Shaka: Pamoja na Ukame unaondelea nchini ambao haujasababishwa na CCM wala Chama chochote Rais Samia anatekeleza miradi ya maji 1,194 kuukabili

CM 1774858

JF-Expert Member
May 29, 2021
4,986
4,083

SHAKA HAMDU SHAKA ASEMA NI HAKIKA WATANZANIA WATAMPA RAIS SAMIA TUZO YA HESHIMA MWAKA 2025 KWANI ATAPATA KURA ZA MAFURIKO
===
Ampongeza kwa namna anavyochapa kazi bila mbwembwe wala zogo

Asisitiza Chama kuridhishwa na juhudi hizo kwani matokeo yanaonekana

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan, Watanzania watampa tuzo iliyotukuka na ya heshima mwaka 2025.

Amesema Rais Samia meonyesha uungwana wa hali ya juu kwa kuendelea kuchapa kazi yenye tija na kuleta matokeo mazuri ikiwemo kutekeleza miradi ya maji yenye lengo la kupunguza na kuondoa changamoto ya upatikanaji wake katika maeneo mbalimbali nchini.

Shaka ameyasema hayo leo Novemba 11, 2022 wakati akizindua mradi maji wa Kimbiji uliopo Kigamboni Dar es Salaam na kukabidhi mitambo ya kutafuta na kuchimba visima virefu vya maji na kukabidhi eneo la uchimbaji bwwa la Kidunda kwa mkandarasi atakayetekeleza mradi huo.

"Kwa heshima unayoileta Watanzania watakupa tuzo iliyotukuka na ya heshima mwaka 2025.

"Mheshimiwa Rais Samia hongera sana kwa mzigo huu unaochapa yuko mshairi alisema na yuko mshairi alitunga tungo 'ada ya mja ni kunena' akimaanisha kwamba kawaida ya binadamu ni kusema 'muungwana ni vitendo na kila aliyemuungwana atatenda. Mheshimiwa Rais wewe ni muungwana wa taifa hongera sana.

"Akamalizia (mshairi) kusema tenda watu wataona majigambo weka kando. Mheshimiwa Rais unatenda, huna zogo, huna mbwembwe unawaletea maendeleo wananchi vijana wa mjini wanasema unakimbiza kimyakimya," amesema.

Amesema pamoja na ukame uliopo kwa sasa ambao umesababisha upungufu wa maji katika maeneo mbalimbali serikali inafanya kazi nzuri na kwamba Chama kuanzia kamati za siasa za wilaya, mikoa, sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa na wajumbe wa Halmashauri Kuu, wametembelea na kujiridhisha kuna miradi ya maji 1,194, hivyo nchi nzima inaguswa na utekelezaji huo.

===
 
Wale vijana wa Upinzani wao wanachukua Ukame kama Agenda yao kesho mvua ikinyesha yakatokea MAFURIKO wanapata tena Agenda mpya,

Watu hata Ofisi hawana wanataka tuwaamini ili watujengee Sisi Ofisi za Serikali kweli??!
 
Kwenye hii mabalaa yote yanasababishwa na madhambi ya CHADEMA mnaficha nini,

Tuacheni maasi mvua zinyeshe
IMG-20221105-WA0121.jpg
 
Wale vijana wa Upinzani wao wanachukua Ukame kama Agenda yao kesho mvua ikinyesha yakatokea MAFURIKO wanapata tena Agenda mpya,

Watu hata Ofisi hawana wanataka tuwaamini ili watujengee Sisi Ofisi za Serikali kweli??!
We nae akili zako kama kuna funza kichwani karne ya 21 unasingizia ukame huku kunaaziwa yamejaa maji-hizo akili au matope.
 
Shaka anahitaji ushauri wa kisaikolojia. Soon ataanza kuokota chupa chakavu mitaani.

Hivi CCM iliweka lini sera ya ufugaji bora ili kuondokana na ufugaji wa kutangatanga unaoharibu mazingira?

CCM imesimamia lini sera ya mazingira kikamilifu? Wao wanalinda vyanzo vya maji kama wanavyolinda vyanzo vya HAZINA ili wanufaike. Hawana mikakati endelevu wala nia ya dhati ya kuyakabili mabadilko ya tabianchi

Uwepo wa CCM madarakani kinyume na katiba ni laana kwa nchi. Mwenye laana hajitambui lakini utayaona matendo yake laanifu. Ndivyo CCM ilivyo.

Kukosekana kwa mvua ni matokeo ya laana iliyo juu ya nchi. Laana hiyo ni CCM
 
Back
Top Bottom