako, badala ya qaraa, hadith na miratul rasul [emoji47] [emoji15]
 
Andiko refu herufi kubwa zote zina bore. Herufi kubwa zina maana yake jamani ka! Ni sawa na unapigia mstati kila neno.
 
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.

Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.

Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.
Mbona wapagani hawalalamiki? Kwa nini waislam wanapenda kuwaza dini kwenye kila jambo? Kwani wanataka sawa kwa sawa kwani tuko sawa? Kwa idadi ya wasomi na population in general? mwenzenu alijaribu tu kuwabeba mkajisahau hamkubebeka mkadhani nchi ya kwenu mpaka mabomu mkatupiga.
 
Huyu shekhe anahitaji kupewa ushauri nasaha kwa upole. Lakini, niseme tu kwamba, manung'uniko yake ni kama ya kina Hellen Kijo Bisimba kuhusu ubaguzi wa kijinsia katika teuzi za JPM. Kina Hellen wanataka nafasi za uteuzi zigawiwe pasu kwa pasu kati ya wanawake na wanaume. Sasa shekhe anataka nafasi zigawiwe kwa kuzingatia uwiano fulani kati ya makundi mbalimbali ya kidini na kikanda. Naona auanongelea Ukristo dhidi ya Uislam, Umashariki dhidi ya Umagharibi. Amesahau kuongelea ujana dhidi ya uzee, Ukulima dhidi ya Ufanyabiashara, Usomi dhidi ya Kutosoma, na migawanyiko kama hiyo.

Yeye pamoja na kina Bisimba ni watu wa kuelimishwa hivi: Vyeo havigawiwi kwa kuangalia vigezo vinavyohusiana na migawanyiko ambayo haina tija katika ofisi. Kwa mfano, mwalimu wa hesanu anaweza kuwa mwanamke au mwanamume, mkristo au muislamu, mmashariki au mmagharibu, kijana au mzee. Lakini hawezi kuwa mkulima wala mfanya biashara kama ambavyo hawezi kuwa asiye na kisomo. Vigezo vya ujuzi, ustadi, uzoefu na utayari vinahusika. Hivi hoja hii ni ngumu?

Kuna performance indicators in good governance wanatuletea hawa development partners kama vile gender equity, denominational equity, geographical equity, inter generational equity, n.k. Haya mambo tuyakatae kwa hoja kwa kuwa hayana tija. Tukikubali kila kitu tutakuwa kama madodoki.
So maana yake unataka kusema wanawake hawatakiwi kuteuliwa kwakuwa sio viongozi wazuri sio? Acha hizo hapa juzi tu Dr. DAU WA NSSF alipigwa vita mitandaoni kuwa ni mdini na anawapendela waislam kwenye ajira leo rais anafanya hivyo kwenye teuzi zake... Kinaonekana kitu cha kawaida?
 
[emoji814] Daah...HUWA NAJIULIZA HILI:

■ Awamu iliyopita,

[emoji666]RAIS= Muislam.

[emoji666]MAKAMU WA RAIS= Muislam

[emoji666]RAIS WA ZANZIBAR = Muislam

■ Awamu hii

[emoji666]RAIS= Mkristo

[emoji666]MAKAMU WA RAIS = Muislam

[emoji666]WAZIRI MKUU= Muislam

[emoji666] JAJI MKUU= Muislam

[emoji666] RAIS WA ZANZIBAR= Muislam

Sijui kama ingekuwa ni wakristo wameshikilia nafasi hizo ingekuaje kama sasahv lawama haziishi.

- Hata kwenye all 3 National pillars wangekuwa waislam wote bado kuna watu wangelaumu tu.
Mbona waziri mkuu haukumuweka kama alikuwa mkristo na jaji mkuu haukujua kuwa tangu inaze tanzania yeye ndio jaji mkuu wa kwanza mkristo hauoni hilo bora jeshi la polisi wao wanabadilishana ma IGP kulingana na dini na uwezo wao.... Tafakari kijana ishu ya udini , ukabila, na jinsia ni kubwa sana na siku zote serikali lazima izingatie haya ili kuleta sura ya kinchii
 
Mimi siamin kuwa mungu yuko makah

Kama askofu wako ndivyo anavyokuongopea kakosea sana

Mungu wangu mimi yupo kila mahala mimi nilipo na halali wala hapitiwi na usingiz

Makah ni mji mtakatifu ambao mtume wangu kazikwa hapo...kwenda kuhijj ni ibada maalum ambayo natakiwa kuifanya na siyo kwa kigezo kua namfuata mungu wangu huko

Mungu wangu mimi si dhaifu kama wa kwako alikadundwa na kusulubiwa akiwa uchi wa mnyama

Wewe tokea lin mungu akapewa kichapo
Asante mkuu... makkah ni mji ambapo mtume Muhammad amezaliwa.. sahihisho
 
wapi ndani ya ilimu isilamu hao ndio rejea yako, badala ya qaraa, hadith na miratul rasul [emoji47] [emoji15]
Mgen,
Nilijua hutofika mbali na mie.
Kawaida ya watu mfano wa wewe huwa wanaanza na dharau.

