Shetani hawezi kukubali Yesu kuwa mwana wa Mungu. hilo ndilo shetani analopingana nalo sana. sababu anajua hicho cheo ni kikubwa sana na kinazidi kumuondoa na kumuweka mbali zaidi zaidi na nia yake ya kujifanya ni mungu. lakini kwa mimi mtu akinambia Yesu si mwana wa mungu. haindhuru kitu kabisa. maana kwa yeye kuamini hivyo ni sawa kabisa na si ajabu. ingekuwa ajabu anapokubali jambo hilo. so hata ukimtukana Yesu na ukaikanyaga biblia n. wala haina athari kwangu kwa sababu Mungu wangu yupo ndani yangu na ukuu wake umeonekana kwa namna nyingi. na lakini yeye alikataa kupigana vita vya damu na nyama kupigania ukristo. alisema vita vyenu si vya damu na nyama bali ni dhidi ya mfalme wa anga hili,mfalme wa giza.
una uhuru kabisa wa kuamini Yesu si lolote si chochote. unaweza mfananisha na watu wengine wengi upendavyo lakini kwa mimi " kwa maana neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu"1wakorintho1-18" na Mungu alichagua mambo dhaifu ya dunia ili awaaibishe walio na nguvu.
(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome😉"
2 wakorintho 10:4