Shamba la Miti ukanda wa Pwani

newmzalendo

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
1,378
550
nimepata ardhi kubwa,ninahitaji kujua shamba la Miti ukanda wa pwani linawezekana?if yes miti gani inahimili mazingira ya ukanda wa pwani [rufiji,kilwa].
nawaza miti ya under 10 years.
 
nimepata ardhi kubwa,ninahitaji kujua shamba la Miti ukanda wa pwani linawezekana?if yes miti gani inahimili mazingira ya ukanda wa pwani [rufiji,kilwa].
nawaza miti ya under 10 years.

Wengi wanaotesha mitiki, lakini nashauri usifanye hivyo. Sioni ikinenepa. Hata mie nimeotesha mitiki michache, lakini naona inakuwa kama mirunda.

Kwa nini usioteshe mikorosho kitaalamu ukawa umefanya kweli? Miti minene ya mbao siioni huko unakosema. Nimeona ndugu mmoja alijaribu kuotesha mierezi, tena mingi, lakini yote imeshindwa kunenepa. Atavuna mirunda tu.
 
Ninataka kuotesha miti isotoa matunda,kwa ajili ya kuvuna mbao,au nguzo,kwa kuwa bado nipo mazingira ya mjina nataka nioteshe vitu vinavyohitaji ukaguzi mdogo,e.g fire break, etc.
nimefikiria zao Bamboo.kwani kenya wameanzisha mashamba ya bamboo.wataalam mnasemaje?
 
Kama uangalizi utakuwa mdogo, basi nadhani usioteshe miti yenye thamani kubwa. Maana wabongo wanaiba hata miche iliyooteshwa shambani.

Sasa hizo bamboo zitakuwa bomba za maji au vipi? Kuna soko Tanzania au uko tayari kuuza Kenya?

Wataalamu wako bize kwenye Jukwaa la Siasa, ndio maana nimeona heri hata mie nikujibu kuliko wote tukae kimya kana kwamba hatuthamini swali lako.
 
Ninataka kuotesha miti isotoa matunda,kwa ajili ya kuvuna mbao,au nguzo,kwa kuwa bado nipo mazingira ya mjina nataka nioteshe vitu vinavyohitaji ukaguzi mdogo,e.g fire break, etc.
nimefikiria zao Bamboo.kwani kenya wameanzisha mashamba ya bamboo.wataalam mnasemaje?

mkuu , mimi nimewahi kufanya study ya ku promote Bamboo plant as a building material kama wanayofanya china , vietnam na sasa Costa Rica kuna miradi mikubwa sana ya ujenzi wa low cost housing kwa kutumia Bamboo material, there are more than 24 spicies of Bamboo in Tanzania, the forests and plantation are found mostly in southern highlands , the most found specie in Tanzania is Arundaria Alpina, bamboo is environmental friendly and resists earth quakes

Bamboo can be used in walls,floors, roof structure, scaffolding, rainwater gutters and rainwater haresting accessories, also can be used as reinforcement in concrete

pia kuna products nyingi sana za bamboo kama furnitures, doors,crafts, toothpicks, ice cream sticks, hospital spatulas, skewers for barbaque

ukiangalia hii utaona BAMBOO ni sector tosha ya kuingizia nchi kipato, lakini mapungufu yaliyopo ni haya

  • kwa sasa matumizi makubwa ya bamboo ni utayarishwaji wa pombe ya ulanzi
  • nchi yetu haina technology ndogo ndogo na kubwa to industrialize bamboo plant hivyo tunahitaji transfer of technology mechanism
  • bamboo zinaoza katika maeneo mengi kwama kyela na maeneo makubwa ya iringa na kilosa na kuharibika kwa kukosa wanunuzi kwa kuwa hakuna matumizi
kuna plant ambayo ni similar na bamboo inaitwa rattan, hii ni nyembamba na hutumika kusuka viti vikapu na kadhalika , nayo ni potential kubwa hapa tukiikazania kwani utengenezaji wa product zake haiitaji technology kubwa
 
ahsante sana ndugu LAT mchango wako ninauthamini sana. Nimekuwa nikifikiria mradi bamboo kwa muda sana sasa nafikiri ninepata platform ya kuongeza maarifa.JF pamoja tutaikomboa Tanzania na kurudisha hadhi yake.

Nauliza mkuu LAT je Bamboo zinaweza kushamiri ukanda wa miinuko wa pwani?eg Morogoro AHSANTENI.
 
mkuu tena sana .maeneo ya miinuko ya morogoro kule Kijiji cha mtega kilosa morogoro, bamboo inastawi sana, kwa study niliyofanya hata maeneo ya coastal highland regions bamboo inakubali kushamiri

hapa nilipo nina project ya bidhaa ya bamboo ambayo anytime will be in operation, it is a simple production process and technology transferred from china which needs very little resources

mkuu what do you intend to do? bamboo plantation or bamboo agro processing , please pm fvor more collaboration

Bamboo is a lovely plant,kuna organization inaitwa INBAR (International Network For Bamboo and Rattan) join and be a member it is very useful
 
Kwa ukanda wa pwani hasa mkoa wa Pwani kuwa na shamba la miti (teak au cederela) ni kasheshe kidogo, lakini ukienda maeneo ya Muhoro kama unakwenda Somanga kuna mitiki minene,lakini lazima ina miaka zaidi ya 20. Mitiki iko vizuri sana Tanga, Mtibwa na bonde la Kilombero. Ila naamini ukipanda eucalyptus aina ya grandis unaweza kuvuna ktk kipindi kifupi kama boriti au fito za kujengea mahotel ya ufukweni.

Kwa sasa fito nzuri za kujengea mahotel zinatoka Iringa,kila siku kuna shehena inayoshuka Dar kwa malori. Hii inaweza kukulipa mkuu. Ardhi yake isiwe kavu sana. Ardhi ya Rufiji,Mhoro mpaka Somanga inafaa kwa sababu ina maji mengi.

Mwaka jana, gazeti moja la kila siku walitangaza kuwa wanataka kuanzisha mashamba ya mianzi Tz, walikuwa ni Japan kwa kushirikiana na Sido, nikapiga kwata hadi Sido pale Nyerere Road, nikakuta jamaa hata hawajui nini kinaendelea ktk ulimwengu wa mianzi, baadae wakanionyesha sample ya mianzi inayoagizwa toka Kigoma/kusini nyanda za juu kwa ajili ya vikapu. Wakanionyesha ni fito fulani ambazo zinakunjika kirahisi.

Siku moja niliiba mianzi kama 3 hivi ktk shamba la jamaa pale Vianzi, mianzi rangi ya njano, nikakta vipande vipande nikapeleka shambani kuotesha kwa majaribio, imeota vizuri. Zaidi ya matumizi waliotoa jamaa zetu hapo juu, mianzi pia hutumika kwa kufugia samaki,hasa kama kuna fisi maji, ile hupangwa vizuri na fisi maji hawezi kupita, na samaki hupenda kula gamba lake. Kwa hiyo go for it man. Nakumbuka kulikuwa na kitu kilikuwa kinaitwa mianzi miti zamani kule Iringa.
 
mkuu tena sana .maeneo ya miinuko ya morogoro kule Kijiji cha mtega kilosa morogoro, bamboo inastawi sana, kwa study niliyofanya hata maeneo ya coastal highland regions bamboo inakubali kushamiri

hapa nilipo nina project ya bidhaa ya bamboo ambayo anytime will be in operation, it is a simple production process and technology transferred from china which needs very little resources

mkuu what do you intend to do? bamboo plantation or bamboo agro processing , please pm fvor more collaboration

Bamboo is a lovely plant,kuna organization inaitwa INBAR (International Network For Bamboo and Rattan) join and be a member it is very useful

Ndugu Kilaza,
Saidia mimi ili nijiunge na hao INBAR, kule kwetu kuna milima iko tupu naweza kuiotesha kwa wingi, hata sasa SIDO wanategemea kutoka huko.
 
hivi sasa bamboo haiitaji maji au hata sehemu kavu kama kiwangwa na Fukayosi huko bagamoyo inaweza kukubali?

nakubaliana na mtoa hoja aliyetangulia kuwa mitiki hainenepi sana ukanda wa pwani (e.g. bagamoyo bagamoyo).. mimi nimejaribu kupanda kama ekari 5 za Gmelina arborea,(white teak) huko Fukayosi. naona inakubali, ila sijajua sana kama inanenepa sana au la. ukitaka habari yake unaweza kwenda Gmelina arborea - Wikipedia, the free encyclopedia ila naona LAT anafahamu suala la species za miti unaweza kutusaidia taarifa zaidi
 
Sehemu kame jamii kubwa ya mimea hukua kwa taabu, hata huko milima ya nyanda za juu kusini iliko mingi,kuna mvua nyingi sana ndio maana mianzi inamea kama msitu. Ukienda sehemu za Bulongwa Makete kuna mapori yana mianzi tupu. Maeneo ya kiwangwa itakuwa taabu sana kuuotesha muanzi mpaka ukubali,japo unaweza kuotesha,ila utakuwa dhaifu sana. Nimejaribu mashina mawili pale Mbezi msakuzi, nako ni kukame,inakuwa kwa taabu na haiwi mirefu wala hainenepi.

Ukifika Banana njia ya kwenda Ukonga,ingia njia ya kwenda Kitunda,kona ya kwanza kushoto,kuna mtu kapanda grandis, sikufanya utafiti,zile grandis zina miaka mingapi, au ukienda Segerea seminary, kuna mitiki mingi lakini haijanenepa, ipo eucalyptus pia kama boriti. Ni msitu mzuri, kwa hiyo NM nenda kapate uzoefu Segerea seminary.
 
Asante sana,LAT,Malila kwa ushauri,nitaenda segerea kupata uzoefu,wa kupanda mikaratusi,ila swala la mianzi nimefanya tafiti nimegundua ina matumizi mengi mno,na kuwa nchi jirani imekuwa declared na UN kuwa ni semi-desert,hivyo wameamua kuondoa jangwa kwa kupanda mianzi kwa wingi.nadhani kitakachofuata ni Technology transfer from china to East AFrica.

LAT- unaweza kushare research yako kuona ninwezaje kufanikiwa ktk upandaji huu ,ni species ipi inatoa miti yenye thamani zaidi ktk kutengeneza products.nimevutiwa zaidi na hizi products toothpicks, ice cream sticks, hospital spatulas,nadhani kwa bongo zote hizo bado tuna-import
 
Ninataka kuotesha miti isotoa matunda,kwa ajili ya kuvuna mbao,au nguzo,kwa kuwa bado nipo mazingira ya mjina nataka nioteshe vitu vinavyohitaji ukaguzi mdogo,e.g fire break, etc.
nimefikiria zao Bamboo.kwani kenya wameanzisha mashamba ya bamboo.wataalam mnasemaje?
Mianzi ni mizuri kwani inavumilia lakini ungehitaji mianzi ya asili ambayo iko kama aina mbili kuna ile ya rangi ya manjano ambayo huwa mikubwa na ile ya rangi la kijani ambayo ni miembamba,mikubwa hutumika sana kutengenezea mapambo ikichanwa,tatizo ni moto inabidi ujitengenezea njia za kuepusha moto
 
  • Thanks
Reactions: tyc
Asante sana,LAT,Malila kwa ushauri,nitaenda segerea kupata uzoefu,wa kupanda mikaratusi,ila swala la mianzi nimefanya tafiti nimegundua ina matumizi mengi mno,na kuwa nchi jirani imekuwa declared na UN kuwa ni semi-desert,hivyo wameamua kuondoa jangwa kwa kupanda mianzi kwa wingi.nadhani kitakachofuata ni Technology transfer from china to East AFrica.

LAT- unaweza kushare research yako kuona ninwezaje kufanikiwa ktk upandaji huu ,ni species ipi inatoa miti yenye thamani zaidi ktk kutengeneza products.nimevutiwa zaidi na hizi products toothpicks, ice cream sticks, hospital spatulas,nadhani kwa bongo zote hizo bado tuna-import

Mkuu tatizo liko ktk kukusanya mbegu (cuttings), kwa kusaidiana tunaweza kupata haraka.
 
Safi sana kwa somo hili hapa juu. Ni vizuri ku-invest katika miradi kama hii kwa ajili ya "Pension" yako mwenyewe. Lakini kuna angalizo hapa, kuwa makini katika kutwaa ardhi hiyo kwani kuna mzee mmoja alienda B'moyo zamani na kukununua pori zaidi ya eka 10, akapanda mazao mbali mbali lakini minazi ndo mingi. Sasa eneo lake limevamiwa na watu waliojikusanya na kugawiana kuwa ni lao. Ujio wa vyama vingi na wanasiasa uchwara wanaotafuta cheap popularity wamemliza mzee wa watu ingawa kesi ipo mahakamani. Yeye awezi vuna mazao yake kwani korti imetoa amri status ikae kama walivyokuwa siku ya amri ile. Hivyo wavamizi wanaendelea kuvuna
 
malila si tunaweza kupanda kule mkuranga mipaka ya mashamba, ukizingatia kuna maji maji?
keep in touch

Naam,
Lile bonde nalipiga mianzi lote, nimefanya majaribio ya kuotesha kwa kutumia cuttings ziko safi. Nitakuonyesha sehemu yenye mbegu za njano, ni za kujichotea tani yako. Ziko kule Yavayava, sio zile za pale njiani kwa Wakorea, ziko pale Sangatini, hazina mwenyewe.
 
Du! Yaan mzee wawatu wamempora shamba lake!!? inauma sana mtu kula jasho la mwingine bila ridhaa yake. Waheshimiwa Salut wote, keep going!, uchumi tuunyooshe.
 
malila

take it from from me, i will soon start production of bamboo skewers (mishikaki sticks) , so i will be your customer if you have bamboo harvests
 
malila

take it from from me, i will soon start production of bamboo skewers (mishikaki sticks) , so i will be your customer if you have bamboo harvests

Umeniambia kitu kizuri sana, nakwenda kununua mianzi yote (ile ya njano) kule Mkuranga na utakapo nishitua tu nakwenda navuna. Asante kwa hilo.
 
Back
Top Bottom