Sheikh Hamisi Mataka: Nilivyokoseshwa elimu ya Sekondari

Ralph...
Kama nilovyokueleza hapo mwanzo ikiwa huamini kuwa EAMWS ilivunjwa kwa kuwa ilikuwa na mipango imara ya kuwanyanyua Waislam mimi siwezi kukulazimisha uamini.

Lakini wahusika wakuu wanajua fika ukweli huu.
Utabakia hivyo hivyo huamini kuwa wapo wanaofaidika na hali hii lakini jua kuwa hutoacha kutusikia sisi tukiwakumbusha viongozi wetu kuhusu dhulma hii na wala si nia yetu kuleta farka katika jamii.

Allah katufunza Waislam kwa onyo kali akitueleza: "Msidhulumu wala msikubali kudhulumiwa."

Historia ya wazee wetu katika kupigania uhuru wa nchi yetu na kuleta haki na kujenga umoja mimi ndiyo niliyoiandika kwa huu mkono wangu unaoandika hapa tena nikiwa kijana wa miaka 30.

Historia hii kwa hofu tu ilifutwa lakini nimeirejesha na kitabu kinakwenda toleo la tano katika miaka 20.

Hakuna yeyote aliyesimama kusema mimi nimesema uongo.

Mimi kwa mkono huu ndiye niliyeweza ku-document historia nzima ya Baba wa Taifa toka siku ya kwanza anatia mguu wake anavuka kizingiti cha nyumba ya marehemu Abdulwahid Sykes nikaeleza yote na vipi alijulishwa kwa Sheikh Hassan bin Ameir na mipango yote iliyopita kote akitembezwa nchi nzima akifikia nyumba za Waislam hadi uhuru ukapatikana mwaka 1961.

Haiyumkiniki mimi kizazi cha wazalendo hawa niwe na haja ya kufarikisha.

Mkono huu ndiyo ulioandika pia kwa masikitiko makubwa yote yaliyotokea baada ya uhuru ya kuandikwa kwa historia ya TANU mwaka 1981 na kwa hofu na khiyana historia hii ikafutwa.

Vipi nikulazimishe uamini haya yote?

Lakini mimi hawa waliounda TANU na kupigania uhuru wa nvhi yetu ni wazee wangu na wengi nimewaona kwa macho yangu na wengine wameniona nikiwa mtoto na kuwajua wazazi wangu.

Hakika mimi na wewe hatuwezi kuwa sawa katika uelewa wa historia hii.
Sheikh wangu,
Sina uhakika kama nimefanikiwa kukuonesha tunachotofautiana katika huu mjadala. Ngoja nijitahidi kueleza kwa kifupi.
Nakubaliana na wewe kiasi kikubwa kwa mambo makuu mawili:
  1. Historical facts unazotoa. Nyingi hazina ubishi, na hakika tunaelimika kusoma kuhusu hayo matukio mbalimbali uliyoeleza katika kitabu chako (nimekisoma chote) yaliyotokea wakati wa harakati za uhuru, na za wahusika wake. Kama mtu alishiriki harakati fulani, hiyo ni fact, haiwezi kubadilishwa ikasemwa hakushiriki. Kama mtu alitoa mchango fulani, haiwezekani kukanusha na kudai hakutoa, hata kama ikikanushwa ukweli haubadiliki ukawa uwongo kwa kuwa kuna watu wamekanusha.
  2. Vyanzo unavyotumia na kuhakiki taarifa zako vipo, na ni traceable, hata mwingine akifuatilia atahakiki.
Ninatofautiana nawe mambo kadhaa lakini hapa nataja moja kuu: ingawa unaeleza matukio ya kweli, unayapa maelezo ama sababu zisizothibitishwa ukweli wake, na hiki ndicho chanzo cha farka.

