Sheikh Farid: Tunashukuru tumeachiwa ni mwanzo mwema wa Rais Mwinyi na Samia

Sheikh Farid: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, kiufupi tunashukuru sisi tumeachiwa lakini huu ni mwanzo mwema ya busara ya marais wetu, Rais wa Zanzibar na Rais wa Tanzania, Amiri Jeshi mkuu, mama Samia Suluhu. Wamefanya busara kubwa sana kuondoa hii hali ya mtanziko ya muda mrefu sana wa hii Kesi.

Sheikh Mselem: Tumechukuliwa Gerezani jana Usiku, Maghrib na Insha tumeswali palepale gerezani, tumechanganywa na baada ya kuswali Maghribi tumetoka zetu tukaja Airport.

Airport tumeingia kwenye ndege ilikuwa iko faragha, tumefika zetu hapa tumefikia VIP ya zamani, ndege imekaa peke yake, hakuna mtu zaidi ya wenyewe na tulivyotoka pale kila mtu akaingia kwenye gari lake, akaulizwa nikupeleke wapi?

Mzee Mselem nikupeleke kwa mke wa kwanza, wa pili, wa tatu? Nikawaambia kwanza naenda kwetu, muda mrefu sijafika, nikayasome matatizo, ya kutatua nitatue na mengine alafu ndio nitaanza tena kwenda.

Hatukupewa waraka wowote.


Ni wakati wa kuanza kufunguwa kesi ya madai dhidi ya Serikali zote mbili.
 
Hivi kweli kama wanahusika na jinai hizo serikali ilishindwa kuwafungulia mashtaka wahukumiwe? Mbona walishikiliwa gerezani kwa tuhuma za ugaidi?

Bila shaka serikali ilitunga tuhuma za uongo na hata tuhuma za kuwamwagia watu tindikali ilifanywa na ma-agent wa serikali wasiojulikana! Mambo mengi mabaya yamefanywa na serikali nyuma ya mgongo wa wasiojulikana!


WAVAMIZI HAWANA HURUMA NA WAZANZIBARI , wanatumia kila mbinu hata kutuuwa wakati wa chaguzi , Allah awalani hawa watu watiliane masumu wenyewe kwa wenyewe wauwane. Aaamin
 
Anawashukuru watu?
Kwani haki haijaamua?
Mbona mnatuweka mtanziko?
Kwani wameachiwa na mahakama na hawa marais wetu wawili?
Nijuavyo mm wazanzibar kwa sasa ni muda wao wa kutesa hapa mjini, lkn ni hawahawa ndo walio na fujo juu ya masuala ya Muungano. Mm nadhani hatuwezi kuishi na wazanzibar kwa kukamiana eti kisa Muungano. Ikiwapendeza wabaki na Zanzibar yao. Kwa sasa Marais wrote ( was Zanzibar na was Muungano wanatoka Zanzibar ) jambo ambala haitakuja kutokea rais wa Zanzibar akatoka Bara.
 
Waje tuwaunge kamati ya amani kupinga matumizi ya neno Mwendazake
 
Amshughulikie kwa kumbariki Safi sana
Ninyi si mlikuwa mnashabikia udhalimu
susp.png
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Magufuli unayemchukia ametawala Tanzania kwa miaka 6 tu. Masheikh wamekaa mahabusu miaka 9 kwa zaidi ya miaka mitatu ya Magufuli. Kumlaani Magufuli ni kumwonea.
Ndugu, nikwambie kitu, kwa hali ninavyoiona katika Mitandao ya kijamii, nadhani kama kweli kuna siku ya hukumu, basi tujiandae kuhojiwa na kujibu mambo mengi sana. Zaidi no chuki binafsi tu. Watu wanashindwa kujikontroo, hawana kipimo cha kumpenda au kumchukia MTU. Jambo ambal ni hatari sana.
 
Nashauri masheikh warudi tena mahakamani kudai fidia. It took 9 yrs kwa upande wa jamhuri kusema hatuna mamlaka ya kusikiliza kesi. Huku ni kunajisi mfumo wa sheria.
 
Waachiwe wafungwa wooote wanaoonewa sio mnaachia kwa kuangalia vinasaba... na walopotea warudishwe pia iwe hai au wamekufa! warudishwe!! Hii nchi watu hawako conscious kabisa hakuna cha kusifia hapa!! Kunatofauti kubwa kati ya haki na upendeleo...
 
Kwani kusema hatutaki muungano ni dhambi ndani ya biblia au Quran, au katiba ya uVAMIZI YA MUUNGANO ??
Ni haki yenu kuukataa Muungano! Lakini tatizo linakuja pale mnapotumia njia zisizofaa! Kuua raia wasio na hatia, kuwamwagia Wakristu tindikali au kuchoma nyumba zao za ibada, kwa mgongo wa kuukataa Muungano, ni jambo lisilo kubalika kwa wapenda amani.
 
Back
Top Bottom