Shahidi kesi ya Sabaya aieleza mahakama alivyotoa Sh90 milioni

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
5,079
8,219
Mfanyabiashara Francis Mrosso (44) anayedaiwa kuombwa rushwa ya Sh 90 milioni na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, ameanza kutoa ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, akidai kuwa alitishiwa asipotoa fedha hizo atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.

Leo Novemba 22, 2021 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Patricia Kisinda, Mrosso ambaye ni mmiliki wa gereji ya kutengeneza magari ya Mrosso Injector Pump na fundi magari, ameanza kutoa ushahidi wake wa msingi akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tarsila Gervas.

Katika kesi hiyo Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashtaka matano wanayodaiwa kuyatenda Januari 22, 2021 jijini Arusha.

Shahidi huyo ameieleza Mahakamana namna Sabaya na vijana wake walimtishia na kumtaka awapatie Sh90 milioni ambazo alidai kumpatia moja ya vijana hao wa Sabaya baada ya kuzitoa benki ya CRDB tawi la Kwa Mromboo jijini Arusha.

Mrosso amedai kuwa Sabaya na wenzake walimtishia kuwa anakwepa kodi ya Serikali kwa kuingiza spea za magari kwa njia ya panya huku akimtishia kuwa atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi ambayo haina dhamana.

Amedai kuwa alipata woga baada ya kuelezwa maneno hayo ambapo pia alilazimika kutoa fedha hizo kwa sababu Sabaya alimweleza aispotoa wataondoka naye.

Hakimu anayesikiliza kesi hiyo ameiahirisha hadi kesho Novemba 23, 2021 ambapo Mrosso ataendelea kutoa ushahidi wake wa msingi kabla ya kuanza kuhojiwa na mawakili wa utetezi.

Katika kesi hiyo watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Mwananchi
 
Sie tuliokulia Uswahilini, maisha yetu especially enzi hizo tunayajua wenyewe!!

Hapo mnakuta watoto mmecheza kutwa nzima hadi lunch imewapita!!

Unafika home, unakuta patupu! Inawezekana wakati wa msosi uliitwa lakini michezo ilikuzidi, au watu waliamua tu kukufanyia ubandidu!

Basi bhana, hapo njaa ishaanza kuwatafuna, basi utasikiadua za watoto wa Uswahilini --

"je, mara tu tunaona gari ya soda na mikate zinagongana"

"Mara tunaona Mungu anashusha pilau na kuku pamoja na soda za fanta"

Hatimae unafika umuda wa dua kutoka kwa toto boya boya linalojichanganya na watukutu, huyu nae anakuja na dua zake

"Je, mara Mungu anaturushia juishi na bishkuti"

Nikifikiria hayo, ndipo kwa mbaaaaaaali ninapomuona Sabaya na na dua yake...

"Mara pah! JPM huyooo amefufuka, anarudi tena Ikulu na kumtimua Samia"
 
Sabaya hakuwa jambazi,alikuwa wakala tu.
Jambazi mkuu tunaye na ataendekea kwa njia mbadala.
NB! Sabaya hakuwa jambazi.
Pia kwa hisia zangu anaumizwa bila sababu.
Jambazi mkuu ni aliyemteua na kumkingia kifua, atakuja kumtaja atapopewa nafasi ya kujitetea
 
Hizi kesi ni kutuzubaisha tu ...MAMA NA MAKAMBA wana-saini tu Mikataba ya ajabu ajabu huko mlango wa nyuma

D70C0393-24A8-41E4-AC50-546AECEC0ADB.jpeg
 
Nilikua nashangaa sana nikimuona kanisani akipiga magoti kwa unyenyekevu wa kinafiki.Mungu fundi aisee.
Jamaa alikuwa ni mnafiki aliyekubuhu, Jumamosi anabambikia mahasimu wake kesi ya uhujumu uchumi, next day anaenda kanisani kushiriki ekaristi na kujifanya mtu mwema sana
 
Hizi kesi ni kutuzubaisha tu ...MAMA NA MAKAMBA wana-saini tu Mikataba ya ajabu ajabu huko mlango wa nyuma
Hiyo mikataba haitakua siri milele itaanikwa tu na watakaokuja. Ila hawa wahuni walijipachika jina la uzalendo lazima washughulikiwe ipasavyo
 
Mfanyabiashara Francis Mrosso (44) anayedaiwa kuombwa rushwa ya Sh 90 milioni na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, ameanza kutoa ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, akidai kuwa alitishiwa asipotoa fedha hizo atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.
Kwa nini hawakuripoti wakati ule takukuru badala yake wakaamua kutoa hiyo rushwa? Njama hizo za kizandiki dhidi ya mwanamapinduzi hazitafaulu mwisho haki itatendekeka. Kwanza rushwa ina pande mbili hao watoaji wanajiamini nini maana wao hawaburuzwi mahakamani.
 
Back
Top Bottom