Nikupe mfano kwa kunukuu sehemu ya sentensi yako ya kwanza hapo juu. Umesema "..........EAMWS ilivunjwa kwa kuwa ilikuwa na mipango imara ya kuwanyanyua Waislam......." Sentensi hii ina tunachokubaliana na tunachotofautiana.

EAMWS ilivunjwa (hii ni fact, tunakubaliana) kwa kuwa ilikuwa na mipango imara ya kuwanyanyua waislam (hapa tunatofautiana. Ushahidi wa hili uko wapi?) Hao waliovunja hiyo taasisi walitoa sababu gani, na je hizo sababu zina ukweli au uongo gani? (kwa ushahidi). Je taasisi nyingine zilizokuwa zinawanyanyua waislamu nazo zilivunjwa, au hazikuwepo? Waislamu walikatazwa au kuzuiwa kuunda taasisi nyingine yenye malengo yaleyale ya kuwanyanyua waislamu?

Hiyo conclusion ya kuhusu sababu ya kuvunjwa kwa taasisi hiyo huna data za kuithibitisha.

Kwa hakika nakusifu kwa uandishi mzuri wa kiswahili na kiingereza, na nimekusikia ukizungumza lugha zote mbili kwa umahiri kabisa. Simulizi zako kuhusu yaliyotokea na yalivyotokea hazipingwi kwa kuwa kwa kiasi kikubwa ni za kweli. Kwenye zile za "What happened, when, where, by who and how" uko vizuri. Tatizo liko kwenye "why", hapo ndipo unapotuingiza chaka mzee wangu.
 
Sheikh wangu,
Sina uhakika kama nimefanikiwa kukuonesha tunachotofautiana katika huu mjadala. Ngoja nijitahidi kueleza kwa kifupi.
Nakubaliana na wewe kiasi kikubwa kwa mambo makuu mawili:
  1. Historical facts unazotoa. Nyingi hazina ubishi, na hakika tunaelimika kusoma kuhusu hayo matukio mbalimbali uliyoeleza katika kitabu chako (nimekisoma chote) yaliyotokea wakati wa harakati za uhuru, na za wahusika wake. Kama mtu alishiriki harakati fulani, hiyo ni fact, haiwezi kubadilishwa ikasemwa hakushiriki. Kama mtu alitoa mchango fulani, haiwezekani kukanusha na kudai hakutoa, hata kama ikikanushwa ukweli haubadiliki ukawa uwongo kwa kuwa kuna watu wamekanusha.
  2. Vyanzo unavyotumia na kuhakiki taarifa zako vipo, na ni traceable, hata mwingine akifuatilia atahakiki.
Ninatofautiana nawe mambo kadhaa lakini hapa nataja moja kuu: ingawa unaeleza matukio ya kweli, unayapa maelezo ama sababu zisizothibitishwa ukweli wake, na hiki ndicho chanzo cha farka.

Nikupe mfano kwa kunukuu sehemu ya sentensi yako ya kwanza hapo juu. Umesema "..........EAMWS ilivunjwa kwa kuwa ilikuwa na mipango imara ya kuwanyanyua Waislam......." Sentensi hii ina tunachokubaliana na tunachotofautiana.

EAMWS ilivunjwa (hii ni fact, tunakubaliana) kwa kuwa ilikuwa na mipango imara ya kuwanyanyua waislam (hapa tunatofautiana. Ushahidi wa hili uko wapi?) Hao waliovunja hiyo taasisi walitoa sababu gani, na je hizo sababu zina ukweli au uongo gani? (kwa ushahidi). Je taasisi nyingine zilizokuwa zinawanyanyua waislamu nazo zilivunjwa, au hazikuwepo? Waislamu walikatazwa au kuzuiwa kuunda taasisi nyingine yenye malengo yaleyale ya kuwanyanyua waislamu?

Hiyo conclusion ya kuhusu sababu ya kuvunjwa kwa taasisi hiyo huna data za kuithibitisha.

