Shaka Hamdu Shaka azungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
108
NUKUU: BAADHI YA NUKUU ZA KATIBU WA NEC ITIKADI NA UENEZI WA CCM, SHAKA HAMDU SHAKA ALIPOKUA ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO 12 OCTOBA 2021 DODOMA

"Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kusimamia na kuimarisha haki za binadamu, usawa, demokrasia, kupinga aina zote za ubaguzi pamoja na kupiga vita ubadhirifu"

"Chama cha Mapinduzi kinakipongeza ACT Wazalendo kwa kushinda katika jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni mkoani Kaskazini Pemba na hiyo ndio siasa safi"

"Kumalizika kwa chaguzi hizi ndogo za udiwani na ubunge majimbo ya Konde na Ushetu kwetu kumetupa funzo kwa wenzetu katika uso wa demokrasia"

"Katika kujenga na kukuza uchumi serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia uwekezaji"

"Chama cha Mapinduzi kinaendelea kuwaomba na kuwahamasisha wananchi wote kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan, Rais ambaye ana dhamira njema ya kutaka kutufikisha kule tunakotaka na kudumisha huduma za msingi za jamii ikiwemo afya, maji, elimu"

"Chama cha Mapinduzi kinatoa wito kwa wanachama na kamati za siasa za ngazi zote kuhakikisha kwamba wanafuatilia kwa karibu sana utekelezaji wa mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19 kuhakikisha hakuna fedha zinaliwa"

"Fedha za mradi wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19 sadaka bali zimekuja kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania. Fedha zimekuja kwa ajili ya kuwaletea maendeleo ya Watanzania na kuhakikisha uchumi wa mtu mmoja mmoja unainuka"

"Chama cha Mapinduzi ni chama kikubwa katika mambo ambayo CCM iko nayo makini ni mambo ambayo yanayobeba maslahi mapana ya CCM na ndio sababu inaendelea kusalia madarakani. Kwa yeyote ambaye aliyekwenda kinyume na taratibu, taratibu zake zipo na zitafuatwa"

"CCM ndio inaunda dola na kupewa dhamana ya uongozi, tumekuwa tukipita na kuangalia miradi na kusema hapa tumeridhika na hapa hatujaridhika na kutaka hatua zichukuliwe, tunafanya hivyo kwa kuwa sisi ndio tumebeba dhamana na maslahi ya serikali"​

JamiiForums-1727968917.jpg
 
Shaka hajawahi kuniangusha katika kulinda na kutetea na kulinda umoja, amani na Utulivu wa nchi yetu,

ACT Wazalendo na wenzao watambue Kuwa demokrasia sio mpaka wao washinde,

Mungu ambariki sana Mhe Shaka na viongozi wengine wote wa CCM,

KAZIIENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
Angeacha tu kuharibu pesa zachama kuongea na wanahabari,maana hata akiongea hamuna mtu wa kumsikiliza,Labda wanaokula mezani mwa Hangaya.
 
Huyu hafai hata kuitwa msanii. Ni demokrasia ipi na haki zipi anazozilinda Samia na CCM?

Kubbikia watu kesi na kuzuia mikutano ya vyama vya kisiasa iliyoidhinishwa na katiba?? Huyu shaka kuna mashaka makubwa kama kichwani kupo sawa.

Angekuwa ndani ya kichwa chake ana angalao ya kiwango cha ukubwa wa mbegu ya haladali, angenyamaza tu.
 
Taarifa ambazo zinapaswa kutolewa na wizara ya fedha na wizara ya afya zinatolewa na kiongozi wa chama cha siasa. Inamaana mipango ya nchi inapangwa Lumumba wanavyotaka wao, wataalamu waliopo kwenye mawizara wao ni ketekeleza tu maagizo.
 
Chama ndio serikali mkuu ila serikali sio chama
 
Hamia CCM
Huyu hafai hata kuitwa msanii. Ni demokrasia ipi na haki zipi anazozilinda Samia na CCM?

Kubbikia watu kesi na kuzuia mikutano ya vyama vya kisiasa iliyoidhinishwa na katiba?? Huyu shaka kuna mashaka makubwa kama kichwani kupo sawa.

Angekuwa ndani ya kichwa chake ana angalao ya kiwango cha ukubwa wa mbegu ya haladali, angenyamaza tu.
shida iko wapi?
 
Shaka hajawahi kuniangusha katika kulinda na kutetea na kulinda umoja, amani na Utulivu wa nchi yetu,

ACT Wazalendo na wenzao watambue Kuwa demokrasia sio mpaka wao washinde,

Mungu ambariki sana Mhe Shaka na viongozi wengine wote wa CCM,

KAZIIENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
Huyu shaka tuliambiwa na mwendazake ni mla rushwa
 
Shaka hajawahi kuniangusha katika kulinda na kutetea na kulinda umoja, amani na Utulivu wa nchi yetu,

ACT Wazalendo na wenzao watambue Kuwa demokrasia sio mpaka wao washinde,

Mungu ambariki sana Mhe Shaka na viongozi wengine wote wa CCM,

KAZIIENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
Hio sentensi ya pili nakubaliana nayo, ila naona shida kidogo. Mmezuia mikutano ya wapinzani, mnatarajia sera zao watanadi wapi? CCM wako huru kuzunguka nchi nzima na kufanya mikutano ila wapinzani wamezuiwa. Huu sio uwanja sawa wa kufanya siasa. Acha sera zishindanishwe, wananchi waamue.
 
Back
Top Bottom