Shehe Khalifa jibu maswali haya

Shehe Khalifa jibu maswali haya

Siwezi kuunga mkono hoja inayotokana na mnafik KHALIFA KHAMIS hata kama yupo sahihi. KHALIFA ana alama zote zinazofaa yeye kuitwa mnafik. Khalifa anatafuta Kiki kw kuchukua Akili wa waislam ambao si wanaccm. msishangae Khalifa huyo huyo kesho akaja kuyakanusha yote aliyoyatamka kwa kuwa haya hayatoki moyoni mwake bali aliyoyaongea yamo mioyoni mwa waislam wengi ambao si waassm.

Kwani huo unaoitwa upendeleo haujaanza leo toka serikali ya ccm.

Khalifa analijua hilo. Siwezi muunga mkono mnafik Khalifa hata kama anachoongea yu sahihi. Khalifa ni mnafik mnafik.

Na zuri zaidi ni kubwa tuna maelezo yanayoitwa nyeti kuwa taarifa hizi za upendeleo zishamfikia mkuu wa kaya na keshawaita viongozi wa kiislam (mashekhe) mbao ni wanachama wa ccm chini ya mwanvuli wa Baraza Lao. kuwa anataarifa za malalamiko kuwa ana upendeleo ktk uteuzi. Kikao hicho kimefanyika miezi zaidi ya sita. mkuu wa kaya akasema tatizo lililopo ni kuwa yeye kama yeye anajua kuwa kuna idadi kubwa ya wasomi waislam nchini lkn yy kama yy hawajui na wala hana orodha ya waislamu wenye sifa, kama angeletewa orodha ya waislam wenye sifa za kulitumikua taifa yaani elimu, maarifa, , uzoefu, uadilifu yeye angewateua Na akawaomba mashekhe wale wapelekee orodha. Sasa ni zaidi ya miezi 6 orodha haijapelekea tofauti na upande wa pili wao walipeleka orodha wa wasomi inayoona wanafaa kutumikia taifa hili hata kabla wajaombwa kufanya hivyo . Na kwa kufanya hivyo si kosa.

Badala yake viongozi wetu waliishia kumsifia na kumpongeza kuwa anafanya kazi kwa weledi bila ubaguzi.

Tuseme tu kama habari hizo ni za kweli na zinatoka kwa mkuu wa kaya basi mkuu ana hoja na haipaswi kubezwa bali tuifanyie kazi. Bali kama ni maneno ya vijiwe kwa kahawa basi
tuna kitu ziada cha kufanya. mi niwaombe taasisi ya wana taaluma waislam TAMPRO kama wapo humu wapeleke orodha ya Muslim proffessionals kwa mufti hapo Watakua wametimiza wajibu wao. Muft na wanachama wenzie watamfikisha kwa mkuu wa kaya au mpambanaji wenziwe MKM kwani yy kaonyesha kutaka ukaribu hata na viongozi waislam wasio wanachama wa ccm.

Nadhani hii itakuwa moja ya hatua mzuri. lkn ikipelekwa orodha ya bado tusione mrejesho wake basi kura yako ndio iwe mustakbali wako.

Waislam wanaweza kuiondoa serikali iliyo madarakani kwa tutumia kura tu na huu ujinga wa sijui hamjasoma ukaishilia mbali.

Ni wajibu wetu tuachane na msimamo ya kuegemea vyama ambayo sio karata kwetu ya kututendea haki. Tunapoamua tuamue kupiga kura ya maslahi sisi kama jamii na sio wa maslahi ya chama fulani. Kura yetu iwe kura ya kuamua nani awe kiongozi wetu.

Lkn huyu kada Khalifa ni njaa tu inamsumbua kwasasa na akishapata anachotaka huwageuka wenzie kama kinyonga anavyojigeuza rangi.

Siwezi kuunga mkono hoja inayotokana na mnafik KHALIFA KHAMIS hata kama yupo sahihi. KHALIFA ana alama zote zinazofaa yeye kuitwa mnafik. Khalifa anatafuta Kiki kw kuchukua Akili wa waislam ambao si wanaccm. msishangae Khalifa huyo huyo kesho akaja kuyakanusha yote aliyoyatamka kwa kuwa haya hayatoki moyoni mwake bali aliyoyaongea yamo mioyoni mwa waislam wengi ambao si waassm.

Kwani huo unaoitwa upendeleo haujaanza leo toka serikali ya ccm.

Khalifa analijua hilo. Siwezi muunga mkono mnafik Khalifa hata kama anachoongea yu sahihi. Khalifa ni mnafik mnafik.

Na zuri zaidi ni kubwa tuna maelezo yanayoitwa nyeti kuwa taarifa hizi za upendeleo zishamfikia mkuu wa kaya na keshawaita viongozi wa kiislam (mashekhe) mbao ni wanachama wa ccm chini ya mwanvuli wa Baraza Lao. kuwa anataarifa za malalamiko kuwa ana upendeleo ktk uteuzi. Kikao hicho kimefanyika miezi zaidi ya sita. mkuu wa kaya akasema tatizo lililopo ni kuwa yeye kama yeye anajua kuwa kuna idadi kubwa ya wasomi waislam nchini lkn yy kama yy hawajui na wala hana orodha ya waislamu wenye sifa, kama angeletewa orodha ya waislam wenye sifa za kulitumikua taifa yaani elimu, maarifa, , uzoefu, uadilifu yeye angewateua Na akawaomba mashekhe wale wapelekee orodha. Sasa ni zaidi ya miezi 6 orodha haijapelekea tofauti na upande wa pili wao walipeleka orodha wa wasomi inayoona wanafaa kutumikia taifa hili hata kabla wajaombwa kufanya hivyo . Na kwa kufanya hivyo si kosa.

Badala yake viongozi wetu waliishia kumsifia na kumpongeza kuwa anafanya kazi kwa weledi bila ubaguzi.

Tuseme tu kama habari hizo ni za kweli au maneno ya vijiweni tu tuna kitu cha kufanya. mi niwaombe taasisi ya wana taaluma waislam TAMPRO kama wapo humu wapeleke orodha ya Muslim proffessionals kwa mufti hapo Watakua wametimiza wajibu wao. Muft na wanachama wenzie watamfikisha kwa mkuu wa kaya au mpambanaji wenziwe MKM kwani yy kaonyesha kutaka ukaribu hata na viongozi waislam wasio wanachama wa ccm.

Nadhani hii itakuwa moja ya hatua mzuri. lkn ikipelekwa orodha ya bado tusione mrejesho wake basi kura yako ndio iwe mustakbali wako.

Waislam wanaweza kuiondoa serikali iliyo madarakani kwa tutumia kura tu na huu ujinga wa sijui hamjasoma ukaishilia mbali.

Ni wajibu wetu tuachane na msimamo ya kuegemea vyama ambayo sio karata kwetu ya kututendea haki. Tunapoamua tuamue kupiga kura ya maslahi sisi kama jamii na sio wa maslahi ya chama fulani. Kura yetu iwe kura ya kuamua nani awe kiongozi wetu.

Lkn huyu kada Khalifa ni njaa tu inamsumbua kwasasa na akishapata anachotaka huwageuka wenzie kama kinyonga anavyojigeuza rangi.

Sikiliza ndugu yangu, wewe unakiri kuwa Aliyoyasema sheikh Khalifa yana ukweli lakini wewe chuki yako iko tu kwa sheikh Khalifa, sisi hatuna haja ya kujua sheikh Khalifa ni nani sisi tuko Interested kujua facts!. Na Sheikh Khalifa kaja na data, na kwa kuwa data zimewekwa hapo sasa kataa facts kwa kuleta facts siyo kwa kushambulia personality ya mtu, hilo ni jambo la kwanza.

Pili wanaopropose majina na kufanya vetting kwa ajili ya teuzi mbalimbali siyo Makanisa wala Misikiti, Hapa utakuwa umetuingiza chaka ndugu yangu, haiwezekani Mtawala akawaambia Masheikh au Maaskofu wampe majina ya kuwateua katika kazi za Umma, Isipokuwa ni Jukumu lake kama ana nia ya dhati kubalance teuzi ili ziwe na sura ya kitaifa kuwaambia hao wenye dhamana ya kufanya vetting wampe watu wenye background tofautitofauti ili kuwepo na diverse demography katika serikali.

Vyombo vya serikali kama vile Vyuoni, TCU , Kwenye Mashirika ya Umma kote huko kuna watu, na rekodi zao, Haiwezekani vyombo vya vetting vikawa kila wakati vinawapata watu wa mrengo mmoja kwa wingi halafu eti vyombo hivyohivyo visiwaone wa mrengo mwingine. Ninachokiona mimi binafsi ni kuwa havijafanya juhudi za kutosha kuondoa hili gepu la kijamii.

Simtetei sheikh Khalifa lakini zile data alizoweka, kwa mtu yeyote aliye na fikra zisizo biased bila kujali dini yake, zile data zinafikirisha kaka, na ni vyema serikali ikatoa majibu la sivyo nahofia hii ni kansa inayotutafuna polepole!
 
Napenda kumwomba shehe Khalifa ajibu maswali haya:

1.Mashehe na maimamu wangapi wana PhD? Pia Maaskofu, mapadri na wachungaji wangapi wana PhD

2. Je unategemea viongozi wa dini wasio na elimu wataweza kuhamasisha waumini wao kusoma?

3. Viongozi wa sampuli IPI wanatazamiwa kuwa walalamishi? Ni wale ambao kwa wastani elimu yao ni ya chini au wale ambao kwa wastani elimu yao ni ya juu?

3. Kwa wastani kati ya shule zinazomilikiwa na mashirika/dini ya kiislamu na zile zinazomilikiwa na mashirika/dini ya kikristo ni zipi zinafanya vizuri kitaaluma?

4. Hivi kama shule za waislamu ambazo wanaosoma huko wengi ni waislamu hazifanyi vizuri kulinganisha na za wakristo ambazo wanafunzi wake wengi ni wakristo (wale wengine wanaogopa kusoma na makafri), unategemea muujiza UPI wale wasiofanya vizuri wawe wengi vyuoni? Ukifahamu kuwa dini siyo kigezo kwenye mchakato wa udahili vyuoni?

5. Hivi kuna Madrasa ngapi na kuna shule za sekondari ngapi wanazomiliki waislamu!

6. Samahani, hivi she he Khalifa na shekhe Ponda mmesoma mpaka wapi vile? Kama nyie mmesoma kwa nini hamkuhamasisha na wenzenu wasome? Kama nyie hamjasoma kwa kiwango cha juu mnategemea wenzenu wangesomaje?
Mwisho naomba wadau tuanike hapa matokeo ya kidato cha NNE ya shule za waislamu kama vile kinondoni Muslim na zile za wakristo kama vile Loyola. Hii itasaidia jamii kuona kuwa ni ufaulu wala siyo dini au upendeleo uliopelekea tofauti za kielimu miongoni mwa dini mbalimbali.

Ushauri:

Japo hawa ndugu zetu wamekumbuka shuka kukiwa kumekucha, nawashauri wahamasishane kusoma, na waweke kigezo cha angalau shahada ya kwanza ili MTU awe shehe! Waige mazuri ya wenzao! Huwezi kukuta Padri asiye na elimu lakini kwa wenzetu ni aibu hata kusema! Ndio maana ni wataalamu wa kulalamika na kudai nafasi za upendeleo!

Haiingii akilini jamii mbili zenye tofauti kubwa kielimu zitegemewe kuwa na nafasi sawa kwenye jamii. Hivi kama Leo Rais akiamua kuteua viongozi wa dini mbalimbali kuwa mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi lakini kwa kigezo cha kuwa na angalau Masters digrii, hivi ni mashehe wangapi wangepenya? Kwa wakristo maaskofu wengi wana PhD acha mbali na masters na bachelors za kumwaga! Hapo Shehe Khalifa angesema Rais ametutenga!

Hivi watoto wa shehe huyu anayewafahamu wamesoma mpaka wapi? Unaweza kukuta MTU analalamika kumbe hata watoto wake mwenyewe hajawapa fursa ya kusoma mpaka ngazi za juu!
Vyeti ni vyao kweli au ni kama kawaida.
 
Umeandika maneno meengi lakni ni upuuzi mtupu hilo unaliona ss hivi na huo mfumo kristo toka enzi za baba yenu wa taifa kabla ya kuja na jambo hili anagalia kwanza toka uhuru viongozi wa baraza la mitihan walikua dini gani ndio urudi hapa hayo ma phd ya kutafutiwa tu na usijidanganye ww ongelea kizazi cha sasa waislm sio wajinga tena ila nafas hawapewi utajuaje elimu zao endelezeni tu huo mfumo kristo wenu ipo siku watu tutachoka
Acha ujinga. Kama watu wa kuwalaumu ambao wamepoteza mwelekeo wa uislamu ni Waarabu walivyokuja kututawala. Embu fananisha utawala wa waarabu na waingereza au wajerumani. Waarabu hawakua na nia nzuri yoyote ya kuuendeleza uislam na elimu ya dunia. Zao zilikua biashara za utumwa tu na kunufaisha biashara zao. Hawakujali kuanzisha mashule kwa waislam wala nini. Huu ndio ukweli! Utake usitake. So laumu waarabu walioweka msingi mbovu huo. Unategemea nini. Angalia kuna waislam ilibidi wasome katika ma missionaries tena bila ubaguzi wowote. Wakristo hawakuwabagua. Lakini na elimu ya dini ya kikristo waliipata pia kwa walipenda. Usitake kurushia mpira wengine wakati tatizo unalijua na unataka ufumbie macho. Ni aibu.
 
Nilitegemea baada ya kupewa na Mkapa kilichokuwa chuo cha tanesco morogoro na kuwa chuo kikuu cha kiislamu pasingekuwa na manung'uniko tena
 
dada unazidi kuwaaibisha waislamu si bora ungenyamaza maana hata huna hoja unaleta tena mipasho. hapa tujitahidi tujibu hoja kisomi si kimipasho. unajua hii ndo inasababisha waislamu waonekane ni hopeless wamejawa na mapepo tu. mi nakushauri hebu jibu hoja achana na habari za mipasho na stori za kipuuzi.
sasa hivi waislam nao wameamka wanaenda shule na kuna chuo kikukuu mkapa aliwapa kama sikosei. so si haba elimu dunia(boko haramu) pia ipo ipo .kile kigezo cha kusema hawana elimu kitaisha ikiwa wakiendelea kusoma na kutumia elimu zao vizuri. uongo mama?

PHD inasaidia nn kama unaamini mcheza snema ndio mungu wako. Mfyuuuuuu! !!!!
 
Huwa namshangaa sana mtu anaejivunia hizi DINI mpaka mishipa inamtoka.

Hivi tusingetawaliwa hizi kelele zote zingekuwapo??

Kwa maoni yangu haya ni mawazo ya kitumwa.
 
Kikwazo kikubwa cha Waislaam ambacho kwa miaka nenda rudi wanakilalamikia ni NECTA kugeuzwa Parokia,Kwa akili yako unafikiri watumishi wa Necta wapo wangapi mpaka waislaam wakosekane kwa nchi nzima?

Unamaanisha hakuna waislaam wenye masters na PhD wanaotosha kufanya kazi NECTA?

Kwamba Mungu aliandika kuwa Watumishi wa NECT wawe waroma tu? Na huwa inatokea by chance na sio makusudi?

Mwaka 2013 NECTA ilipofumaniwa kuwafelisha vijana wa kiislaam kwa maelfu mpaka kupeldkea kutangaza matokeo ya form six mara mbili tena kimyakimya baada ya Kubananishwa kwa ushahidi usio na mashaka.

Wewe ni kama wakoloni,wakati wanatawala Afrika walikuwa wanaamini Waafrika ni wajinga na wanatoka bara la giza.

Waliamini kuwa Waafrika hawakuwa na Mfumo wa Elimu,hawakuwa na utamaduni,hawakuwa na ustaraabu

Lakini Waafrika wenyewe walijitambua na kuwafukuza wakoloni

Shida ni kwamba bado waafrika tunafikiria na kutenda kikoloni.
Huku sio kujitambua
 
Wewe una umri gan?

Na nan kakuambia kila muarabu ni muislam?

Ndiyo kina nyinyi mkienda huko uarabuni mkakuta makanisa na waaarabu wanaingia makanisani huku Wakiabudu kwa kutumia lugha ya kiarabu hamuamin mnadhan kama mpo misikitin

Kwa taarifa yako soma katika agents of colonialisms na slave trade utakuta kuna missionaries,traders and explorers

uislam at the first place ulipoingia uliingia na kupiga vita biashara ya utumwa

Tokea uislam anaufundisha nabii Muhammad suala la kupiga vita biashara ya utumwa lilikua ni la kwanza uislam kama dini ya hak haiwez kushabikia biashara ya dhulma na unyo yaji kama utumwa...

Uislam unapinga kila aina ya unyonyaji na dhulma

Pia hilo suala la waislam kutobaguliwa na hao wakoloni kipind wamekuja kueneza ukoloni wao wacha tuh nikupe homework ukajisomee huenda utapata mwangaza wa kujifunza mengineyo meengi.
Acha ujinga. Kama watu wa kuwalaumu ambao wamepoteza mwelekeo wa uislamu ni Waarabu walivyokuja kututawala. Embu fananisha utawala wa waarabu na waingereza au wajerumani. Waarabu hawakua na nia nzuri yoyote ya kuuendeleza uislam na elimu ya dunia. Zao zilikua biashara za utumwa tu na kunufaisha biashara zao. Hawakujali kuanzisha mashule kwa waislam wala nini. Huu ndio ukweli! Utake usitake. So laumu waarabu walioweka msingi mbovu huo. Unategemea nini. Angalia kuna waislam ilibidi wasome katika ma missionaries tena bila ubaguzi wowote. Wakristo hawakuwabagua. Lakini na elimu ya dini ya kikristo waliipata pia kwa walipenda. Usitake kurushia mpira wengine wakati tatizo unalijua na unataka ufumbie macho. Ni aibu.
 
NATANGULIZA KUKIRI KWANGU KUWA MIMI NI MWISLAM NA ALHAMDULILAH NIMESOMA.
NAIJIBU TU POST HII JAPO HUWA SIJIHUSISHI NA POST ZA KIJINGA KAMA HII (NIMESEMA ZA KIJINGA SIO ZA KIPUMBAVU), INANIBIDI KUJIBU HII KWA KUWA IMEGUSA DINI NA UISLAM NA KWA HOJA ZA KUUKEJELI UISLAM KAMA HIVI NASHINDWA KUKAA KIMYA.

NDUGU, NINGEDHANI UNGEANZA NA HOJA ZA SHEIKH KASSIM KASEMA NINI, HALAFU UJENGE HOJA KUANZIA HAPO, PILI UNGETOFAUTISHA BAINA YA MAONI YA SHEIKH KASSIM NA UISLAM, ALIYOYASEMA SHEIKH KASSIM NI YA SHEIKH KASSIM WALA UISLAM HAUJASEMA HAYO, HATA HAPA MIMI NAKUJIBU WEWE NIKIAMINI HAYA NI MANENO YAKO WALA SIO YA WAKRISTO NA UKRISTO.

TATU UNGEANZA KWA KUKUBALI AU KUZIPINGA HOJA ZAKE KWA KUZIWEKA ZA KWAKO ILI ZITUSAIDIE WANA JAMII FORUMS.

UMEONGEA KWA HISIA KALI SANA ZA KIDINI, SIJUI IMEKUCHUKUA SIKU NGAPI KUANDIKA UZI HUU, NAJUA UKIITAZAMA FAMILIA YAKO NZIMA UTAGUNDUA INA CONNECTION MAHALA FULANI NA DINI NYINGINE, HIYO MAANA YAKE SISI TUWAMOJA.

SHEIKH KHALIFA AMETOA TAKWIMU ZA UTEUZI, LABDA NINGEKUELEWA UNGESEMA KIGEZO CHA RAIS HAKIKUWA DINI KWAKE YEYE ALIKUWA ANATEUA MTU ANAEMFAA ZAIDI, MAANA NI UKWELI USIOPINGIKA RAISI ANATEUA KWA UTASHI WAKE, MAANA KIGEZO KINGEKUWA NI USOMI NAAMINI KWENYE BARAZA LETU LA MAWAZIRI WASINGEKUWA HAWA AMA WANGEKUWA WACHACHE KAMA PROFESA MUHONGO.

NDUGU, NAPENDA KUKUFAHAMISHA TU KIINI CHA DINI NI MAANDALIZI YA MAISHA YETU YA JAYO, SOTE SISI NI WAFUASI WA MITUME WETU NA MANABII, ILA HATUJUI DEGREE NA MASTERS ZAO WALIZIPATIA VYUO VIPI.

MAMILIONI TUNAWAFUATA MITUME WETU HAWA TUKIAMINI MAFUNDISHO YAO BILA KUJALI ELIMU ZAO.

NAJUA HUTAPENDA KUIFANANISHA ELIMU YAKO NA YA YESU KRISTO WALA PENGINE HUJAFIKIRIA KUIFANANISHA.

NINACHO JARIBU KUSEMA HAPA HUENDA UNGEPENDA NI SEME WAKRISTO MMESOMA TENA SANA NA WAISLAMU NI MAMBUMBUMBU KABISA ILA INASAIDIA NINI?

KUMBUKA KUNA VITU VINGINE ZAIDI YA ELIMU VINAWEZA KULETWA NA KUPAMBANISHWA NA HUENDA IKAWA ZAMU YAKO KUWA MNYONGE.

RUDI KWENYE HOJA NI JUU YA UTEUZI WA NAFASI MBALI MBALI ZINAZOFANYWA NA MHESHIMIWA RAISI, UNGEWEZA KUJIBU VIZURI BILA KUUONA UMBUMBUMBU WA WAISLAM.

TUACHE LUGHA ZA CHUKI NA ZA UDINI NAMNA HII, MAANA HAZINA FAIDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU.

SAMAHANI NDUGU MSOMI SANA SANA SANA MWENYE ALIMU ILIYO TUKUKA.
NI MIMI MWANA MADRASA.
 
Yeyote akipata nafasi ya uongozi bila kujali dini yake anatufaa kama akiwa mwadilifu. Akiwa mwislam wakristo hatutapungukiwa na kitu! Pia akiwa mkristo waislamu hawatapungukiwa na kitu!
Mkristo akilalamika kuwa nafasi za uongozi wamepewa waislamu maana yake ni kuwa: 1. Alikuwa anatarajia upendeleo kama kiongozi angekuwa mkristo 2. Ana wasi wasi kiongozi akiwa mwislamu.
atawapendelea waislamu.
Hali kadhalika mwislamu akilalamika kuwa nafasi za uongozi wamepewa wakristo maana yake ni ile ile kuwa 1. Alikuwa anatarajia upendeleo kama kiongozi angekuwa mwislamu 2. Ana wasi wasi kuwa kiongozi akiwa mkristo atawapendelea wakristo.
Katika jamii yetu ya watanzania wote tutakubaliana kuwa waislamu ndio wanaongoza kwa kulalamika kwa hiyo ndiyo wanaoongoza kwa kutarajia upendeleo toka kwa waislamu wenzao! Wakristo hawana hulka ya kulalamika maana wanamwamini sana Mungu wao kuwa atawatetea katika hali zote! Vinginevyo malalamiko ya wakristo huko Tanzania visiwani yangetisha! Huko Zanzibar viongozi wote ni waislamu! Hivi huku bara ikitokea viongozi wote ni wakristo kutakalika kweli kama kunavyokalika Zanzibar?
Fanyeni kazi, someni! achaneni na ndoto za mbeleko kama ile mbeleko ya Uda huko fssn!
 
Na siyo vyeti fake tuh

Hata watumishi hewa waliojazana humo maofisini ni hawa hawa wagalatia wanaojiita wasomi

Taifa limeingia kwenye hasara ya kulipa mabillion sababu ya hawa hawa makatonta
Naikumbuka hii thread yako. Hivi sasa napitia list ya vyeti feki nimegundua kitu! Wagalatia wamewapiga sana wenzao!
 
mleta mada Acha upuuzi wako mbona asilimia 99 ya wenye vyeti feki ni hao wa dini yako!! ww hujitambui kabisa hata huyo khalifa Khamisi ana afadhali kuliko wewe!! Udini hauwafikishi popote
 
Nauliza

Kama nikweli kuwa akiwa Raisi Mkristo anateua Wakristo wengi katika nafasi za kazi za teuzi

Anapokuwa Raisi Mwislamu kama, Alhaj Alli Hassan Mwinyi au Jakaya Kikwete
Je nao waliwateua Waislamu wengi kwenye teuzi zao ?

Kama ndivyo basi kusiwe na lawama kwani kila awamu inateua maofisa wengi wenye dini moja na Raisi

Kama Maraisi Waislamu nao wanateua Wakristo wengi, basi kigezo cha taaluma kinatumika, na asilaumiwe Raisi au Wakristo au Waislamu kwani ni jambo la kimfumo.

Kama kila Raisi anateuwa maafisa wengi kutoka kwenye dini yake basi hakuna haja ya kulalamika, kwani kila awamu, watu wa dini flani wanapata upendeleo.

Sasa kwanini kuna malalamiko?
 
mleta mada Acha upuuzi wako mbona asilimia 99 ya wenye vyeti feki ni hao wa dini yako!! ww hujitambui kabisa hata huyo khalifa Khamisi ana afadhali kuliko wewe!! Udini hauwafikishi popote
Siyo kweli! Lakini pia katika jamii yetu yenye mwingiliano mkubwa, huwezi kujua dini ya mtu kwa kigezo cha jina! Jina halitambulishi dini ya mtu! Jina linatambulisha ukoo wa mtu tu! Nina ndugu zangu ni wakristo lakini wana majina yanayotumiwa zaidi na waislam! Ninao pia wenye majina rasmi ya kikristo lakini ni waislam!
 
Back
Top Bottom