Kwa hakika nakusifu kwa uandishi mzuri wa kiswahili na kiingereza, na nimekusikia ukizungumza lugha zote mbili kwa umahiri kabisa. Simulizi zako kuhusu yaliyotokea na yalivyotokea hazipingwi kwa kuwa kwa kiasi kikubwa ni za kweli. Kwenye zile za "What happened, when, where, by who and how" uko vizuri. Tatizo liko kwenye "why", hapo ndipo unapotuingiza chaka mzee wangu.
Ralph...
Mimi kutoa ushahidi wa aina ya mahakama sitaweza nitabaki kwenye utafiti tu
ambao wewe huukubali.

Ila nimeshukuru kuwa umetimia neno, ''shaka.''
Shaka inaweza ikawa kweli au vinginevyo.

Hapa ndipo penye uzuri wa shaka.

Yapo mengine siwezi kuandika hapa lakini ikiwa In Shaa Allah itatokea siku mimi
na wewe tukakutana uso kwa macho nitakueleza na wala si nia yangu ukubali kuwa
nasema kweli, la hasha nia ni kutaka ujue kuwa hili nalo limesemwa hata kama wewe
hutaamini.

Upo ushahidi wa Rashid Kayugwa nimemweleza kwa undani katika kitabu na pia
uko ushahidi wa Geoffrey Sawaya na yeye nimemweleza katika kitabu cha Abdul
Sykes.


Lakini upo ushahidi wa Sivalon ambao ni maarufu.

Upo pia ushahidi wa Bergen ambao baada ya kuonekana aliyoandika ni maneno mazito
Cathedral Bookshop ambao ndiyo walikuwa wasambazaji wa kitabu hicho hawakiagizi
tena.

Naamini kuwa unazo taarifa pia kuwa mchapaji wa wa Sivalon Ndanda na wao pia kitabu
hiki wamekizuia na hizo nakala unazoona zinauzwa nje ya misikiti ni vijana wajasiriamali
wanachapa kwa njia zao wenyewe kujitafutia riziki.

Ushahidi wa Njozi haukuweza kuwafikia wananchi kwa kuwa kitabu kilipigwa marufuku.
Ukikutwa na kitabu hicho ni kosa la jinai.

Ralph,
Nakushukuru sana kwa uungwana wako na kwa hakika unakisukuma kichwa changu
kufikiri tofauti na wenzangumie humu ambao huishia kunitukana.

Napenda kumaliza kwa kukueleza kitu.

Marehemu Prof. Haroub Othman aliumizwa sana na kitabu changu na cha Ali Muhsin
Barwani
kiasi alimkabili Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akamuomba atoe
majibu ya yale tuliyoandika kuhusu historia ya nchi yetu ili ukweli ujulikane.

Prof. Haroub alitaka Baba wa Taifa athibitishe au akane yale yaliyoandikwa.
Kwake huo ndiyo ungekuwa ukweli lakini hakuweza kutuamini sisi wawili.

Huwa sishangai watu wanaponikanusha.
 
Huo ndio uhalisia, lengo ni kukatisha tamaa lakini kwakua hakuweza kukata tamaa, alipambana mpaka damu ya mwisho kuona aalichokitarget kinafanikiwa....
Kwahiyo huko mbele alikoendelea alisomea madrasa au kwa wale wale unaosema walikuwa na lengo la kumkatisha tamaa? AU huko juu alikutana na waislamu wenzie?
 
MAENDELEO NI PAMOJA NA KUBADILI MTIZAMO.
Ndugu zanguni,
Nimesoma huko nyuma post zilizojaa kejeli na kebehi hata baada ya mimi
na Ralph kufanya mjadala ambao kwangu mimi naona una mengi ya msingi
katika kulielewe tatizo linalokabili nchi yetu kwa miaka mingi.

Naamini huenda tatizo ni kuwa wengi hawajui historia ya hii nchi yetu wapi
tulikotoka na hali ilikuwaje.

Nakuombeni ndugu zangu muingie hapo chini na chukueni muda hapo kwani
kipo cha kujifunza.

Hii ni simulizi ya mkasa wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ilipodhaniwa
kalishwa chakula kilichotiwa sumu kwa nia ya kutaka kukatisha maisha yake nyumbani kwa Abdulwahid Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu katika miaka ya kati 1950 baada ya Mwalimu kutoka UNO safari ya kwanza 1955.
Mohamed Said: WOMEN LEADERSHIP SUMMIT 2018 MLIMANI CITY 27 FEBRUARY 2018
 
Ndugu yangu, kwanza nIMPONGEZE Shehe kwa JUHUDI zake katika Ilmu. Napenda pia kuwashirikisha wana Jamvi kuwa MTAZAMO kuwa ELIMU ya DARASANI NDIO Ukombozi PEKEE wa Mwanadamu, SIYO kweli kabisa (Ushahidi ni kazi alofanya Shehe kule Ubalozini haikuhitaji ELIMU ya CHETI alopata darasani). Hapa, kwa maoni yangu, HAPASWI kulaumu nafasi yake ya kwenda Sekondari na Kuona kuwa ni hasara kupangwa kusomea Ufundi......Aweke JUHUDI. Ikibidi AYAALIZE MMadarasa YOTE kwa Kujipatia Shahada ya UZAMIVU katika eneo analopenda zaidi.... Elimu HAINA MWISHO!
 
Chochote tunachokijenga kwenye misingi ya uongo kitalaaniwa. Kamwe hakiwezi kusimama
 

Sheikh Hamisi Mataka

Shule ya Msingi Mchikichini sikupata kushika zaidi ya nafasi tatu za juu muda wote wa miaka saba hapo shuleni. Kwa kuwa nilianza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 11 ule moja wa miaka mine ambayo ningekuwa shule ya msingi iliniwezesha kumiliki chuo changu mwenyewe yaani madrasa, nikiwa mwalimu mkuu katika umri mdogo wa miaka 15.

Nilipoanza shule darasa la kwanza katika huo umri wa miaka 11 ambao ni mkubwa kwa kuanza darasa la kwanza pale Shule ya Mchikichini nilikuwa pia mwalimu wa dini kwa wenzangu.

Kwa ajili ya makuzi yangu ya Kiislam nilikuwa nikilitoka eneo la shule tu nilivaa kanzu yangu juu ya sare kwa kuwa sikujisikia kuvaa kaptula mitaani kwani uchi wa mwanmme unaanza juu ya magoti yake.

Mwalimu wangu wa Historia Mzee Kasunsumo alipata kuniambia: '’Sheikh Khamis, pamoja na uwezo wako wa kielimu hutochaguliwa kwenda sekondari na kinachokuponza ni huu ualimu wako wa Dini ya Kiislamu.'’

Hakika na kweli ikawa hivyo badala ya kuchaguliwa kwenda sekondari nikapelekwa Chuo Cha Ufundi Chang'ombe kusomea Usukaji Mota. Uhodari wangu wa masomo na tabia yangu nzuri hazikutazamwa. Kilichoangaliwa ni ule Uislam wangu.

Sikukaa sana pale Chuo Cha Ufundi na kwa hakika moyo wangu ulikuwa ukiniuma nikiwaona wale ambao mimi nikiwapita katika masomo wako sekondari wanasoma na mimi nimepelekwa Chuo Cha Ufundi nikiwa muhitimu wa darasa la saba. Kilichofuatia ni kuwa nikaacha katikati na kujiunga na Chuo Cha Biashara ambapo nilichukua Basic Book-Keeping Certificate (BBC) na kufanya vizuri sana.

Katika mitihani ya ndani, '’’I was first out of 67 candidates,’’ yaani nilikuwa mwanafunzi wa kwanza nikiongoza katika wanafunzi 67. Huu ndiyo ulikuwa uwezo wangu mimi mwanafunzi niliyotokea shule ya msingi Mchikichini na maalim wa madras mtoto.

