Mawenzi
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 1,251
- 345
Wana JF,
Hebu tuongelee kidogo kuhusu hawa vijana wanaochipukia ktk utajiri/umaarufu, typical example: Sharobaro.
Hawa vijana (wake kwa waume) kwa kweli wanahitaji watu wa kuwa kama parents/guardians/mentors/counsellors/advisors ili utajiri na umaarufu usiwaangamize mapema. Wengi wao wanakuwa na elimu ndogo sana na pia hutoka kwenye familia maskini. Kwa hiyo utajiri/umaarufu wa ujanani unawazuzua sana kiasi kwamba tabia zao zinakuwa hatarishi sana kwao.
Wakipata vijisenti haraka haraka na wakajua kiingereza cha "English Course" basi wanajiona wamemaliza kila kitu!! Wanaparamia na kubadilisha kila kukicha wamama, wanajiremba kupindukia, wanaanza kununua magari ya bei mbaya kabla hata ya kuwa na kibanda!! Na wanapenda kuendesha magari wenyewe tena kwa mbwembwe nyingi ili watu wawaone kuwa wanajua ku-drive! Hawataki kuajiri madereva!!
Wanakuwa na watu wanaowaita Meneja. Lkn hawa watu inaelekea kazi zao ni kuwasifia, kuwaandalia maonyesho, kuwatongozea, n.k., lakini siyo kuwakanya kwani wanaogopa kuwaudhi na kukosa umeneja!
Kwa mfano Sharobaro: Inaelekea katoka katika family maskini maana ameishia la saba tu. Hakukuwa na mtu kumwendeleza. Kwa bahati nzuri akaja Dar na kipaji chake kikamwokoa. Lkn bahati mbaya inaelekea alikosa mtu/watu wa ku-monitor tabia yake. Akawa anaishi peke yake. Akawa anafanya apendalo. Mfano mzuri wa hili ni ule uamzi wake wa ghafla kuanza safari ya Tanga saa 11 jioni akiwa peke yake huku akiwa na Sh. 6 million!! Drving kwenye highway, tena usiku, kunahitaji professional drivers, of which he was not!! Kwa nini hakuomba msaada wa kusindikizwa na mmoja wa marafiki zake??
Hatujui, au sijui, huenda pia alikuwa na kiroba kwenye gari!! Ila linalojulikana ni kuwa alikuwa anatuma na kupokea sms!! Na pia lililo wazi ni kwamba hakufunga mkanda!!
Sharo alikuwa anajitahidi kuishi kama jina lake lilivyo!
Tatizo lilopo ni kwamba ukitaka kujitolea kwa nia njema kabisa kuwa kama parent/guardian/mentor/counsellor/advisor watu watasema huyu jamaa anataka kumuibia hela kijana wa watu!!
Duh! Sasa nini kifanyike ili kuokoa hawa vijana talented? Ikumbukwe kwamba Diamond naye alipata ajali hivi karibuni!!
Nawasilisha!