Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,925
- 30,274
- Thread starter
- #121
Ralph...Hiyo hatua iliyochukuliwa dhidi ya huyo Municipal Education officer ni sahihi, na inapaswa wengine wote waliobainika kutenda mambo yanayoashiria ubaguzi wachukuliwe hatua. Mimi bado naona kuwa mengi ya matendo haya yalifanywa kwa utashi binafsi wa mtendaji, sio kwa kufuata maelekezo ya taasisi au mfumo wowote rasmi, hivyo ni bora kila case ikashughulikiwa binafsi. Na zikishashughulikiwa nyingi hivyo, hata mwingine anayetaka kufanya hivyo atasita.
Hili nalichukulia kama ubaguzi ninaouona nchi za Marekani na Ulaya dhidi ya watu weusi na wasiokuwa wazungu. Sera iko wazi kuwa ubaguzi ni kinyume cha sheria, lakini bado wapo wanaobagua hadi leo. Na dhambi nyingine zote ni hivyohivyo.
Rais Benjamin Mkapa alipoelezwa matatizo haya katika risala rasmi aliyosomewa
na viongozi wa Waislam alitoa majibu kama hayo yako na akaomba ushahidi wa
kisayansi.
Ushahidi wa kisayansi ukatayarishwa katika njia ya kitabu ili uwafikie watu wengu
zaidi.
Kitabu kilizuiwa uwanja wa ndege na baada ya kama siku mbili tatu hivi serikali ikatoa
tamko kuwa kitabu hicho kimepigwa marufuku hakiruhusiwi kuingia nchini.
Huo ndiyo ukawa mwisho wa ushahidi wa hiyo dhulma ambayo iliombwa upatikane
ushahidi wa kisayansi.
Toafauti yangu mimi na wewe ni kuwa sisi ni watendewa na tumekivaa kiatu kwa hiyo
tunajua upande gani kinabana.