Nilipokabidhiwa cheti cha BBC taarifa ya ufaulu ilinizuia kuendelea na NABOCE kwa ibara hii: '’If you are Standard Seven you will be eligible to sit for NABOCE Exams after you have completed formal Form Four Education.’’ Bahati mbaya ilikuwa inazidi kuniandama.

Wakati huo umaskini wa familia ulinilazimisha kufanya kazi za kutafuta riziki halali mbali ya kuendelea kufundisha dini katika chuo change. Baba yangu Sheikh Saidi Mnuta Mataka akinilazimisha kuoa mapema ili amuone mjukuu wa jina lake kabla hajafa.

Nilioa.

Sasa kwa ajili ya kizingiti kile cha kuwa na cheti cha kidato cha nne nililazimika kuitafuta elimu ya sekondari kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (National Correspondence Institute) na nikafaulu QT (NECTA) Mtihani wa Kidato cha Nne na nikaweza kurudi chuoni CBE kuendelea na masomo ya NABOCE huku nikipata ajira ya kudumu ya Mfasiri wa Lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kiswahili katika moja ya balozi nchini.

Laahawla! chuoni sikuikuta tena NABOCE bali mtaala mpya wa ATEC I na II nami nikazisoma kozi husika nikafaulu na nikaweka cheti kibindoni. Lakini ajira mpya ya Ubalozi haikuendana na mambo ya uhasibu nikalazimika kubadili upepo na nikasoma Lugha ya Kiingereza na kufanikiwa kutunukiwa Diploma ya Lugha (Kiingereza).

Muhimu leo nikuandikiapo haya nimeweza kupata vyeti hivi vifuatavyo hapo chini:

1. B.A. (Philosophy, Religious Studies & Kiswahili) - OUT.
2. Post Graduate Diploma (Education) - UDSM.
3. M.A. (Education) - UDSM.
4. Post Graduate Diploma (Management) - IGNOU/UDSM under Pan African E-Network (African Union/Government of India) through Tele-Conference facility.
5. Post Graduate Diploma (Human Resource Management)- IGNOU/UDSM.

Hapa nilipo sasa In Shaa Allah nasubiri MBA (HRM) baada ya kuwasilisha tasnifu yangu juu ya Time Management kupitia utafiti nilioufanya IFM, Dar es Salaam chini ya Dr. Adam Jamal kwa anuani hii: ‘’Managing Time Effectively: A Case of Lecturers in the Higher Learning Institutions.’’

Sasa hivi ni mwanafunzi wa LLB anayefikiria kuja kufanya Comperative Study kati ya Islamic Law na Conventional Law (Common Law and Others).

Kinachofurahisha siku ya Graduation wale walioungaunga elimu na waliounganisha husimama mstari mmoja kutuzwa.

HM
 
Ulalamishi tu.Sasa mbona mlisema Malina alibadilisha watainiwa wakatumia namba lakini bado performance ipo low? Nilisoma kinondoni Muslim high school tulikuwa asilimia 96 wenye shule walikuwa asilimia 4 tu.
 
Nyiokunda,

Tatizo kubwa ni wewe kutojua historia hii ambayo unajitahidi kujadili.

Inaelekea huna taarifa ya mkasa wa Shule ya Kinondoni na Kibohehe zilipofanywa kuwa seminari na kushikwana Warsha na matokeo mazuri yaliyotokea.

Nadhani pia huna taarifa kuwa ilitoka amri kutoka juu kuwa shule hizo zirejeshwe kuwa za kawaida na uongozi ulioleta maendeleo hayo ufukuzwe.

Historia hii nimeieleza hapa si muda mrefu uliopita.

Naingia Maktaba nikipata nitakuwekea.
Ingia:
Mohamed Said: BAKWATA Kibaraka (kipindi maalum)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom