Shehe Ponda Issa Ponda ataka serikali isiingilie mambo ya Al-Shaabab | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shehe Ponda Issa Ponda ataka serikali isiingilie mambo ya Al-Shaabab

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 25, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=2]25 NOVEMBER 2011[/h][h=3][/h]

  Na David John

  KAMATI ya Kutetea Haki za Waislamu nchini, imeihadharisha Serikali kutojihusisha na mambo ya kidini hasa yanayohusu kundi la Al-shaabab kwa shinikizo la mataifa
  makubwa.

  Katibu wa kamati hiyo, Shekhe Ponda Issa Ponda, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari.

  Alisema kamati hiyo imemwandikia barua Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha, kupinga kauli yake aliyowataka Watanzania kuwa makini na wahamiaji haramu ili kudhibiti kundi hilo lisiingie nchini.

  Shekhe Ponda alisema ni vyema Serikali ikawa makini na sera za mataifa makubwa ambayo yameingia katika migogoro na baadhi ya nchi za Afrika kwa maslahi binafsi.

  “Serikali iache kujiingiza katika migogoro na kundi hili, jambo la msingi ni kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu si vinginevyo,” alisema Shekhe Ponda na kuongeza kuwa, si kweli kwamba kundi hilo ni la kigaidi kama alivyosema Bw. Nahodha bali kinachofanywa na kundi hilo ni kulinda mipaka ya nchi yao.

  Alisema Bw. Nahodha hapaswi kuwaweka Watanzania katika hofu ya kuvamiwa na kushindwa kusafiri kwa shughuli mbalimbali ambazo ndioz huwapatia kipato na kukuza uchumi wao kutokana na taarifa za upotoshwaji dhidi ya kundi hilo.

  “Waziri anapozungumzia kundi hili ni sawa na kudhalilisha Uislamu, mbona hivi karibuni wameingia Wakongo wakiwa na silaha nzito lakini Serikali haikufanya kitu, kwanini Al-Shaabab,” alihoji Shekhe Ponda.

  Bw. Ponda alisema kauli iliyotoa Bw. Nahodha, imelenga kuwagawa Watanzania ili waichukie nchi ya Somalia kitu ambacho si sahihi.

  Hivi karibuni, Bw. Nahodha alisema kutokana na nchi jirani ya Kenya kukumbwa na vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na kundi hilo, umefika wakati wa Watanzania kuwa makini na watu ambao wanaingia nchini kinyemela bila kufuata utaratibu   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  aisee.... sasa hapa anawatetea au anawasemea alshababu the killers?
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Sasa inamaana Waslamu wetu wa Tanzania wana habari toka AL-Shaab cha kufanya ili tusivamiwe?

  Tanzania ina kosa gani nao? Au ndio Chuki ndani za roho za hao wanadamu?
   
 4. L

  LAT JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  hivi al shabaab ni kundi la kidini au kigaidi?
   
 5. T

  Thesi JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hapa ndipo uislamu inapokuwa dini ya utata. Na Mungu wao kama Mungu wa kusadikika. Alshabab ni kundi la kigaidi au la kidini? Kwa hiyo serikali ya Somalia wanaopigana na Alshabaab si waislamu ila Alshabaab?

  Kwa hiyo kundi linaloua na linalojisifia kuua ni waislamu safi? Kwa maana hiyo uislamu unaunga mkono wauaji? Ushasikia wapi kiongozi wa kanisa akiwatetea magaidi kama LRA eti kuwa si magaidi kwa kuwa ni wakristo?

  Itajitetea vipi kuwa si dini ya ugaidi na mauaji?
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Alichoongea Sheikh Ponda kina maana kubwa sana kwa siasa za Tanzania. Serikali inawatumia Al Shabaab kama excuse ya kupitisha agenda zao za kuzuia maandamano. Serikali inawatumia Al shabaab kama njia ya kuminya uhuru wa watanzania kwa kuwatisha. Serikali inawatumia Al Shabaab kama njia ya kuua uchumi wetu kwa kutisha watalii na wawekezaji kuja Tanzania bila serikali kujua.

  Kwa maana hiyo Serikali inaonekana itakuwa tayari kuwadhuru watanzania either kwa kulipua sehemu ili kuonesha kuwa wao walichokuwa wanasema kina ukweli.

  Tunataka tishio la Al shabaab lisiwe wimbo wa kubembelezea mwana Tanzania. Watanzania ni watu wenye hulka ya utulivu na kutopenda misukosuko, matamko kama haya ya viongozi wetu yanawaandaa watanzania kuwa watu wa kujiandaa na vurugu na uvunjifu wa amani.

  Al Shabaab wana agenda yao huko Somalia, kama ni wauaji au magaidi hiyo suala la atakayewaona. Hata Gaddafi aliwaita NTC Magaidi, Al Qaeda. ANC iliitwa chama cha kigaidi na mandela akaitwa Gaidi. Tusiwe matarumbeta ya propaganda. Kazi ya serikali ni kuhakikisha mipaka yetu ipo salama na watanzania wanaishi vile watakavyo wao bila kuwa influenced na tukio lolote la kutoka nje.

  Ponda ameongea kitu ambacho ni wachache wanaweza kuongea, whether ana sympathise na Al Shabaab hiyo inatokana na jinsi anavyowaona yeye, kikubwa ni kwamba haoneshi nia wana hana nia ya kumzuru mtanzania yeyote yule.
   
 7. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Thanks waislamu hata mimi nilidhani kweli. Unajua watu wasio na sera na upeo wanapenda kurukia mambo ambayo hayapo kwenye scope yao ya kazi na kuyafanya priority. sasa kila mtu al shabab al shabab mim i inanikera saana kwa tz kufanya hivyo. brilliant waislam.
   
 8. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  ushauri wangu wa kiintilejensia huyo sheikh achunguzwe na ikibidi ahojiwe kwa kauli yake hyo ambayo wazi kabsa inaonesha ni mtetez wa al-shabaab, eti wanalinda mipaka ya nchi yao foolish pondaaaa..
   
 9. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,804
  Likes Received: 36,842
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Somalia iliwaunga mkono Kenya kwa kazi ya kupambana na kuwathibiti Alshabab, Sasa Sheikh Ponda anawatetea Alshabaab kuwa wanalinda mipaka ya nchi yao, ni mipaka ya nchi gani anayoizungumzia Sheikh kuwa inalindwa na Alshabaab while Somalia inawapiga vita hao wanaoitwa walinda mipaka na Ponda???
  Kwa kweli wanaowakilishwa na Sheikh huyu wanachoreshwa tena kwa ngazi ya kimataifa.
   
 10. K

  KIBONGOMKUTI JF-Expert Member

  #10
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 1,415
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Sheikh Ponda katika hili ni vyema akaweka bayana kuwa anawasilisha msimamo wake binafsi, haiingii akilini kiongozi wa kidini kuunga mkono watu wanaonyofoa roho za watu kwa maslahi yao binafsi.

  Pia inatia shaka juu ya ufahamu,uelewa na lengo la huyu Sheikh Ponda kwa hawa jamaa wa Alshababu. Ki-mtazamo wangu hawa jamaa hawafuati misingi ya Dini ya Kiislamu ambayo tunaambiwa kuwa ni Dini ya AMANI na HAKI.

  Huu ni wakati muafaka wa Serikali yetu kuchukua hatua za makusudi kuhusu haya MATAMKO ambayo ni vyema yangeitwa ******. Nasikitika kusema kuwa siku hizi kila mtu akiamka asubuhi anatoa TAMKO.

  Hii ni nchi gani ambayo haina mipaka katika uhuru wa kutoa maoni hata kama kwa kufanya hivyo kuna hatarisha amani ya nchi na maslahi ya watu wengine?
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Kwani Al shabab ni waislamu???? na kuna uhusiano gani kati ya Uislam na ugaidi??????
   
 12. T

  Tata JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,736
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana kimsingi na mtazamo wa Sheikh Ponda kuwa serikali isigeuze Al-Shabaab kuwa mtaji wa kuminya haki za watanzania na kuzuia shughuli za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Ila sina uhakika kama wanachofanya Al shabab ikiwemo kuteka, kuua watu, kuzuia misaada ya kibinadamu kupelekwa maeneo wanayotawala etc, ni kwa maagizo ya dini yao ya kiislamu. Na sidhani kuwa waziri alipozungumzia kundi la Al Shabaab alikuwa anaudhalilisha uislam kama huyu Sheikh anavyodai.
   
 13. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuua watu kwa mabomu kama kule Kampala ndio kulinda mipaka. Sheik Ponda anatetetea kundi linalotumia mbinu chafu kama hizi kwamba ni uislam?
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,804
  Likes Received: 36,842
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red wana agenda gani Kenya??
  Kuhusu swala la serikali na dola kutumia tishio la Al Shaabab kama sababu ya kutisha na kuogopesha watanzania binafsi siliafiki na nina muunga mkono Sheikh Ponda kuhusiana na hilo, Ila;
  Je, ni sahihi Sheikh Ponda kuhusishanisha uislamu na Al shabaab??
  Je, anayepinga mashambulio ya Al shabaab anaupinga uislam???
  Je, waislamu wanaowakilishwa na Sheikh Ponda wanaridhia kuwa fedheha dhidi ya Al Shaabab ni fedheha dhidi ya waislamu???
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  Nov 25, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hata mimi nashangaa
   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  Nov 25, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nyuki huwa hawaumi mpaka uwachokonoe kwenye mzinga wao. Kawaulize wakenya hilo swali waliwafanya nini Al shabaab?.

  KUHUSU HOJA YA SHEIKH PONDA ANATUMIA UHURU WAKE WA MAWAZO NA SI WOTE LAZIMA TUYAKUBALI AMA KUYAKATAA ILI MRADI TU UHURU HUO HAUTISHII UHURU WA WENGINE.
   
 17. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #17
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,804
  Likes Received: 36,842
  Trophy Points: 280
  Sheikh Ponda anaongea kama muwakilishi wa waislam, Je ni msimamo wa waislam wote wa Tanzania kuwa Nahodha afute kauli zake dhidi ya vitisho vya Al shabaab kwa sababu Al shabaab ni waislam??
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Haya sasa; chimbuko la kundi la kigaidi Al-Shaabab lapata watetezi nchini Tanzania.

  Alhaj Rostam Aziz katuongezee fedha tukawaandikishe wengine wengi zaidi kujiunga na jeshi hilo 'rafiki' linalolinda Uislamu ndani na nje ya mipaka ya Somalia.

  Vile vile tunazo taarifa kwamba baadhi ya msikiti yetu nchini ni maeneo 'patakatifu sana' kwa wanachama wa kundi hili hatarishi la Al-Shaabab kuishi na kukamilisha biashara zao and withe the full knowledge and glare of our security apparatus anyway.
   
 19. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #19
  Nov 25, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Majibu: ktk uislam kuua si vibaya kama unamtetea allah au mtume! kwaufupi hata mtume wao aliua sana ktk kueneza uislam, the same spirit is working up today!
   
 20. y

  yaya JF-Expert Member

  #20
  Nov 25, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uelewa wa nini kinaendelea katika dunia yetu ni kitu muhimu sana. Hivi mkuu, ulitegemea Alshaabab waingie Kenya na kuteka watalii na hivyo kuathiri sekta ya utalii na uchumi wa nchi yao, halafu Wakenya wakae wanawaangalia tu na kuwachekea? Katu, wamechokoza nyuki. Kuhusu uhuru wa kuongea, mkuu, hatukatai lakini walau anachokiongea kiwe na mantiki kikiendana na uhalisia.
   
Loading...