Shairi: Nyege ni kunyegezana by Andanenga

Neno NYEGE likisimama peke yake humaanisha kichocheo cha ngono, haibadiliki maana abadani.

Ila ikiwa NYEGE NI KUNYEGEZANA ndiyo humaanisha wema ni kutendeana.. Hii ni maana nzima ya methali, haitolewi maana kwa neno moja tu. Ukijaribu hivyo jua umemaanisha ashiki
Hata maana ya neno moja inatolewa,,nenda kwenye kamusi usome..nyege ni hamu ya kutenda jambo kwenye jamii.
 
Haiyaa haiyaa!

Wimbo wa Raymond/ Rayvany akimshirikisha Diamond Platnumz umezua tahanani na kuwafanya BASATA waingilie kati na kuupiga marufuku kwa kutumia kisingizio cha maadili.

Sungusungu wa maadili Tanzania hii hawaeshi kustaajabisha.

Sasa mimi Ngabu, nisiye na hili wala lile, nauliza tu hapa.

Shairi la yule gwiji mshairi, si mwingine yule bali Amiri Abdalah Sudi almaaruf kama Andanega, lijulikanalo kama ‘Nyege ni Kunyegezana, nalo liliwahi fungiwa na hawa mgambo wetu wa maadili ya Kitanzania?

Kama hujawahi lisikia au kulisoma hilo shairi, nakuwekea hapa.

Furahia utunzi murua kabisa wa gwiji Andanenga:

Peni yangu Andanenga, uwino unapotona,
Mantiki huzilenga, na balagha na bayana,
Hufaidika malenga, huvurugika akina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Msemo wa Kiswahili, nyege ni kunyegezana,
Maana yaki kamili, wema ni kutendeana,
Wasiojua fasili, hunamba nimetukana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ni msemo maarufu, ambao shaka hauna,
Kwenye kamusi sanifu, funueni mtaona,
Niwezeje kukashifu, nami mwana muungwana!
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ninataja ukurasa, wazi hapa naunena,
Soma mbili moja tisa, soma bila ya fitina,
Msemo siyo wa sasa, si juzi licha wa jana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ushairi kubwa fani, mithili yake haina,
Kujua zake bayani, yataka kikubwa kina
Muoneni mwafulani, hata kuku wamguna,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ulipotamkwa mlo, kaja akitunatuna,
Akakabwa koromelo, akabaki kugunaguna,
Kabakia lolololo, uzamani umechina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Alhaji Jitukali, pokea pongezi tena,
Kikubwa chako kilili, hapandi yule mtwana,
Atuache tule wali, yeye ugali wa dona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Kaditama wa Busara, na Mbwezi heko kijana,
Pongezi ndugu Kagera, Yobu has ante sana,
Ndimi Mshairi Bora, kipofu ninaeona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
(Mshairi Bora)

Amiri A. S. Andanenga (Sauti ya Kiza)
SLP 4775,
Kinondoni Shamba
Dar es salaam.

Jana ulikuwa na Mahaba.... au ulishikwa na Sulikhaa...:p:p:p

All the fingers...... hehehehehhehehe midoleee.
 
Wazee wa zamani walikuwa wajanja sana,ila vijana wa sasa akili zao wanazijua wenyewe
 
Kamusi ipo hapa jirani nami hata huyo mleta uzi nimemtumia picha kaona maana kamili. Sijui wewe unasemea kamusi ipi

Kwa nini unadhani nilikuwa sijui maana yake?

Nishakwambia kamusi za Kiswahili ninazo 10 na huwa nazisoma.

Maana ya huo msemo naijua tokea zamani.

Wewe hujanionyesha chochote ambacho nilikuwa sikijui.

Acha kujipa ujiko ambao huna!!

Unadhani ni wewe tu ndo mwenye kamusi ya Kiswahili??
 
Jana nilienda ofisi fulani za serikali. Nikakuta wahudumu wa pale wanagombania kurushiwa wimbo wa Rayvanny uliopigwa marufuku.
 
Haiyaa haiyaa!

Wimbo wa Raymond/ Rayvany akimshirikisha Diamond Platnumz umezua tahanani na kuwafanya BASATA waingilie kati na kuupiga marufuku kwa kutumia kisingizio cha maadili.

Sungusungu wa maadili Tanzania hii hawaeshi kustaajabisha.

Sasa mimi Ngabu, nisiye na hili wala lile, nauliza tu hapa.

Shairi la yule gwiji mshairi, si mwingine yule bali Amiri Abdalah Sudi almaaruf kama Andanega, lijulikanalo kama ‘Nyege ni Kunyegezana, nalo liliwahi fungiwa na hawa mgambo wetu wa maadili ya Kitanzania?

Kama hujawahi lisikia au kulisoma hilo shairi, nakuwekea hapa.

Furahia utunzi murua kabisa wa gwiji Andanenga:

Peni yangu Andanenga, uwino unapotona,
Mantiki huzilenga, na balagha na bayana,
Hufaidika malenga, huvurugika akina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Msemo wa Kiswahili, nyege ni kunyegezana,
Maana yaki kamili, wema ni kutendeana,
Wasiojua fasili, hunamba nimetukana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ni msemo maarufu, ambao shaka hauna,
Kwenye kamusi sanifu, funueni mtaona,
Niwezeje kukashifu, nami mwana muungwana!
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ninataja ukurasa, wazi hapa naunena,
Soma mbili moja tisa, soma bila ya fitina,
Msemo siyo wa sasa, si juzi licha wa jana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ushairi kubwa fani, mithili yake haina,
Kujua zake bayani, yataka kikubwa kina
Muoneni mwafulani, hata kuku wamguna,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ulipotamkwa mlo, kaja akitunatuna,
Akakabwa koromelo, akabaki kugunaguna,
Kabakia lolololo, uzamani umechina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Alhaji Jitukali, pokea pongezi tena,
Kikubwa chako kilili, hapandi yule mtwana,
Atuache tule wali, yeye ugali wa dona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Kaditama wa Busara, na Mbwezi heko kijana,
Pongezi ndugu Kagera, Yobu has ante sana,
Ndimi Mshairi Bora, kipofu ninaeona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
(Mshairi Bora)

Amiri A. S. Andanenga (Sauti ya Kiza)
SLP 4775,
Kinondoni Shamba
Dar es salaam.
Mediocrity everywhere, hivi ' kua na hamu na hamu ya mapenzi " ni tusi tangu lini? Watu wanasema oooh, huwezi kuimba mbele ya wazazi wako, yale tunayofundishwa darasa la tano mambo ya mavuzi na mikunndu unaweza sema mbele ya wazazi? Tena yapo kwenye mtaala kabisa. Sisi watanzania tuna fikra za kawaida sana yani.
 
Andanenga amenena lililo mwake moyoni
mwasema ametukana kwenu lipi lilo geni
nani hapa alo mwana mnalaumu kwanini
kiswahili lugha pana utamu wake lahajani

Tusi katukana nani alosema lipi baya
kipi ni tusi jamani tukisute bila haya
nijuze nipate amani kipi kimeleta haya
kiswahili lugha pana utamu wake lahajani
i wish i was a GIP ningetoa order unipe namba yako mara moja
 
Mkuu kiranga sijaona ubeti wako hapa

Nyege kitu asili, anazo na nyungunyungu
Nyege si za akili, katazo ni la mzungu
Nyege zi maadili, hamnazo kwa uvungu
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama

Nyege bila kuwepo, singekuwepo uzao
Nyege na yake michepo, zadumu kila uchao
Nyege zi na kicheko, na damu pata ugawo
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama

Babio na mamio, wametokana na nyege
Umbulo na amiyo, hawakujengwa kwa zege
Vipi uzungu salio, kututenga degedege?
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama

Nyege kunyegezana, kwa wema tukafanana
Twende kugezeana, sema hatutabanana
Vipi leo tunakwama, asili kuhamahama?
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama

Andanenga kaanzisha, mimi kuja kumaliza
Nyege nimeidhinisha, ukipata kumaa liza
Si jambo la kirihisha, ukidata unafiza
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama

Kalamu naweka chini, nimefika kaditama
Vijijini na mijini, tujitwike baba mama
Kazi yataka makini, uzazi dawamu kama
Nyege ni kunyegezana, kuiepuka kiama
 
Peni yangu Andanenga, uwino unapotona,
Mantiki huzilenga, na balagha na bayana,
Hufaidika malenga, huvurugika akina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Msemo wa Kiswahili, nyege ni kunyegezana,
Maana yaki kamili, wema ni kutendeana,
Wasiojua fasili, hunamba nimetukana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ni msemo maarufu, ambao shaka hauna,
Kwenye kamusi sanifu, funueni mtaona,
Niwezeje kukashifu, nami mwana muungwana!
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ninataja ukurasa, wazi hapa naunena,
Soma mbili moja tisa, soma bila ya fitina,
Msemo siyo wa sasa, si juzi licha wa jana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ushairi kubwa fani, mithili yake haina,
Kujua zake bayani, yataka kikubwa kina
Muoneni mwafulani, hata kuku wamguna,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Ulipotamkwa mlo, kaja akitunatuna,
Akakabwa koromelo, akabaki kugunaguna,
Kabakia lolololo, uzamani umechina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Alhaji Jitukali, pokea pongezi tena,
Kikubwa chako kilili, hapandi yule mtwana,
Atuache tule wali, yeye ugali wa dona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.

Kaditama wa Busara, na Mbwezi heko kijana,
Pongezi ndugu Kagera, Yobu has ante sana,
Ndimi Mshairi Bora, kipofu ninaeona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
(Mshairi Bora)

Amiri A. S. Andanenga (Sauti ya Kiza)
SLP 4775,
Kinondoni Shamba
Dar es salaam.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom