Shangilia ya Wabunge haina tofauti na Wanafunzi wanaoshangilia Mtihani ulioonekana mwepesi halafu...

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Ukiona Wanafunzi wametoka chumba cha Mtihani halafu wanashangilia kuwa ulikuwa mwepesi jua ya kwamba matokeo yakitoka wengi wao huwa Wanafeli tena vibaya mno hadi huja kushangaa.

Tukio hili naona halina tofauti na Wabunge wa JMT ambao jana wengi wao niliona wakifurahia sana uwasilishwaji wa Bajeti pendekezwa kwa 2017 / 2018 ambayo hata hivyo bado haijadiliwa na utekelezwaji wake haujulikani.

Kwa Wataalam wa Saikolojia ile shangilia ya jana ya muda wote inatupa mno mashaka na si dalili nzuri / njema japo kiusomaji wake inaonekana / imeonekana ni nzuri.

Yangu macho!
 
Kweli, wabunge wameshangilia sana bajeti, haijawahi kutokea. Lakini je, hizo pesa zitatoka au zitakuwa kama za bajeti iliyopita zilipopatikana asilimia 37 tu?

Halafu, eti pato la Mtanzania limepanda mpaka zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mwaka kwa kila mtu. Watu maelfu hawana ajira, biashara nyingi zimefungwa, ukame uliathiri mamilioni ya wakullima mwaka jana, sasa hicho kipato kimepanda vipi? Sielewi !
 
Back
Top Bottom