Shahidi: Sabaya aliniwekea Bastola mdomoni na kichwani kutaka kuniua

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Shahidi wa nane, Magdalene Mallya au Zulfa (32)Mkazi wa Sombetini jijini Arusha ameieleza mahakama jinsi alivyonusurika kuuawa Kwa kupigwa risasi na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai ole Sabaya baada ya kuwekewa bastola kichwani na mdomoni .

Akitoa ushahidi wake Mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,katika kesi ya Unyang'anyi wa kutumia silaha na kupora Mali na fedha,inayomkabili Sabaya na wenzake wawili ,Zulfa ambaye ni mwalimu katika jiji la Arusha alisema alinusurika kuuawa Kwa bastola akiwa anamwokoa mumewe Bakari Msangi aliyekuwa ametekwa na Sabaya na Genge lake.

Akiongozwa na wakili Mkuu wa Serikali, Tumaini Kweka alisema siku ya tukio Februari 9 mwaka huu,majira ya saa tano usiku mume wake Bakari Msangi alimpigia simu baada ya kutopatikana kwenye simu yake ya mkononi tangia majira ya saa 11 jioni na kumweleza kuwa ametekwa na Sabaya na kupigwa Sana na yupo chini ya ulinzi katika hotel ya Tulia iliyopo Sakina jijini Arusha.

Shahidi huyo ambaye alikuwa akiangua kilio kikubwa mara kwa mahakamani hapo wakati akitoa ushahidi wake,alidai kuwa alimwomba jirani yake amsindikize katika hotel hiyo ya Tulia na baada ya kufika ndani ya hotel hiyo walikuta magari mengi yameegeshwa na kuwaona watu wakiwa wamesimama kwenye makundi matatu.

Alidai kuwa kundi la kwanza lilikuwa na vijana wawili wakiwa wameegemea gari ya Serikali na kundi la pili walikuwa wanne mmoja akiwa ameshika siku mkononi na mwingine akifanya mazoezi ya viungo huku kundi la tatu walikuwa wanne na wawili Kati yao walikuwa ameshikilia silaha aina ya bunduki kubwa Kila mmoja.

Alidai aliwauliza wale vijana kama Bakari Msangi(Mumewe) yupo eneo hilo lakini walimjibu kuwa hawamfahamu ndipo aliamua kuingia ndani ya hotel hiyo kuulizia mapokezi lakini alijibiwa kuwa kwenye orodha yao hakuna jina kama hilo.

Shahidi alidai kuwa alirejea katika gari lake na kushauriana na dereva wake waondoke eneo hilo lakini wakati wakijaribu kuondoa gari ndipo simu yake iliita na alipoipokea aliona jina la la Bakari Msangi ambaye alimwambia asiondoke kwani alikuwepo kwenye gari nyeupe ya Serikali akiwa amefungwa Pingu miguuni na Mikononi.

Alisema kijana mmoja kwenye yale makundi matatu alimfuata na kumuuliza amepata wapi habari kuwa Bakari Msangi yupo hapo ndipo alipomjibu kuwa simu yake ina GPS ndio iliyomwongoza kutambua kuwa yupo hapo.

Shahidi alidai kuwa baada ya muda mfupi Sabaya alitoka ndani ya hoteli hiyo na mkono wake wa kushoto aliomekama kushika bahasha kubwa ya Kaki na mkono wa kulia alikuwa ameshika bastola aliyokuwa akiichezea Kwa kuizungusha.

Alieleza kuwa Sabaya alimpita alipokuwa amesimama na kwenda kuongea na wale vijana waliokuwa kwenye vikundi na baadaye aliwaona wakitawanyika na kuingia kwenye magari ambayo yaliwashwa Kwa ajili ya kuondoka.

Alidai baada ya kuona Sabaya akiondoka na msafara wake alikimbia Mbele ya lango la kutokea katika hotel hiyo na kupiga magoti akiwa amenyanyua mikono juu huku akilia kwa sauti kubwa akimwambia Sabaya amwachie mume wake kwani alikuwa katika magari hayo.

Shahidi huyo ambaye wakati akitoa maelezo yake alikuwa akiangua kilio mara Kwa mara Kwa sauti kubwa mahakamani hapo alimlazimu wakili Kweka aliyekuwa akimhoji kumnyamazisha Kwa kumbembeleza .

Shahidi baada ya kunyamaza alidai kuwa Sabaya aliamuru Msangi ashushwe katika gari ili akazungumze na Mke wake kwenye gari lao.Baada ya kuingia ndani ya gari Msangi alitoa simu zake mbili alizokuwa ameficha sehemu za Siri na kumkabidhi Mkewe na baada ya dakika mchache kijana mmoja alikuja kuwagongea ndani ya gari na kumtaka Msangi atoke ili waondoke .

Shahidi alidai kuwa wakati Msangi akitoka ndani ya gari yao kuelekea kwenye gari la Sabaya ,alianza kulia kwa kupiga kelele akimwomba Sabaya amsamehe mume wake na Kama atakuwa na makosa ampeleke kituo Cha polisi.

Alidai kuwa Sabaya akiwa na hasira Kali alichomoa bastola na kumwekea kichwani huku akimwambia Malaya mkubwa wewe funga mdomo.

Shahidi alidai kuwa aliendelea kulia Kwa nguvu ndipo Sabaya alihamisha bastola kutoka kichwani na kumwekea mdomoni huku akimwambia Malaya wa wapi wewe,Malaya wenzake wanalilia pesa wewe unalilia mapenzi nitakumwaga ubongo.

Alisema kauli hiyo ilimwogopesha sana na kumfunga mdomo wake.

Ushahidi unaendelea..


IMG_20210806_091156_874.jpg
 
Hilo Sabaya halistahili kuishi kabisa bora polisi wangelimaliza halafu waje maelezo mafupi tu kwamba lilijaribu kutoroka na walilidhibiti kwa kumpiga risasi ya mguu lakini kwa bahati mbaya wakati wanaliharikisha hospitali likafia njiani.
 
Hii taarifa imejikanganya sana....sasa sijui ni Muandishi au ndivyo ilivyo.

Mke wa Msangi akasema "aliona simu yake inaita ikiwa na jina Bakari Msangi" ina maana hivyo ndivyo alivyo save jina la Mumewe?.

Msangi aliingia ndani ya Gari akatoa simu alizokuwa amezificha, sasa ni vipi Msangi alipiga simu awali kumtaka Mkewe asiondoke kama simu alikuwa amezificha na alikuwa amefungwa Pingu mikononi na miguuni?.

Sina shaka kuhusu kutokea kwa hayo maovu yaliyomkuta Msangi na Mkewe ila nadhani Muandishi hapa si Mbobezi kuweka taarifa vizuri.
 
Ukisikia ushahidi wa kutunga ndiyo huo. Hebu jiulize kaswali kadogo, kitu cha kwanza mtu makini unapomkamata mtuhumiwa, unasachiwa eti simu kaweka sehemu za nyeti? Uongo mtupu, eti amepigiwa simu na mume wake, kweli watu makini wakuache na simu uanze kuwapigia simu watu ili wakamatwe au kuja kushuhudia tukio kweli inakuja kichwani??? hao watakuwa siyo askari makini wakuache na vinasa sauti na kamera. Hebu wewe mama lete kapicha ka hayo matukio. Kweli dereva wako ashindwe hata kupiga kapicha kokote? eti nikawekewa bastora mdomoni nika kaa kimya?? hapo shida ingine hapo uongo uliokubuhu..
 
Back
Top Bottom