Shairi: Nyege ni kunyegezana by Andanenga

Yes Poetic licence BASATA ndio wanatoa!
hapana!
BASATA hawatoi poetic licence!
hata kwanza nawashangaa wanavodhalilisha taaluma yao!
Poetic devices ni uhuru wa msanii kutumia lugha/ sanaa bila kufungwa na kanuni na misingi ya lugha husika!
 



Nyege kitu asili, anazo na nyungunyungu
Nyege si za akili, katazo ni la mzungu
Nyege zi maadili, hamnazo kwa uvungu
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama

Nyege bila kuwepo, singekuwepo uzao
Nyege na yake michepo, zadumu kila uchao
Nyege zi na kicheko, na damu pata ugawo
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama

Babio na mamio, wametokana na nyege
Umbulo na amiyo, hawakujengwa kwa zege
Vipi uzungu salio, kututenga degedege?
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama

Nyege kunyegezana, kwa wema tukafanana
Twende kugezeana, sema hatutabanana
Vipi leo tunakwama, asili kuhamahama?
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama

Andanenga kaanzisha, mimi kuja kumaliza
Nyege nimeidhinisha, ukipata kumaa liza
Si jambo la kirihisha, ukidata unafiza
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama

Kalamu naweka chini, nimefika kaditama
Vijijini na mijini, tujitwike baba mama
Kazi yataka makini, uzazi dawamu kama
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama


Kiranga sende mrama, kaditama sio kiama ,
Kienda si mwanae kwenda, kienda rudi tuanze sema ,
Nani matusi kasema, nayasaka nitoe lana ,
Raha ya nyege nyegeni, shairi lake uhuru .

Utusi u kamusini, kwani yalowekwa na nani ?
Ninayo I kamusini , hilo katazo la nini ?
Si wanayo shubakani, hawalioni kwa nini ?
Raha ya nyege nyegeni, shairi lake uhuru .

Tulikwenda na shuleni, tukakariri vichwani ,
Mwanagenzi yu huruni, kukunja viriga tungoni ,
Haya kwetu ni mageni, sizo kunga shairini ,
Raha ya nyege nyegeni, shairi lake uhuru .

Andanenga na Mloka, sifazo kwao hakika ,
Walitunga yakatundika, na Shabani msifika ,
Wote nao na Soyinka, walijua kuandika ,
Raha ya nyege nyegeni , sheria zilianza lini ????
 
hapana!
BASATA hawatoi poetic licence!
hata kwanza nawashangaa wanavodhalilisha taaluma yao!
Poetic devices ni uhuru wa msanii kutumia lugha/ sanaa bila kufungwa na kanuni na misingi ya lugha husika!
Ha ha ha joking! Poetic licence is like I say the bus growled uphill instead of simply bus went uphill.The player who scored was completely unmarked he was free as a molecule.
 
Kiranga sende mrama, kaditama sio kiama ,
Kienda si mwanae kwenda, kienda rudi tuanze sema ,
Nani matusi kasema, nayasaka nitoe lana ,
Raha ya nyege nyegeni, shairi lake uhuru .

Utusi u kamusini, kwani yalowekwa na nani ?
Ninayo I kamusini , hilo katazo la nini ?
Si wanayo shubakani, hawalioni kwa nini ?
Raha ya nyege nyegeni, shairi lake uhuru .

Tulikwenda na shuleni, tukakariri vichwani ,
Mwanagenzi yu huruni, kukunja viriga tungoni ,
Haya kwetu ni mageni, sizo kunga shairini ,
Raha ya nyege nyegeni, shairi lake uhuru .

Andanenga na Mloka, sifazo kwao hakika ,
Walitunga yakatundika, na Shabani msifika ,
Wote nao na Soyinka, walijua kuandika ,
Raha ya nyege nyegeni , sheria zilianza lini ????

Vitabu viliandika, vuguvugu hatakiwi
Hata peponi kufika, tiketiye hapatiwi
Vipi kufumba hakika, cheusi cheupe Kiwi
Tungo vina na mizani, vingine wenda kizani

Tungo vina na mizani, vingine wenda kizani
Utatupiga tufani, kutufunga gerezani
Tuachia tafrani, tukosekane nyumbani
Ya kivinje hutaghani, kutupaya Mikindani

Chaguzi ni kuchagua, kwa hakika kwa agua
Sifanye kujibutua, kwa tungo zenye kujua
Vipi kwenda kwa kujivua, sanaa kuiumbua?
Kwafagio kubagua, kwa majilisi vumbua

Nyege ni kunyegezana, si tungo ya lelemama
Upitie karakana, si vungo la maulana
Vipi tungo kwama kwama, kwa rula hazilalana?
Tungo za malenga wana, hazikeshi za mchana

Tungo huru nazijua, kiziona natambua
Zenda zarudi bamvua, kwa urefu ka mashua
Haiku nazo chagua, sheria zake pasua
Vipi waruka kagua, upande unapotua?