Kinachofuatia kwao ni kupigwa na mshtuko mkubwa.
Wewe si wa kwanza.

Umeshtuka kusoma kuwa nimefanyakazi na Oxford na Harvard
kusomesha Kiingereza na kuandika historia ya Afrika.

Baada ya kutulia sasa unakuja na maskhara.
Si ''qaara,'' ni ''kala.''

Si ''miratul,'' ni ''milatul.''

Ndiyo maana mwenzako nikajua Kiingereza kwani Kiarabu kimenisaidia
sana katika matamshi.

Je, nikuongeze vitu vingine nikudhihirishie pasi shaka kuwa mie nafahamika
kwingi?

YJIWLvi1aadzVCAC6pGV1vqkS3ww7Gz044Lu4rzcDmqrrNc3zS22beQP1NPVXyopqVScsfMGADvui8-h9uXmyTlaRQ6ZAwh2OzTi1lTsm4CVa_0l6sHhw0gvh2GqTgww1RtlFMLCZTEO517j6YfP8olcWJO1IqS9A6u5UkpUlGOvalSIejFCExffjpPym5Rz5uGzYg1GiO5Iq7Cix8EfUkFIgFGL_Xgs0L241UwmveQ5QMziXpulXSGsDytKJNlV8pe4QhhCU0p59p1uW2qoy_Uf6i4SbAvrztSDww9ZzplXKK_dS2QHL7IPXf6pJd1c3x8PVbK30B9kGGmzOVMavb0alj7fv9ImOoLZG5vUSzWZlQeUZOuimi2dZVCg_WGRRvQptxT_8Wjhi9DXhQFpXkKooskUHSZ_BIbIzcyN_C-rlV8rDKNQmHy4wiypS1-cAyS93naoXu5ShBmi4-SdNXr869dcTkIz5pLmoy8YCJzYLg0fRF-4dy17LgwcnIgVzZto4TLYAI6prO-X_fArkoXTr9YoxpsuRY-q8H3gWZ6-CQVB1B7gUj2YB48lopahE4-LQkOHv2huP1GqLCQIF-HubiA3_DLPLvu-U35wyaRSw8qD=w505-h581-no

VOA Washington, DC
 
Mbona wapagani hawalalamiki? Kwa nini waislam wanapenda kuwaza dini kwenye kila jambo? Kwani wanataka sawa kwa sawa kwani tuko sawa? Kwa idadi ya wasomi na population in general? mwenzenu alijaribu tu kuwabeba mkajisahau hamkubebeka mkadhani nchi ya kwenu mpaka mabomu mkatupiga.
Bugzbunny,
Imekuwa kawaida kuletwa ''bogey'' la Wpagani kila pale Waislam
wanapodai haki zao.

Mimi nimetafiti historia ya Tanganyika kwa karne nzima iliyopita
katika siasaza Waafrika.

Sikuwaona Wapagani popote katika Vita ya Maji Maji 1905 - 1907.

Sikuwawaona Wapagani katika harakati za kuasisi African Association
1929.

Sikuwaona Wapagani katika kuanzisha vuguvugu la kudai uhuru wa
Tanganyika na kuasisi TANU 1954.

Nimekuja kuwasikia Wapagani baada ya uhuru ati ipo na hii dini hii ya
Wapagani nayo inahaki sawa na Waislamu na kusikia at inaweza kudai
haki zao.

Lakini kichekesho cha kustaajabisha hao Wapagani huwaoni popote ni
''bogey.''

Nchi yetu inakabiliwa na tatizo zito sana la udini tusifanye maskhara.
 
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.

Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.

Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.
sasa yeye si ametoa na ushahidi hapo uongo wake uko wapi mi naona kuna ukweli wa asilimia 100 ama wewe bado una mtazamo wa baba wa taifa kwamba hakuna waislam wanao fit kwa nafasi hizo?
 
UDINI awamu hii hasa ule wa kuwatenga waislamu katika nafasi mbalimbali si jambo lililojificha katika awamu hii. Tanzania ni secular state ambapo, nafasi za uteuzi haziangalii dini ya mtu, lakini pale kila teuzi inakuwa ni teuzi kwa watu wa dini moja, maswali yanaibuka kuhusu ukweli wa tamko hili. Udini huvunja uzalendo na utaifa. Sio jambo la kufumbiwa macho. Kwanini mtu mmoja atuharibie nchi yetu? Hii ni nchi yetu sote, haiingiiakilini eti wanaofaa uongozi ni wakristo peke yao
 
Nafasi za uteuzi haziangalii dini ya mtu halafu unataka dini ziangaliwe ili wa dini unayotaka wewe waongezwe kwa idadi unayoiwaza; yaani wewe unataka dini iwe mojawapo ya sifa za uteuzi. Sijui unapinga nini na unataka nini! Mbona wewe ndiye mdini? Wakati anayeteua haangalii dini ya mtu wewe kutwa kucha kuhesabu dini za wateuliwa. Mdini kweli wewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom