Shahidi: Sabaya aliniwekea Bastola mdomoni na kichwani kutaka kuniua

Hii taarifa imejikanganya sana....sasa sijui ni Muandishi au ndivyo ilivyo.

Mke wa Msangi akasema "aliona simu yake inaita ikiwa na jina Bakari Msangi" ina maana hivyo ndivyo alivyo save jina la Mumewe?.

Msangi aliingia ndani ya Gari akatoa simu alizokuwa amezificha, sasa ni vipi Msangi alipiga simu awali kumtaka Mkewe asiondoke kama simu alikuwa amezificha na alikuwa amefungwa Pingu mikononi na miguuni?.

Sina shaka kuhusu kutokea kwa hayo maovu yaliyomkuta Msangi na Mkewe ila nadhani Muandishi hapa si Mbobezi kuweka taarifa vizuri.
Wewe ni mumewe na bakari msangi au shemeji yake au jabulani wa sabaya?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Ukisikia ushahidi wa kutunga ndiyo huo. Hebu jiulize kaswali kadogo, kitu cha kwanza mtu makini unapomkamata mtuhumiwa, unasachiwa eti simu kaweka sehemu za nyeti? Uongo mtupu, eti amepigiwa simu na mume wake, kweli watu makini wakuache na simu uanze kuwapigia simu watu ili wakamatwe au kuja kushuhudia tukio kweli inakuja kichwani??? hao watakuwa siyo askari makini wakuache na vinasa sauti na kamera. Hebu wewe mama lete kapicha ka hayo matukio. Kweli dereva wako ashindwe hata kupiga kapicha kokote? eti nikawekewa bastora mdomoni nika kaa kimya?? hapo shida ingine hapo uongo uliokubuhu..
Ingekuwa unafuatilia hii kesi tangu awali ungeelewa kuhusu hizi simu. Ziliwahi kuelezewa hapo kabla
 
Hii taarifa imejikanganya sana....sasa sijui ni Muandishi au ndivyo ilivyo.

Mke wa Msangi akasema "aliona simu yake inaita ikiwa na jina Bakari Msangi" ina maana hivyo ndivyo alivyo save jina la Mumewe?.

Kumbuka shahidi na mwathirika wa unyama huo wa Sabaya ana jina la "Bakari Msangi". Ulitaka aseme, "....aliona simu yake inaita ikiwa na jina la 'my sweetheart?'...."

Mwisho wa siku angeulizwa tu na wakili wake swali hili ".…huyo sweetheart ndiye nani..?"
Msangi aliingia ndani ya Gari akatoa simu alizokuwa amezificha, sasa ni vipi Msangi alipiga simu awali kumtaka Mkewe asiondoke kama simu alikuwa amezificha na alikuwa amefungwa Pingu mikononi na miguuni?.
Wapi imesemwa alikuwa amefungwa pingu miguuni na mikononi? Soma vizuri. Hata Sabaya aliamuru aonane na mkewe. Hakusema alifunguliwa pingu kwanza. Hii ni ishara hakuwa amefungwa pingu. Alikuwa yuko chini ya ulinzi tu jamaa wakimtaka atoe pesa awape..!
Sina shaka kuhusu kutokea kwa hayo maovu yaliyomkuta Msangi na Mkewe ila nadhani Muandishi hapa si Mbobezi kuweka taarifa vizuri.
Si shida sana. Tumepata ujumbe vizuri. Lakini kumbuka pia hapa hatuko mahakamani kwamba tunaweza kufanyia cross examination ushahidi huo....

Hapa tumetaarifiwa kilichojiri mahakamani na kimeeleweka vyema kabisa tu. Mimi sijaona tatizo lolote...
 
Shahidi wa nane, Magdalene Mallya au Zulfa (32)Mkazi wa Sombetini jijini Arusha ameieleza mahakama jinsi alivyonusurika kuuawa Kwa kupigwa risasi na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya baada ya kuwekewa bastola kichwani na mdomoni .

Akitoa ushahidi wake Mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,katika kesi ya Unyang'anyi wa kutumia silaha na kupora Mali na fedha,inayomkabili Sabaya na wenzake wawili ,Zulfa ambaye ni mwalimu katika jiji la Arusha alisema alinusurika kuuawa Kwa bastola akiwa anamwokoa mumewe Bakari Msangi aliyekuwa ametekwa na Sabaya na Genge lake.

Akiongozwa na wakili Mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka alisema siku ya tukio Februari 9 mwaka huu,majira ya saa tano usiku mume wake Bakari Msangi alimpigia simu baada ya kutopatikana kwenye simu yake ya mkononi tangia majira ya saa 11 jioni na kumweleza kuwa ametekwa na Sabaya na kupigwa Sana na yupo chini ya ulinzi katika hotel ya Tulia iliyopo Sakina jijini Arusha.

Shahidi huyo ambaye alikuwa akiangua kilio kikubwa mara kwa mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake,alidai kuwa alimwomba jirani yake amsindikize katika hotel hiyo ya Tulia na baada ya kufika ndani ya hotel hiyo walikuta magari mengi yameegeshwa na kuwaona watu wakiwa wamesimama kwenye makundi matatu.

Alidai kuwa kundi la kwanza lilikuwa na vijana wawili wakiwa wameegemea gari ya Serikali na kundi la pili walikuwa wanne mmoja akiwa ameshika siku mkononi na mwingine akifanya mazoezi ya viungo huku kundi la tatu walikuwa wanne na wawili Kati yao walikuwa ameshikilia silaha aina ya bunduki kubwa Kila mmoja.

Alidai aliwauliza wale vijana kama Bakari Msangi(Mumewe) yupo eneo hilo lakini walimjibu kuwa hawamfahamu ndipo aliamua kuingia ndani ya hotel hiyo kuulizia mapokezi lakini alijibiwa kuwa kwenye orodha yao hakuna jina kama hilo.

Shahidi alidai kuwa alirejea katika gari lake na kushauriana na dereva wake waondoke eneo hilo lakini wakati wakijaribu kuondoa gari ndipo simu yake iliita na alipoipokea aliona jina la la Bakari Msangi ambaye alimwambia asiondoke kwani alikuwepo kwenye gari nyeupe ya Serikali akiwa amefungwa Pingu miguuni na Mikononi.

Alisema kijana mmoja kwenye yale makundi matatu alimfuata na kumuuliza amepata wapi habari kuwa Bakari Msangi yupo hapo ndipo alipomjibu kuwa simu yake ina GPS ndio iliyomwongoza kutambua kuwa yupo hapo.

Shahidi alidai kuwa baada ya muda mfupi Sabaya alitoka ndani ya hoteli hiyo na mkono wake wa kushoto aliomekama kushika bahasha kubwa ya Kaki na mkono wa kulia alikuwa ameshika bastola aliyokuwa akiichezea Kwa kuizungusha.

Alieleza kuwa Sabaya alimpita alipokuwa amesimama na kwenda kuongea na wale vijana waliokuwa kwenye vikundi na baadaye aliwaona wakitawanyika na kuingia kwenye magari ambayo yaliwashwa Kwa ajili ya kuondoka.

Alidai baada ya kuona Sabaya akiondoka na msafara wake alikimbia Mbele ya lango la kutokea katika hotel hiyo na kupiga magoti akiwa amenyanyua mikono juu huku akilia kwa sauti kubwa akimwambia Sabaya amwachie mume wake kwani alikuwa katika magari hayo.

Shahidi huyo ambaye wakati akitoa maelezo yake alikuwa akiangua kilio mara Kwa mara Kwa sauti kubwa mahakamani hapo alimlazimu wakili Kweka aliyekuwa akimhoji kumnyamazisha Kwa kumbembeleza .

Shahidi baada ya kunyamaza alidai kuwa Sabaya aliamuru Msangi ashushwe katika gari ili akazungumze na Mke wake kwenye gari lao.Baada ya kuingia ndani ya gari Msangi alitoa simu zake mbili alizokuwa ameficha sehemu za Siri na kumkabidhi Mkewe na baada ya dakika mchache kijana mmoja alikuja kuwagongea ndani ya gari na kumtaka Msangi atoke ili waondoke .

Shahidi alidai kuwa wakati Msangi akitoka ndani ya gari yao kuelekea kwenye gari la Sabaya ,alianza kulia kwa kupiga kelele akimwomba Sabaya amsamehe mume wake na Kama atakuwa na makosa ampeleke kituo Cha polisi.

Alidai kuwa Sabaya akiwa na hasira Kali alichomoa bastola na kumwekea kichwani huku akimwambia Malaya mkubwa wewe funga mdomo.

Shahidi alidai kuwa aliendelea kulia Kwa nguvu ndipo Sabaya alihamisha bastola kutoka kichwani na kumwekea mdomoni huku akimwambia Malaya wa wapi wewe,Malaya wenzake wanalilia pesa wewe unalilia mapenzi nitakumwaga ubongo.

Alisema kauli hiyo ilimwogopesha sana na kumfunga mdomo wake.

Ushahidi unaendelea..

Maelezo yote yanaonyesha kulikua na kazi ya kiserikali anafanya sabaya. Badala yake wahusika na makosa yaliyokua wanafuatiliwa hadi kufikishwa polisi ndio kwenye hii awamu eti walalamikaji wameibiwa na kunyang'anywa mali zao. Hao watu hawasemi kwa nini walikua wanafuatiliwa na dc wa hai na timu yake ya kamati ya ulinzi wa wilaya ya hai. Yaani mama kukubali kumsimamisha na kumdhalilisha dc sabaya ni kitu amekosea sana. Labda kama ana ajenda tofauti na magufuli.
 
Duh....
 
Kumbuka shahidi na mwathirika wa unyama huo wa Sabaya ana jina la "Bakari Msangi". Ulitaka aseme, "....aliona simu yake inaita ikiwa na jina la 'my sweetheart?'...."

Mwisho wa siku angeulizwa tu na wakili wake swali hili ".…huyo sweetheart ndiye nani..?"

Wapi imesemwa alikuwa amefungwa pingu miguuni na mikononi? Soma vizuri. Hata Sabaya aliamuru aonane na mkewe. Hakusema alifunguliwa pingu kwanza. Hii ni ishara hakuwa amefungwa pingu. Alikuwa yuko chini ya ulinzi tu jamaa wakimtaka atoe pesa awape..!

Shahidi alidai kuwa alirejea katika gari lake na kushauriana na dereva wake waondoke eneo hilo lakini wakati wakijaribu kuondoa gari ndipo simu yake iliita na alipoipokea aliona jina la la Bakari Msangi ambaye alimwambia asiondoke kwani alikuwepo kwenye gari nyeupe ya Serikali akiwa amefungwa Pingu miguuni na Mikononi.

Alisema kijana mmoja kwenye yale makundi matatu alimfuata na kumuuliza amepata wapi habari kuwa Bakari Msangi yupo hapo ndipo alipomjibu kuwa simu yake ina GPS ndio iliyomwongoza kutambua kuwa yupo hapo.

Shahidi alidai kuwa baada ya muda mfupi Sabaya alitoka ndani ya hoteli hiyo na mkono wake wa kushoto aliomekama kushika bahasha kubwa ya Kaki na mkono wa kulia alikuwa ameshika bastola aliyokuwa akiichezea Kwa kuizungusha.
Inashangaza kusema kwamba umesoma na kuelewa ili hali hujaona hata hiyo sehemu iliyoandikwa kufungwa pingu za mikono na miguu...sasa unaanza vipi ubishani kama hujasoma andiko vizuri?. huoni kwamba Muandishi ndio anawalenga watu wa sampuli yako msiozingatia hata kinachoandikwa?.

Sijui una maslahi gani na Mleta uzi lakini taarifa 'mliyoandika' hapo imekosa umakini na huo ndio ugomvi wangu, beleshi tuite beleshi.

Hayo yote unayojaribu kueleza ni hisia zako tu na si kulichoandikwa hapo. Sasa je ndivyo unavyotaka kila Msomaji aweke hisia zake?.

Mimi sio Muandishi kitaaluma lakini siamini kama hakuna namna nzuri ya kuandika taarifa inayoeleweka kabla ya kuipeleka kwa Wasomaji.

Huwa nasoma taarifa za kesi huko kwa Wenzetu na huwa kila kitu kinalezwa kwa umakini ili Msomaji aelewe na sio kuachiwa uweke hisia zako...hivi kwa mfano huoni tofauti ya kuandika "simu yake iliita akaona jina la Bakari Msangi" na kuandika "simu yake iliita na akaitambua ni namba ya mumewe"?.

Huu ni ushahidi Mahakamani, na kama inaelezwa kama Muandishi alivyoandika wewe huoni kama ni mkanganyiko?. Huoni kama Muandishi anapelekea Msomaji aone kwamba Mtoa ushahidi hayuko makini au hajui anachokisema?.

Walau basi Muandishi angetahadharisha kuwa yeye si Mweledi wa uandishi hivyo Msomaji asome kwa risk yake Mwenyewe au akatafute vyanzo vingine kwa taarifa iliyonyooka...au la basi angeacha kabisa kuandika ili Wengine waandike.
 
Duniani tunawafuga wanyama katili ndani ya mifumo ya vyama.Huyu jamaa alilelewa wapi?
Hizo silaha alikuwa anapewa na nani?
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama silaha zote zipo chini yake anachagua tu
 
Ukisikia ushahidi wa kutunga ndiyo huo. Hebu jiulize kaswali kadogo, kitu cha kwanza mtu makini unapomkamata mtuhumiwa, unasachiwa eti simu kaweka sehemu za nyeti? Uongo mtupu, eti amepigiwa simu na mume wake, kweli watu makini wakuache na simu uanze kuwapigia simu watu ili wakamatwe au kuja kushuhudia tukio kweli inakuja kichwani??? hao watakuwa siyo askari makini wakuache na vinasa sauti na kamera. Hebu wewe mama lete kapicha ka hayo matukio. Kweli dereva wako ashindwe hata kupiga kapicha kokote? eti nikawekewa bastora mdomoni nika kaa kimya?? hapo shida ingine hapo uongo uliokubuhu..
Sasa ni nani aliekuambia kuwa kina sabaya walikuwa watu makini? Wale walikuwa wanafanya vile kwa vile walikuwa na uhakika hakuna mamlaka yeyote itakayothubutu kuwahoji. Kwani hapo hotelini ni mafichoni?
 
Nimesoma matukio kadhaa ya abduction. Kuanzia kwa serial killers mpaka serial rapists na katika matukio yote mara nyingi mtenda tukio hua anaoverdo matukio ya mwanzoni. Mfano kamba atafunga kama vile hataki uheme hiyo ni namna yao ya kuhakikisha wanakudhibiti.

Tuje kwa Sabaya.

Tayari amemfunga mtu pingu mikononi na miguuni (overdo) halafu ameshindwa kuzuia access ya simu ili asiwasiliane na watu? Na maajabu ni kwamba mateka alipiga, hakutuma sms, alipiga simu.

Mara mbili.

Mateka alipiga simu mara mbili.

Akiwa ndani ya gari. Ambalo nje kuna watu wa Sabaya.

Stori iliyokuja JF ni kwamba Sabaya kapiga watu wawili akiwemo diwani, amewachukua na kuwapeleka kituoni.

Na picha tukaona.

Miaka mbele na video tukaona.

Kama ushahidi utakua unaongezwa chumvi mtuhumiwa atapeperuka
Kwahiyo unataka kusema hilo jambazi halikufanya hayo yanayoelezwa?
 
Yapo mambo utaeza tetea ukaelewa ila sio hili la Sabaya.
Wako walojitahidi kumtetea ila mwenendo wa kesi unavyoenda tayari wako ambao wameshaona mwanga wake.
Kama umkazi wa Arusha na unaongea jambo kama hili itabidi upimwe akili.
Hivi fikiria hadi Police wa kituo anadiriki kusema Hakuwa na namna ya kufanya mana alikuwa ni mteule wa raisi.
Huyu jamaa akichomoka Sidhani uraiyani anafikisha wiki.
Na ukumbuke hapo ni kesi za Arusha bado za wilayani Hai.
Mnajidanganya tu Mkuu, Sabaya anaweza kutoka na hakuna mtu wa kumfanya chochote. Makonda yupo uraiani anadunda tu mpaka leo hakuna aliyemuua,Magu alikuwa anadunda mitaani na hakuuliwa (angekuwepo mtu mwenye uwezo angemdungua tu)
 
Maelezo yote yanaonyesha kulikua na kazi ya kiserikali anafanya sabaya. Badala yake wahusika na makosa yaliyokua wanafuatiliwa hadi kufikishwa polisi ndio kwenye hii awamu eti walalamikaji wameibiwa na kunyang'anywa mali zao. Hao watu hawasemi kwa nini walikua wanafuatiliwa na dc wa hai na timu yake ya kamati ya ulinzi wa wilaya ya hai. Yaani mama kukubali kumsimamisha na kumdhalilisha dc sabaya ni kitu amekosea sana. Labda kama ana ajenda tofauti na magufuli.

..SERIKALI ndio inayomshtaki Sabaya.

..Na huo ni ushahidi kwamba aliyokuwa akiyafanya hayakuwa maelekezo ya serikali.

..Sabaya alitoka wilaya ya Hai ambako ni kituo chake cha kazi, na kwenda kufanya tukio ktk wilaya nyingine, na kituo cha kazi cha DC mwingine.
 
Huwezi kuelewa ukianzia katikati,cm alipewa na dreva akaficha sehemu za siri.Fukunyua mwanzo mwa tukio utaelewa mtiririko wote.Uliwahi lazimisha machozi yatoke bila uchungu ?
Kaficha simu sehemu za siri huku akiwa kafungwa pingu za mikono na miguu halafu akaweza kuitoa simu hiyo na kumpigia mkewe?hao watesi wanamuangalia tu
Ndio maana sisi wapenzi wa somo la sheria tunaamini sana mahakama
 
huvi ni kweli?
Shahidi alidai kuwa baada ya muda mfupi Sabaya alitoka ndani ya hoteli hiyo na mkono wake wa kushoto aliomekama kushika bahasha kubwa ya Kaki na mkono wa kulia alikuwa ameshika bastola aliyokuwa akiichezea Kwa kuizungusha.

Kama movie za kijambazi
 
Shahidi wa nane, Magdalene Mallya au Zulfa (32)Mkazi wa Sombetini jijini Arusha ameieleza mahakama jinsi alivyonusurika kuuawa Kwa kupigwa risasi na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya baada ya kuwekewa bastola kichwani na mdomoni .

Akitoa ushahidi wake Mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,katika kesi ya Unyang'anyi wa kutumia silaha na kupora Mali na fedha,inayomkabili Sabaya na wenzake wawili ,Zulfa ambaye ni mwalimu katika jiji la Arusha alisema alinusurika kuuawa Kwa bastola akiwa anamwokoa mumewe Bakari Msangi aliyekuwa ametekwa na Sabaya na Genge lake.

Akiongozwa na wakili Mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka alisema siku ya tukio Februari 9 mwaka huu,majira ya saa tano usiku mume wake Bakari Msangi alimpigia simu baada ya kutopatikana kwenye simu yake ya mkononi tangia majira ya saa 11 jioni na kumweleza kuwa ametekwa na Sabaya na kupigwa Sana na yupo chini ya ulinzi katika hotel ya Tulia iliyopo Sakina jijini Arusha.

Shahidi huyo ambaye alikuwa akiangua kilio kikubwa mara kwa mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake,alidai kuwa alimwomba jirani yake amsindikize katika hotel hiyo ya Tulia na baada ya kufika ndani ya hotel hiyo walikuta magari mengi yameegeshwa na kuwaona watu wakiwa wamesimama kwenye makundi matatu.

Alidai kuwa kundi la kwanza lilikuwa na vijana wawili wakiwa wameegemea gari ya Serikali na kundi la pili walikuwa wanne mmoja akiwa ameshika siku mkononi na mwingine akifanya mazoezi ya viungo huku kundi la tatu walikuwa wanne na wawili Kati yao walikuwa ameshikilia silaha aina ya bunduki kubwa Kila mmoja.

Alidai aliwauliza wale vijana kama Bakari Msangi(Mumewe) yupo eneo hilo lakini walimjibu kuwa hawamfahamu ndipo aliamua kuingia ndani ya hotel hiyo kuulizia mapokezi lakini alijibiwa kuwa kwenye orodha yao hakuna jina kama hilo.

Shahidi alidai kuwa alirejea katika gari lake na kushauriana na dereva wake waondoke eneo hilo lakini wakati wakijaribu kuondoa gari ndipo simu yake iliita na alipoipokea aliona jina la la Bakari Msangi ambaye alimwambia asiondoke kwani alikuwepo kwenye gari nyeupe ya Serikali akiwa amefungwa Pingu miguuni na Mikononi.

Alisema kijana mmoja kwenye yale makundi matatu alimfuata na kumuuliza amepata wapi habari kuwa Bakari Msangi yupo hapo ndipo alipomjibu kuwa simu yake ina GPS ndio iliyomwongoza kutambua kuwa yupo hapo.

Shahidi alidai kuwa baada ya muda mfupi Sabaya alitoka ndani ya hoteli hiyo na mkono wake wa kushoto aliomekama kushika bahasha kubwa ya Kaki na mkono wa kulia alikuwa ameshika bastola aliyokuwa akiichezea Kwa kuizungusha.

Alieleza kuwa Sabaya alimpita alipokuwa amesimama na kwenda kuongea na wale vijana waliokuwa kwenye vikundi na baadaye aliwaona wakitawanyika na kuingia kwenye magari ambayo yaliwashwa Kwa ajili ya kuondoka.

Alidai baada ya kuona Sabaya akiondoka na msafara wake alikimbia Mbele ya lango la kutokea katika hotel hiyo na kupiga magoti akiwa amenyanyua mikono juu huku akilia kwa sauti kubwa akimwambia Sabaya amwachie mume wake kwani alikuwa katika magari hayo.

Shahidi huyo ambaye wakati akitoa maelezo yake alikuwa akiangua kilio mara Kwa mara Kwa sauti kubwa mahakamani hapo alimlazimu wakili Kweka aliyekuwa akimhoji kumnyamazisha Kwa kumbembeleza .

Shahidi baada ya kunyamaza alidai kuwa Sabaya aliamuru Msangi ashushwe katika gari ili akazungumze na Mke wake kwenye gari lao.Baada ya kuingia ndani ya gari Msangi alitoa simu zake mbili alizokuwa ameficha sehemu za Siri na kumkabidhi Mkewe na baada ya dakika mchache kijana mmoja alikuja kuwagongea ndani ya gari na kumtaka Msangi atoke ili waondoke .

Shahidi alidai kuwa wakati Msangi akitoka ndani ya gari yao kuelekea kwenye gari la Sabaya ,alianza kulia kwa kupiga kelele akimwomba Sabaya amsamehe mume wake na Kama atakuwa na makosa ampeleke kituo Cha polisi.

Alidai kuwa Sabaya akiwa na hasira Kali alichomoa bastola na kumwekea kichwani huku akimwambia Malaya mkubwa wewe funga mdomo.

Shahidi alidai kuwa aliendelea kulia Kwa nguvu ndipo Sabaya alihamisha bastola kutoka kichwani na kumwekea mdomoni huku akimwambia Malaya wa wapi wewe,Malaya wenzake wanalilia pesa wewe unalilia mapenzi nitakumwaga ubongo.

Alisema kauli hiyo ilimwogopesha sana na kumfunga mdomo wake.

Ushahidi unaendelea..

Shahidi alidai kuwa aliendelea kulia Kwa nguvu ndipo Sabaya alihamisha bastola kutoka kichwani na kumwekea mdomoni huku akimwambia Malaya wa wapi wewe,Malaya wenzake wanalilia pesa wewe unalilia mapenzi nitakumwaga ubongo.
 
Le jenerali... Le Grande Ole Sabaya.... Chumaaaaa!!!

Hawa ndo Magaidi sasa! Maaaninah
Shahidi alidai kuwa aliendelea kulia Kwa nguvu ndipo Sabaya alihamisha bastola kutoka kichwani na kumwekea mdomoni huku akimwambia Malaya wa wapi wewe,Malaya wenzake wanalilia pesa wewe unalilia mapenzi nitakumwaga ubongo.
 
Serikali ya Magufuli ilikuwa ni Serikali ya kigaidi.

Kibaya zaidi mkuu ni kwamba bado tunao watu wa aina hiyo na wapo kwenye system. Kuna yule mjinga mmoja anaitwa kenan aliwahi kusema Iringa hadharani kwamba wapinzani wanaoipinga serikali ya hayati wanapaswa kuuwawa. Baada ya hapo alipandishwa cheo na kupewa UDC infact kuna sehemu pia anatajwa kwenye ushahidi kwenye kesi ya mwanaharamu Sabaya.

Jana mjinga huyu bila aibu amesema kuna watu walifurahia kukamatwa kwa sabaya kwanini wanapinga kukamatwa kwa Mbowe? Tumefanya siasa ambao ni uhai wa watanzania kuwa kama Simba na Yanga kweli kbs????!!! Kiongozi wa kitaifa bila kujali chama gani unaongeaje haya hadharani bila aibu? Mimi ninajiuliza kila siku hivi tumefikaje kwenye levels za kijinga hivi kama nchi?
 
Back
Top Bottom