Kaditama nachutama, kata niletee maji
Shairi mithili kama, la malenga wajuaji
Silete rai za chama, za kwenda kama Bajaji
Tungo tunga za maana, wakusikize wazazi
 
Naliweka hapa hilo Shairi:

Peni yangu Andanenga, uwino unapotona,
Mantiki huzilenga, na balagha na bayana
,Hufaidika malenga, huvurugika akina
,Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.Msemo wa Kiswahili, nyege ni kunyegezana
,Maana yaki kamili, wema ni kutendeana,
Wasiojua fasili, hunamba nimetukana
,Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.


Ni msemo maarufu, ambao shaka hauna
,Kwenye kamusi sanifu, funueni mtaona
,Niwezeje kukashifu, nami mwana muungwana!
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.


Ninataja ukurasa, wazi hapa naunena,
Soma mbili moja tisa, soma bila ya fitina,
Msemo siyo wa sasa, si juzi licha wa jana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.


Ushairi kubwa fani, mithili yake haina,
Kujua zake bayani, yataka kikubwa kina
Muoneni mwafulani, hata kuku wamguna,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.Ulipotamkwa mlo, kaja akitunatuna,
Akakabwa koromelo, akabaki kugunaguna,
Kabakia lolololo, uzamani umechina
,Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.Alhaji Jitukali, pokea pongezi tena
,Kikubwa chako kilili, hapandi yule mtwana,
Atuache tule wali, yeye ugali wa dona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Kaditama wa Busara, na Mbwezi heko kijana
,Pongezi ndugu Kagera, Yobu has ante sana,
Ndimi Mshairi Bora, kipofu ninaeona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.(Mshairi Bora)Amiri A. S. Andanenga (Sauti ya Kiza)SLP 4775,Kinondoni ShambaDar es salaam.

KWA MUJIBU WA KAMUSI YA KISWAHILI SANIFU.

Ukisoma Kamusi ya Kiswahili sanifu ( TUKI) ya mwaka 2012 ukurasa wa 315 Msemo Nyege ni kunyegezana maana yake Wema ni mpaka uwe wa kutendeana
 
kashakuambia Andanenga yeye hatukani kamwe "NYEGE KUNYEGEZANA" maana yake "WEMA KUTENDEANA".



Mkuu, kwa yeyote aliyetunga hilo shairi na jinsi maneno hayo yalivyotumika, hapo bila shaka KATUKANA tu na hana utetezi wowote juu ya hilo, kwani hakuyaona hayo maneno mbadala "WEMA KUTENDEANA" hadi aandike ""NYEGE NYEGEZI"'??!!

Wewe unaweza kusoma shairi hilo mbele za wanao au wazazi wako??!!🤔🤔🤔
 
Ufafanuzi wa nyege ni kunyegezana katika Kiswahili
nyege ni kunyegezana | Ufafanuzi katika Kiswahili - Oxford Living Dictionaries



    • nyege ni kunyegezana
MSEMO
1wema ni mpaka uwe wa kutendeana.


Maana yake, wema wa kufanywa upande mmoja tu, si wema, ni unyonyaji na utumwa.

Kwa kweli "Nyege ni kunyegezana" ni msemo wa Kiswahili uliokuwepo miaka mingi kabla Amiri Akida "Sauti ya Kiza" Andanenga hajaandika shairi la jina hilo.Maana yake, gwiji wetu Andanenga hakujizushia tu kuandika shairi hilo, bila muongozo, alilitoa katika misemo ya Kiswahili.

Halafu msemo wa "Nyege ni kunyegezana" ni msemo mrefu sana, hata neno lenyewe "nyege" limekuwa over sexualized.Kwa tunaojua Kiswahili cha ndani, nyege ni tamaa fulani hivi, si lazima hata iwe ya sex.Yani ni hamu kubwa, mtu kusema "nina nyege na movie ya action leo" ni kitu cha kumaanisha nina hamu ya kuangalia movie ya action, nothing sexual.

Kwahiyo huo msemo wa "Nyege ni kunyegezana" ulivyokuwepo zama na zama, unaweza kuwa mpana sana, kumaanisha.

Kimsingi, msemo unasisitiza reciprocity and propagation

1. Habari ni kupashana
2. Mapenzi ni kupendana
3. Kazi ni kushirikiana
4. Familia ni kuzaliana
5.Shughuli ni kukaribishana
6. Chakula ni kugawana
7.Heshima ni kuheshimiana
9. Uzuri ni kukubaliana
10. Vicoba ni kukopeshana




Na hata, kutongoza ni kutongozana--- 😁😁😁

Je, leo Kauli hiyo inatumika "hasa" mahali gani??--- Lugha inapotumiwa ndipo inapokuwa pamoja na wakati (grow with time).

"Nyege kunyegezana" ni TUSI kubwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom