Shambulio la Lissu kupigwa risasi: Polepole aibua mapya

Shambulio la Lissu kupigwa risasi: Polepole aibua mapya

polepole.jpg

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenenzi, Humphrey Polepole amefunguka na kuhoji kuhusu kitendo cha CHADEMA kumficha dereva aliyeshuhudia tukio zima la shambulio la risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na amewataka wananchi wa jimbo la Siha kumhoji Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aeleze sababu za kufanya hivyo.

Ametaka kuhoji siri iliyopo inayowafanya CHADEMA wamfiche dereva huyo wakati anahitajika kuisaidia Serikali kufumbua ukweli na kumjua aliyehusika katika shambulio hilo.

Hivi huyu polepole yupo timamu kweli? Akipatikana dereva wa lissu hao watu wasiojulikana watapatikana baada ya kuhojiwa? Vipi dereva wa Lissu angekufa katika shambulio lile ina maana intelijensia ya jeshi la polisi ingekuwa nayo imekwisha?

Siasa za CCM kupitia huyu jamaa ni mufilisi kabisa.
Jibu hoja, kwanini wamfiche?
 
Kwani Askari wa FFU waliokuwa lindoni Area D siku ya tukio, wakaruhusu gari litoke la washambuliaji litoke getini licha ya kusikia milio ya risasi nyingi wamehijwa?

Kwani rekodi CCTV camera zilizoko kwenye jengo hilo zimeshapelekwa polisi kwa uchunguzi?
Hilo si jibu, kwanini wanamficha? Kunani?
 
Hilo si jibu, kwanini wanamficha? Kunani?
Kwani hawajui yuko wapi? Nani kawazuia kumtafuta?

Kwani uchunguzi wote unamhusu dreva tu? Huo uchunguzi mwingine unakwamishwa na nini?

Kwanini mnapanick mkiulizwa kuhusu walinzi wa FFU area D?

Kwa nini picha za video za ulinzi hazionekani ni muhimu? Kunani?
 
Hivi ukiwa dreva, na gari yenye vioo tinted uliyomo ndani inashambuliwa kwa risasi 30 na ushee, wewe dereva si muhanga wa mashambulizi hayo pia? Sielewi hapo.
 
Pole pole bwana, unakuwa kama huwajui Chadema? walificha Mkanda wa video wa mauaji ya Arusha toka mwaka ule mpaka leo haujapatikana, unatazamia wamlete hadharani Shahidi namba moja dereva wa Tundu Lissu? Hizi ndio zao we endelea na mambo yako.
 
hizi hadithi za tundu lissu zishapitwa na wakati sasa ni usanii mtupu uliofanyika
 
polepole.jpg

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenenzi, Humphrey Polepole amefunguka na kuhoji kuhusu kitendo cha CHADEMA kumficha dereva aliyeshuhudia tukio zima la shambulio la risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na amewataka wananchi wa jimbo la Siha kumhoji Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aeleze sababu za kufanya hivyo.

Ametaka kuhoji siri iliyopo inayowafanya CHADEMA wamfiche dereva huyo wakati anahitajika kuisaidia Serikali kufumbua ukweli na kumjua aliyehusika katika shambulio hilo.

Hivi huyu polepole yupo timamu kweli? Akipatikana dereva wa lissu hao watu wasiojulikana watapatikana baada ya kuhojiwa? Vipi dereva wa Lissu angekufa katika shambulio lile ina maana intelijensia ya jeshi la polisi ingekuwa nayo imekwisha?

Siasa za CCM kupitia huyu jamaa ni mufilisi kabisa.
Hapana mkuu. Huyu dereva ni shahidi muhimu sana katika hii kesi. Kama angekufa hilo ni jambo lingine lakini kwa sasa dereva yuko hai.

Huwezi kuvunjiwa nyumba yako na kuibiwa mali yako wakati unawaona majambazi halafu polisi wanapotaka kukuhoji useme:
"Kwa nini mnataka kunihoji? Kama yale majambazi yangeniua mngeendeleaje na uchunguzi wenu." Hii haina mantiki hata kidogo.

Sijui kwa nini Polisi nao wanaburuza miguu yao. Huyu dereva ni shahidi muhimu sana. Kama CDM wanaleta chenga ni kiasi cha kupata oda ya mahakama kumlazimisha Mbowe amlete dereva sentro. Asipofanya hivyo hayo yatakuwa makosa mawili:
[emoji830]Obstruction of justice.
[emoji830]Contempt of court.

Hapo ni lupango tu msobe msobe.

Kwa nini CDM wanafanya mchezo huu katika kosa baya la jinai kama hili?
 
Kwahiyo mpk mlinzi akamatwe ndio aletwe dereva? Kwani akihojiwa dereva ya walinzi kuna tatizo gani?

Tatizo letu watanzania hatujui haki zetu hivyo hatuwezi kulinda haki za wengine.Mtu wa kwanza kutakiwa kuhojiwa ni Mlinzi aliyekuwa LINDONI na si vinginevyo,leo mlinzi yuko huru halafu unamtafuta DEREVA aliyenusurika kifo,upumbavu huu
 
Rita Warobi, mara tu umesahau kuwa shambulio la Mh Lissu, ndilo linetumika kama kete ya kisiasa katika Kampeni za CHADEMA, wakati wote, na bado kikambulia sifuri (0) katika marudio ya udiwani kata 43! Kwako leo unaona ni kosa la kisiasa CCM kujibu hoja hiyo!

Hivyo siyo sahihi kuwasemea wanaSIHA kana kwamba wao ni mbumbu kulishwa matango ya kisiasa.
Ule uchaguzi mitutu ya bunduki ikatumika ili mpore matokeo na kujitangaza washindi kwa nguvu?! hivi ule nao ni uchaguzi wa kujisifia hadharani eti mlishinda?!! spare me the laughter please.. lol
 
Tatizo letu watanzania hatujui haki zetu hivyo hatuwezi kulinda haki za wengine.Mtu wa kwanza kutakiwa kuhojiwa ni Mlinzi aliyekuwa LINDONI na si vinginevyo,leo mlinzi yuko huru halafu unamtafuta DEREVA aliyenusurika kifo,upumbavu huu
Kwahiyo dereva anazuiwa kwa sababu mlinzi hajahojiwa?
 
Kwahiyo dereva anazuiwa kwa sababu mlinzi hajahojiwa?

Hope umenielewa,kwenye tuhuma zozote za Mauaji au Ujambazi mtuhumiwa number moja ni Mlinzi anayekuwepo kwenye Lindo Period.Mengine jifunze kujua haki zako ili uje kutetea wengine
 
Hope umenielewa,kwenye tuhuma zozote za Mauaji au Ujambazi mtuhumiwa number moja ni Mlinzi anayekuwepo kwenye Lindo Period.Mengine jifunze kujua haki zako ili uje kutetea wengine
Kwahiyo kumzuia dereva ni sehemu ya kudai haki ya mlinzi kuwa mtuhumiwa namba moja? Lkn dereva sio mtuhumiwa anatakiwa kuhojiwa km ambavyo lissu atahojiwa kwa maana nyingine dereva naye ni muathirika wa tukio.
 
KAma huelewi naomba usiniquote.Mtuhumiwa wa KWANZA au NUMBER moja ni Mlinzi,na walinzi ni Polisi walioajiriwa na jeshi la Polisi.

Hivyo kam taaluma ya polisi inavyodai mtuhumiwa wa kwanza ndiyo anayetakiwa kukamatwa na kutoa maelekezo period.Hayo mengine ni siasa chafu za CCM na wapambe wake.
 
CCTV CAMERA IKO WAPI?NANI ANAHUSIKA NAKUFICHA CCTV CAMERA?wapi walinzi wa area d siku hyo?nani aliwatoa kwnye lindo?gari iliyofanya tukio nani mmiliki wake?polepole aje nahayo majibu watz cyo wajinga
Hahahahhaa.....

Lumumba nzima wakae hawajibu haya..
 
KAma huelewi naomba usiniquote.Mtuhumiwa wa KWANZA au NUMBER moja ni Mlinzi,na walinzi ni Polisi walioajiriwa na jeshi la Polisi.

Hivyo kam taaluma ya polisi inavyodai mtuhumiwa wa kwanza ndiyo anayetakiwa kukamatwa na kutoa maelekezo period.Hayo mengine ni siasa chafu za CCM na wapambe wake.
Bado hujaweka hoja wazi kwanini dereva anazuiwa kuhojiwa! Kwa sababu dereva sio mtuhumiwa mpk atakapohojiwa na kugundulika km kuna utata kwenye maelezo yake, lkn kukataa kumpeleka dereva itasaidia nini kuhakikisha haki ya kukamatwa/kuhojiwa kwa aliyekuwa lindoni inatimizwa? Na je ilishawekwa hadharani kuwa dereva anazuiwa mpk aliyekuwa lindoni ahojiwe kwanza?
 
Back
Top Bottom