NYEGE NI KUNYEGEZANA wana JF kwanzia leo mnatakiwa mjue

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,070
3,718
KISWAHILI KITMU SANAHUKU NA KULE...-
Peni yangu Andanenga, uwino unapotona,
Mantiki huzilenga, na balagha na bayana
,Hufaidika malenga, huvurugika akina
,Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.Msemo wa Kiswahili, nyege ni kunyegezana
,Maana yaki kamili, “wema ni kutendeana’,
Wasiojua fasili, hunamba nimetukana
,Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ni msemo maarufu, ambao shaka hauna
,Kwenye kamusi sanifu, funueni mtaona
,Niwezeje kukashifu, nami mwana muungwana!
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ninataja ukurasa, wazi hapa naunena,
Soma mbili moja tisa, soma bila ya fitina,
Msemo siyo wa sasa, si juzi licha wa jana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ushairi kubwa fani, mithili yake haina,
Kujua zake bayani, yataka kikubwa kina
Muoneni mwafulani, hata kuku wamguna,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.Ulipotamkwa mlo, kaja akitunatuna,
Akakabwa koromelo, akabaki kugunaguna,
Kabakia lolololo, uzamani umechina
,Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.Alhaji Jitukali, pokea pongezi tena
,Kikubwa chako kilili, hapandi yule mtwana,
Atuache tule wali, yeye ugali wa dona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Kaditama wa Busara, na Mbwezi heko kijana
,Pongezi ndugu Kagera, Yobu has ante sana,
Ndimi Mshairi Bora, kipofu ninaeona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.(Mshairi Bora)Amiri A. S. Andanenga (Sauti ya Kiza)SLP 4775,Kinondoni ShambaDar es salaam.
 
Hayo mambo ya maloenga yanafuata nini huku MMU? Kwanini hukupeleka kwenye jukwaa mahsusi la lugha?
 
Hata kama ndivyo ila badooo vijana wa sasa wanasema kuna kasoro. kwa nini usingeonyesha shairi la kufa kufaana n.k kama unajidai mzee wa uadilifu. mkuu hapa umechemsha ilaumetuonyesha tu inside wewe umekaaje
 
KISWAHILI KITMU SANAHUKU NA KULE...-
Peni yangu Andanenga, uwino unapotona,
Mantiki huzilenga, na balagha na bayana
,Hufaidika malenga, huvurugika akina
,Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.Msemo wa Kiswahili, nyege ni kunyegezana
,Maana yaki kamili, �wema ni kutendeana�,
Wasiojua fasili, hunamba nimetukana
,Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ni msemo maarufu, ambao shaka hauna
,Kwenye kamusi sanifu, funueni mtaona
,Niwezeje kukashifu, nami mwana muungwana!
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ninataja ukurasa, wazi hapa naunena,
Soma mbili moja tisa, soma bila ya fitina,
Msemo siyo wa sasa, si juzi licha wa jana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ushairi kubwa fani, mithili yake haina,
Kujua zake bayani, yataka kikubwa kina
Muoneni mwafulani, hata kuku wamguna,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.Ulipotamkwa mlo, kaja akitunatuna,
Akakabwa koromelo, akabaki kugunaguna,
Kabakia lolololo, uzamani umechina
,Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.Alhaji Jitukali, pokea pongezi tena
,Kikubwa chako kilili, hapandi yule mtwana,
Atuache tule wali, yeye ugali wa dona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Kaditama wa Busara, na Mbwezi heko kijana
,Pongezi ndugu Kagera, Yobu has ante sana,
Ndimi Mshairi Bora, kipofu ninaeona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili

.(Mshairi Bora)Amiri A. S. Andanenga (Sauti ya Kiza)SLP 4775,Kinondoni ShambaDar es salaam.
Nyegezi ni stand ya mabasi yaendayo Mikoani na dalala iliyopo jijini mwanza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom