Sheikh Hamisi Mataka: Nilivyokoseshwa elimu ya Sekondari

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,916
30,259

Sheikh Hamisi Mataka

Shule ya Msingi Mchikichini sikupata kushika zaidi ya nafasi tatu za juu muda wote wa miaka saba hapo shuleni. Kwa kuwa nilianza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 11 ule moja wa miaka mine ambayo ningekuwa shule ya msingi iliniwezesha kumiliki chuo changu mwenyewe yaani madrasa, nikiwa mwalimu mkuu katika umri mdogo wa miaka 15.

Nilipoanza shule darasa la kwanza katika huo umri wa miaka 11 ambao ni mkubwa kwa kuanza darasa la kwanza pale Shule ya Mchikichini nilikuwa pia mwalimu wa dini kwa wenzangu.

Kwa ajili ya makuzi yangu ya Kiislam nilikuwa nikilitoka eneo la shule tu nilivaa kanzu yangu juu ya sare kwa kuwa sikujisikia kuvaa kaptula mitaani kwani uchi wa mwanmme unaanza juu ya magoti yake.

Mwalimu wangu wa Historia Mzee Kasunsumo alipata kuniambia: '’Sheikh Khamis, pamoja na uwezo wako wa kielimu hutochaguliwa kwenda sekondari na kinachokuponza ni huu ualimu wako wa Dini ya Kiislamu.'’

Hakika na kweli ikawa hivyo badala ya kuchaguliwa kwenda sekondari nikapelekwa Chuo Cha Ufundi Chang'ombe kusomea Usukaji Mota. Uhodari wangu wa masomo na tabia yangu nzuri hazikutazamwa. Kilichoangaliwa ni ule Uislam wangu.

Sikukaa sana pale Chuo Cha Ufundi na kwa hakika moyo wangu ulikuwa ukiniuma nikiwaona wale ambao mimi nikiwapita katika masomo wako sekondari wanasoma na mimi nimepelekwa Chuo Cha Ufundi nikiwa muhitimu wa darasa la saba. Kilichofuatia ni kuwa nikaacha katikati na kujiunga na Chuo Cha Biashara ambapo nilichukua Basic Book-Keeping Certificate (BBC) na kufanya vizuri sana.

Katika mitihani ya ndani, '’’I was first out of 67 candidates,’’ yaani nilikuwa mwanafunzi wa kwanza nikiongoza katika wanafunzi 67. Huu ndiyo ulikuwa uwezo wangu mimi mwanafunzi niliyotokea shule ya msingi Mchikichini na maalim wa madras mtoto.

Nilipokabidhiwa cheti cha BBC taarifa ya ufaulu ilinizuia kuendelea na NABOCE kwa ibara hii: '’If you are Standard Seven you will be eligible to sit for NABOCE Exams after you have completed formal Form Four Education.’’ Bahati mbaya ilikuwa inazidi kuniandama.

Wakati huo umaskini wa familia ulinilazimisha kufanya kazi za kutafuta riziki halali mbali ya kuendelea kufundisha dini katika chuo change. Baba yangu Sheikh Saidi Mnuta Mataka akinilazimisha kuoa mapema ili amuone mjukuu wa jina lake kabla hajafa.

Nilioa.

Sasa kwa ajili ya kizingiti kile cha kuwa na cheti cha kidato cha nne nililazimika kuitafuta elimu ya sekondari kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (National Correspondence Institute) na nikafaulu QT (NECTA) Mtihani wa Kidato cha Nne na nikaweza kurudi chuoni CBE kuendelea na masomo ya NABOCE huku nikipata ajira ya kudumu ya Mfasiri wa Lugha za Kiarabu, Kiingereza na Kiswahili katika moja ya balozi nchini.

Laahawla! chuoni sikuikuta tena NABOCE bali mtaala mpya wa ATEC I na II nami nikazisoma kozi husika nikafaulu na nikaweka cheti kibindoni. Lakini ajira mpya ya Ubalozi haikuendana na mambo ya uhasibu nikalazimika kubadili upepo na nikasoma Lugha ya Kiingereza na kufanikiwa kutunukiwa Diploma ya Lugha (Kiingereza).

Muhimu leo nikuandikiapo haya nimeweza kupata vyeti hivi vifuatavyo hapo chini:

1. B.A. (Philosophy, Religious Studies & Kiswahili) - OUT.
2. Post Graduate Diploma (Education) - UDSM.
3. M.A. (Education) - UDSM.
4. Post Graduate Diploma (Management) - IGNOU/UDSM under Pan African E-Network (African Union/Government of India) through Tele-Conference facility.
5. Post Graduate Diploma (Human Resource Management)- IGNOU/UDSM.

Hapa nilipo sasa In Shaa Allah nasubiri MBA (HRM) baada ya kuwasilisha tasnifu yangu juu ya Time Management kupitia utafiti nilioufanya IFM, Dar es Salaam chini ya Dr. Adam Jamal kwa anuani hii: ‘’Managing Time Effectively: A Case of Lecturers in the Higher Learning Institutions.’’

Sasa hivi ni mwanafunzi wa LLB anayefikiria kuja kufanya Comperative Study kati ya Islamic Law na Conventional Law (Common Law and Others).

Kinachofurahisha siku ya Graduation wale walioungaunga elimu na waliounganisha husimama mstari mmoja kutuzwa.

HM
 
Shule ya Msingi Mchikichini sikupata kushika zaidi ya nafasi tatu za juu muda wote wa miaka saba hapo shuleni. Kwa kuwa nilianza darasa la kwanza nikiwa na umri wa miaka 11
Astaghfirullah! Ulianza darasa la kwanza ukiwa na umri wa miaka 11 tena jijini Dar es Salaam! Nikiwa na umri wa miaka 11 nilikuwa niko darasa la 6 tena kijijini! Ngoja nikae kimya.
 
Astaghfirullah! Ulianza darasa la kwanza ukiwa na umri wa miaka 11 tena jijini Dar es Salaam! Nikiwa na umri wa miaka 11 nilikuwa niko darasa la 6 tena kijijini! Ngoja nikae kimya.
Mag3,
Sheikh Hamisi Mataka
alianza shule ya msingi akiwa na miaka 11.
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alianza shule ya msingi 1934 akiwa na miaka 12.

Usikae kimya nitafurahi kama ukirejea Majlis na kuzungumza.
 
Kumbe Sheikh Hamisi Mataka naye alikuwa miongoni mwa wale wazee waliopigania uhuru, kunradhi!
 
Unachotala kutuambia hapa ni nini?
UDINI (kuonewa uislamu) kwenye kuchaguliwa kuingia sekondari toka la saba? Maana huko kwingine pamoja na kuwa mwalimu wa DINI na kuwa muislamu bado uliendelea..!!!

Ngaliki...
Mimi siwezi kujibu swali hilo labda tungekuwa na uwezo tungemuuliza
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mchikichini vipi mwanafunzi wake hodari
hakuchaguliwa nini inaweza kuwa sababu?

Au Wizara ya Elimu ingetupa jibu.
 
Basi hukuwa na sababu ya kupost....!!! Maana hujui nia hasa ya post yako....
 
Lengo ni kueleza umma hakuchaguliwa kwa sababu ya uislam?? Vipi kipindi hicho hakuna wanafunz wa kiislam walienda secondary, baraza lilikuwa linajua kuwa yeye ana madrassa?
nakumbuka babu yangu ilibidi abadili jina kutoka athumani hadi joseph ili tu aweze kupangwa shule kwa kipindi hicho nyingi zikimilikiwa na wamisionari,

bila good enough alibadili jina ila imani yake haikutetereka R.I.P babu
 
Unajua haya mambo ukweli ni kwamba islam mliwekeza sana kwenye madrassa na hii elimu ya kawaida mliichukulia kama ya wakristo, nimeishi sana lindi na mtwara naelewa kitu nachozungumza kilwa kisiwani nilikuta shule kubwa ya madrassa wanafunz wanaenda asubuhi wanarud jioni huo mda wa kwenda kusoma physics wanaupata wapi? Kwa hiyo wazee wenu aliinyapapaa elimu dunia na wamisionary waliwekeza kwenye elimu dunia, na hii dhana hadi leo ipo ndio mikoa waliokaa sana waarabu kiwango chao cha elimu ni kidogo
 
Sizo,
Mbona hilo usemalo halina uhusiano na kisa cha Sheikh Mataka?
 
Ngaliki...
Mimi siwezi kujibu swali hilo labda tungekuwa na uwezo tungemuuliza
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mchikichini vipi mwanafunzi wake hodari
hakuchaguliwa nini inaweza kuwa sababu?

Au Wizara ya Elimu ingetupa jibu.
Mzee wangu sioni ajabu mwanzfunzi kutokuchaguliwa japo alikuwa anaongoza darasani.
Siku hazifanani na huwezi kufanya vizuri kila siku.
Je hata alifanya vibaya siku ya mtihani wa mwisho achaguliwe?
Binafsi nimeona wanafunzi wengi walioongoza kuanzia la kwanza hadi la 7 hawakuchaguliwa bali ambao walifanya vizuri wastani wakachaguliwa mtihani wa mwisho.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom