Shehe Ponda Issa Ponda ataka serikali isiingilie mambo ya Al-Shaabab

Tz kuna mipaka ya somalia au anavysm wanlnd mpk yao ilhali wameingia tz manake nn?duh noooma.
 
Hapo kwenye red wana agenda gani Kenya??
Kuhusu swala la serikali na dola kutumia tishio la Al Shaabab kama sababu ya kutisha na kuogopesha watanzania binafsi siliafiki na nina muunga mkono Sheikh Ponda kuhusiana na hilo, Ila;
Je, ni sahihi Sheikh Ponda kuhusishanisha uislamu na Al shabaab??
Je, anayepinga mashambulio ya Al shabaab anaupinga uislam???
Je, waislamu wanaowakilishwa na Sheikh Ponda wanaridhia kuwa fedheha dhidi ya Al Shaabab ni fedheha dhidi ya waislamu???

Nyie wagalatia kuweni na akili sasa. Serikali inasingizia al shabab ili ihalalishe kuwakamata vijana wa kiislam. Pia oneni kenya imeingia vitani na ndo wanapata mashambulizi zaidi na watu wake wanafa zaidi. Pia AL-shabab msiwalaumu wapo vitani kama kenya inavyoua Raia wasio na hatia kule somalia nao Alshabab wanajihami. Na vita kwao ni kuangusha majengo marefu.
 
Wajamaa hawa Al shabaab tusiwaingilie kabisa tz. wakenya hadi sasa wamelikoroga kuwafuata kwao maana sijui kama watawamaliza,kinachotakiwa nikua makini na mipaka yetu hilo ndio muhimu kwa wakati huu
 
Haya mambo ya Al shabab yananikumbusha enzi zile akionekana mzungu yeyote na nyendo zisizoeleweka eleweka basi atakuwa ni kaburu anataka kutega bomu!!!!

C'moon serikali Al shabaab inayowaua watanzania kilia siku ni EPA, meremeta, deepgreen and where is the govt on that?
 
25 NOVEMBER 2011



Na David John

KAMATI ya Kutetea Haki za Waislamu nchini, imeihadharisha Serikali kutojihusisha na mambo ya kidini hasa yanayohusu kundi la Al-shaabab kwa shinikizo la mataifa
makubwa.

Katibu wa kamati hiyo, Shekhe Ponda Issa Ponda, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema kamati hiyo imemwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha, kupinga kauli yake aliyowataka Watanzania kuwa makini na wahamiaji haramu ili kudhibiti kundi hilo lisiingie nchini.

Shekhe Ponda alisema ni vyema Serikali ikawa makini na sera za mataifa makubwa ambayo yameingia katika migogoro na baadhi ya nchi za Afrika kwa maslahi binafsi.

“Serikali iache kujiingiza katika migogoro na kundi hili, jambo la msingi ni kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu si vinginevyo,” alisema Shekhe Ponda na kuongeza kuwa, si kweli kwamba kundi hilo ni la kigaidi kama alivyosema Bw. Nahodha bali kinachofanywa na kundi hilo ni kulinda mipaka ya nchi yao.

Alisema Bw. Nahodha hapaswi kuwaweka Watanzania katika hofu ya kuvamiwa na kushindwa kusafiri kwa shughuli mbalimbali ambazo ndioz huwapatia kipato na kukuza uchumi wao kutokana na taarifa za upotoshwaji dhidi ya kundi hilo.

“Waziri anapozungumzia kundi hili ni sawa na kudhalilisha Uislamu, mbona hivi karibuni wameingia Wakongo wakiwa na silaha nzito lakini Serikali haikufanya kitu, kwanini Al-Shaabab,” alihoji Shekhe Ponda.

Bw. Ponda alisema kauli iliyotoa Bw. Nahodha, imelenga kuwagawa Watanzania ili waichukie nchi ya Somalia kitu ambacho si sahihi.

Hivi karibuni, Bw. Nahodha alisema kutokana na nchi jirani ya Kenya kukumbwa na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na kundi hilo, umefika wakati wa Watanzania kuwa makini na watu ambao wanaingia nchini kinyemela bila kufuata utaratibu




Aweke vizuri maelezo yake huyu
Kwani huyu Pondo ameishia la darasa la ngapi,
Ujinga, ujinga,ujinga........................
 
Wakuu ina maana huyu shekh hajaingizwa kwenye daftari la mgao wa ccm? mbona anamponda vuai na anatetea magaidi wa alshabab? Shekh angefunguka zaidi kwa kuiponda Alshabab wa Tz ambao ni ccm na polisi wanao walipua wananchii kwa dhiki, dhihaka na karaa wanazopata shekh angewaeleza hawa ccm kwanza..na nijuavyo mimi alshabab ni kikundi cha kigaidi ina maana gaidi akiwa mwislam ni halali kidini ya kiislam..? au alindwe na kutetewa tu sababu ni mwislam? enzi za mwalimu mashekhe na ma padre walikuwa wanapima kauli zao kabla ya kuingiza public lakini siku hizi kila mtu anaropoka anavoweza..
 
Hivi ugaidi ni nini? Maana kwa definition yake vikundi vya waasi wote duniani ni vikundi vya kigaidi....narudia hivi vikundi havitaisha kama sera za nchi za magharibi hawataacha invasion kwenye ardhi zingine...hivi hao USA,NATO mnaowatetea kila siku wameua watu wangapi? Mbona wao hawaitwi killerz? Na anesema eti uislamu unaruhusu MAUAJI athibitishe maneno yake kutoka katika vitabu vyao nadhani ndo mjadala utakuwa wa kisomi zaidi
 
Tukirudi nyuma kidogo ,kuna nakala moja ya Gazeti la An-Nuur liliandika mbinu na mipango ya kumuondowa Rostam peke yake, na kuwasafisha watuhumiwa wengine ,na hilo leo ndio limeanza kutendeka imeamuliwa iundwe kamati ya kuwasiliza wale wanao tuhumiwa lakini hakuna shaka kila mmoja wetu tunajuwa fika (tunaelewa)nini matokeo ya kamati hiyo (nikuwasafisha)
 
CIA walipomuua patrice Lumumba na kumtia kwenye Tindikali na kuiweka DRC katika civil wars hayo mnakenua tu na vip wale waasi wa ANGOLA walivamia basi la Wachezaji wa TOGO hivi ule sio UGAIDI? Vip Tamil Tigers wanaua kila siku watu wasio(sio waislam ni wahindu na wanajilipua mabomu) na Hatia sio magaidi? Na NRA, UNITA Hawa sio magaidi? Vp mbona serikali ya kikoloni ya waingereza waliwaita akina Ariel Sharon na Rabin magaidi na kundi lao la utetezi la Agonar vp ugaidi umehamia kwa makundi ya kiislam tu? JOSEPH KONI anafanya Uasi kwa kisingizio cha Amri kumi za mungu anaua watu lakini wanaitwa REBELS sio TERRORISTS? Hata George washington aliitwa Gaidi na waingereza kwenye struggle yao 1776....mezeni propaganda za media kama kawaida yenu ndo maana Malcom X alisema "there is nothing strong is this world like the Media"
 
Wakuu ina maana huyu shekh hajaingizwa kwenye daftari la mgao wa ccm? mbona anamponda vuai na anatetea magaidi wa alshabab? Shekh angefunguka zaidi kwa kuiponda Alshabab wa Tz ambao ni ccm na polisi wanao walipua wananchii kwa dhiki, dhihaka na karaa wanazopata shekh angewaeleza hawa ccm kwanza..na nijuavyo mimi alshabab ni kikundi cha kigaidi ina maana gaidi akiwa mwislam ni halali kidini ya kiislam..? au alindwe na kutetewa tu sababu ni mwislam? enzi za mwalimu mashekhe na ma padre walikuwa wanapima kauli zao kabla ya kuingiza public lakini siku hizi kila mtu anaropoka anavoweza..
Ata wewe unaropoka unavyoweza ndo serikali imeachia watu wapige domo wee uhuru wa maoni na ni subjective we ukiona la mwenzio pumba the contrary is true to him to your opinions acheni watu wafunguke tu..
 
Hapa kwenye Udini ndo sihusiki kabisa, ila nimegundua kuna watu wana mapenzi ya dhati sana na tamaduni za watu wengine na nachokiona hapa ni total contradiction, ila Al shabaab, Shekh Mponda, Serikali ya Magamba, na hata kina Pengo wanafahamu wanachozungumza na wanayemtumikia:eyebrows:
 
Hivi ugaidi ni nini? Maana kwa definition yake vikundi vya waasi wote duniani ni vikundi vya kigaidi....narudia hivi vikundi havitaisha kama sera za nchi za magharibi hawataacha invasion kwenye ardhi zingine...hivi hao USA,NATO mnaowatetea kila siku wameua watu wangapi? Mbona wao hawaitwi killerz? Na anesema eti uislamu unaruhusu MAUAJI athibitishe maneno yake kutoka katika vitabu vyao nadhani ndo mjadala utakuwa wa kisomi zaidi

Pole sana ndugu,ukipewa mahali pa kupata ushahidi huendi kutazama unaendelea kulalama tu!
 
Pole sana ndugu,ukipewa mahali pa kupata ushahidi huendi kutazama unaendelea kulalama tu!

ushahidi upi? Ebu ulete jamvini tuuone binafsi sikuona cha maana kule ni mitizamo hasi kama uliyonayo wewe! Ebu ulijibu swali hili kama nawe ni mpenda haki za binadamu...USA na NATO na coalition nations hivi watu wanaowauwa huwa sio nafsi? Au umejaa itikadi hasi? Maswali yangu ungeyajibu nadhani tungeendelea! Pole nawe kwa kumeza propaganda za Media kama samaki anavyomeza ndoano na chambo
 
Back
Top Bottom