Shamsa Ford asema mahari yake ni Milioni 20

Screenshot_2019-11-26-12-45-10.png

Huyu kalipiwa laki 8 tu
 
Mlioko karibu nae akifikia laki 1 mnishtue
View attachment 1262973
Muigizaji wa Filamu Tanzania Shamsa Ford

Muigizaji wa Filamu Tanzania Shamsa Ford, amesema kutokana na uzuri alionao, anaamini mwanaume anayetaka kumuoa kwa sasa anapaswa kutoa mahari ya shilingi Milioni 20.

Shamsa Ford ametoa kauli hiyo katika kipindi cha KIKAANGONI, kinachorushwa kila siku ya Jumatano katika kurasa za Facebook na YouTube za East Africa TV, ambapo amesema kwa mwanaume anayetaka kumuoa aende na gari lililoandikwa 'Will You Marry Me'.

Shamsa Ford amesema kuwa "mtu akitaka kunioa sasa hivi, naangalia kwanza mfuko wake ukoja ila ninachotaka mimi siku ya kwanza kuja kunipa ombi la kunioa aje na gari lililoandikwa Will You Marry Me,"

"Unajua mimi ni ninastahili mahari zaidi ya Milioni 10 au Milioni 20 kwa sababu mimi ni mzuri, na mtu akinipata mimi maana yake amepata mtu mwenye vigezo vya kuwa mke bora, najua kupika najua kulea familia." amesema Shamsa Ford.

Aidha katika kipindi hicho Shamsa Ford, amesema hakumbuki chochote kwa aliyekuwa mume wake Chid Mapenzi wakati wakiwa kwenye mahusiano, bali anayemkumbuka ni Msanii Ney wa Mitego ambaye alikuwa na tabia ya kununa kwenye mahusiano.

Chanzo: EATV
 
Shamsa Ford ni bint mzuri sana, tangu kakiwa kanakua kalionekana atakuja kuwa mwanamke bora sana, mpaka alipomaliza shule yake nchini Uganda bado alikua ni msichana mzuri tu.

Hayo ya mahari nina uhakika kuwa anatania tu ili kunigesha mahusiano.

Sina shida na huyu msichana, kilichomsababishia yote ni mazingira aliyokutana nayo mara tu baada ya shule yake. Mimi ninaamini kabisa hata sasa Shamsa Ford hajabadilika bado ndani yake ana ubora uleule ila ulimwengu wa kisanii ndiyo unaomharibia.
Ikitokea Shamsa Ford amebadili au amebadilishiwa mazingira binafsi naamini atakua mwanamke bora kabisa na wala si mbishi wa kubadilika ila bahati mbaya safari yake ya kimaisha humkutanisha na 'wale wale'
inaonekana unamjua kwa muda mrefu
 
Back
Top Bottom