Shaka: Mitandao ya Jamii zikiwemo blogs zipigwe marufuku!!

Shaka: Mitandao ya Jamii zikiwemo blogs zipigwe marufuku!!

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
13,219
Reaction score
20,570
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Bw. Shaka amewataka wabunge wa baraza la wawakilishi wapeleke hoja ya dharula katika baraza ya kupiga marufuku mitandao ya kijamii na blogs zote kwa sababu ya kuhatarisha usalama wa taifa na kufanya uchochezi!!


Source: Star TV habari adhuhuri.

Je wana - JF hii siyo mbinu ya kudidimiza uhuru wa kutoa maoni na kugandamiza demokrasia nchini?!
 
Nadhani njia sahihi hapo ni kufungia ile tu inayokwenda kinyume.
 
huyu nae nini???Pinda alishasema Zanzibar sio nchi so apige kimya tu tunawasikiliza wenye nchi (Bara) ambao hata JF wameishindwa, wapi Mchungaji Lwakatare
 
Mimi sishangazwi na alichokisema kwa sababu ni wale wale viongozi butu na walio na fikra mgando wa chama chakavu na wezi nyinyiemu!!asamehewe tu bure.
 
Napata SHAKA Sana kama huyu jamaa anajua kama hii ni 2015. Vijana wa CCM ni waoga Sana kwenye demokrasia na Uhuru wa kutoa maneno. Eti CCM inategemea vijana na kama hawa wapenda pombe na ngono na walevi wa madaraka wawe viongozi wa baadae. Kama Field Marshal John Okello angekuwa mwoga hivi hadi Leo Sultani angekuwepo Zanzibar, nani angeongoza mapinduzi?
 
Hivi kuna anayetegemea kupata mawazo bora kutoka kwa kakundi hako kanako jiita UVCCM?
 
Wanataka kuwafunga kufuli midomoni mbaki mnahutubiwa tu!!!!
 
Back
Top Bottom